Posts

Showing posts from June, 2015

Millem Magese atunukiwa tuzo ya heshima ya Global Good ya BET Awards 2015

Image
Miss Tanzania, 2001, Happiness Millen Magese, hatimaye ametunukiwa tuzo ya kwanza ya heshima ya Global Good ya BET Awards 2015. Millen amepewa tuzo hiyo kutokana na jitihada zake za kampeni ya ugonjwa wa endometriosis ambao pia amekuwa nao katika maisha yake yote tangu awe msichana. Tatizo hilo limempelekea kuwa mgumba. Pamoja na hivyo Millen amekuwa mstari wa mbele kutoa misaada mbalimbali kwa wasiojiweza.

Tuzo za BET 2015 zimeshatolewa tayari, list yote ya washindi ipo hapa

Image
Tuzo za  BET Awards 2015  zilichukua headlines kubwa siku ya jumapili tarehe 28 June 2015  Los Angeles  Marekani  ambapo mc alikua ni  Anthony Anderson  na  Trace Ellis Rose. Wakali wa muziki kama  Chris Brown ,  Nicki Minaj , na  Rihanna  na wengine walimiliki stage kwa kuperform.  Janet Jackson  pamoja na  Smokey Robinson  walikua baadhi ya watu waliopewa tuzo za heshima mwaka huu na  BET . Hapa chini nimekusogezea orodha kamili ya wale wakali wote waliopokea tuzo ya  BET Award  mwaka huu wachache wakiwemo  Beyonce   akiongoza na tuzo 3,  Nicki Minaj akiwa na 2,  Kendrick Lamar, Big Sean, Chris Brown, John Legend   wakiwa na tuzo moja kila mmoja na kwenye kile kipengele cha  International Best Act: Africa Stonebwoy  kutoka  Ghana  aibuka kidedea. Best International Act: Africa; Stonebwoy (Ghana) Hii hapa ndio orodha kamili ya wasanii wote waliopokea tuzo za  BET Award , karibu uitazame  Best International Act UK: FKA Twigs Fuse ODG Lethal Bizzle Little Simz

Mfungwa aliyetoroka New York akamatwa

Image
David Sweat aliyekamatwa baada ya kutoroka gerezani katika jimbo la New York alikokuwa akitumikia adhabu ya kifungo kutokana na makosa ya mauaji Polisi nchini Marekani wamempiga risasi na kumkamata mfungwa aliyetoroka gerezani katika jimbo la New York alikokuwa amefungwa kutumikia adhabu kutokana na makosa ya mauaji wiki tatu zilizopita. David Sweat alikamatwa karibu na mpaka wa Canada baada ya afisa wa polisi kumng'amua akifanya mazoezi ya kukimbia kando ya barabara. Mfungwa mwenzake aliyetoroka Richard Matt aliuawa na polisi Ijumaa. Watu hao wawili walitumia zana imara kuweza kutoroka kutoka gereza lenye ulinzi mkali la Clinton na kusababisha msako mkubwa wa polisi kufanyika. Gavana wa jimbo la New York, Andrew Cuomo, amesema jinamizi la wahalifu hao limekwisha. Chanzo:BBC

Lumia ya window 10 yaingia kitaani

Image
  Meneja wa Bidhaa wa Kampuni ya Microsoft Kingori Gitahi akizungumza na vyombo vya habari (havipo pichani) wakati wa uzinduzi wa simu tatu aina ya Lumia jijini Dar es Saalaam. Na Modewji blog team Meneja wa Bidhaa wa Kampuni ya Microsoft Kingori Gitahi  amewataka watumiaji wa simu za mkononi za Smartphone kuacha kuzitumia kwa kusoma barua pepe pekee na kuzifanyisha shughuli za kuzalisha mali. Akizungumza kwenye mkutano na waandishi wa habari hivi karibuni wakati wa uzinduzi wa simu tatu aina ya Lumia,alisema kuwa simu za Smartphone zina huduma mbalimbali ambazo zinaweza kutumiwa kwa faida, zaidi ya kupokea na kutuma barua pepe. Alisema kuwa  katika kuhakikisha kuwa wateja wa kampuni hiyo wananufaika  na huduma za Microsoft kwa sasa imeingiza sokoni simu aina ya Lumia 540, lumia 640 exel na Lumia 430. Kingori Gitahi alisema kuwa kampuni hiyo imeingiza sokoni bidhaa hizo ikiwa ni sehemu ya mikakati yake ya kuwatumikia wateja wake kwa kuwapa huduma bora zaidi za mawasilia

AU YAJIWEKA KANDO UCHAGUZI WA BURUNDI

Image
Makao makuu ya Umoja wa Afrika, Addis Ababa,Ethiopia Umoja wa Afrika umesema hautawapeleka waangalizi wake wa uchaguzi katika uchaguzi wa wabunge wa Burundi utakaofanyika Jumatatu kwa sababu masharti ya uchaguzi huru na wa haki hayajazingatiwa. Vyama vya upinzani vimesusia uchaguzi wakipinga uamuzi wa Rais Pierre Nkurunziza wa kugombea muhula wa tatu katika uchaguzi wa rais mwezi ujao. Mapema Jumapili, Spika wa bunge la Burundi Pie Ntavyohanyuma alisema alikimbia nchi yake kwa sababu ya kuhofia usalama wa maisha yake baada ya kumshauri rais asigombee tena. Jaribio la Bwana Nkurunziza kupata muhula wa tatu limekumbana na wimbi la ghasia ambapo zaidi ya watu sabini wameuawa. BBC

MOTO WAJERUHI 500 NCHINI TAIWAN

Image
Majeruhi katika ajali hiyo wakipatiwa huduma ya kwanza. WATU zaidi ya 500 wamejeruhiwa kufuatia kutokea mlipuko na moto kwenye bustani moja ya burudani nchini Taiwan mapema jana.  Rais wa Taiwan, Ma Ying-jeou (katikati) akiongea na mmoja wa majeruhi aliyelazwa hospitalini baada ya ajali hiyo

KAMANDA MALISA GODLISTEN,AONYESHA NIA YA DHATI YA KULITETEA JIMBO LA MOSHI VIJIJINI KWA KUKOSA MBUNGE WA KULISEMA KWA MIAKA 10

Image
MOSHI VIJIJINI INANIHITAJI - MALISA.! Kamanda Malisa akirudisha fomu UTANGULIZI: Kwa takribani miaka 10 sasa jimbo la Moshi Vijijini limekuwa "iddle" kutokana na kukosa mbunge wa kulisemea. Mbunge aliyepo Dr.Cyril Chami aliteuliwa kuwa Naibu Waziri na baadae Waziri muda mfupi tu baada ya kuchaguliwa (kabla hajaachwa nje ya baraza). Nafasi ya uwaziri imemfanya Chami ashindwe kuwajibika vizuri kwa wananchi wake, kwa sababu akiwa kama Mbunge hawezi kuiwajibisha serikali ambayo yeye ni sehemu yake (Nemo judex in causa sua). Changamoto za Moshi vijijini ni nyingi, hivyo ni dhahiri jimbo hili linamhitaji mtu shupavu anayeweza kulitetea kwa "nguvu ya hoja" na "hoja za nguvu" ktk kusukuma mbele gurudumu la maendeleo. KWANINI NAOMBA RIDHAA YA KUGOMBEA; Kabla sijatangaza azma hii nilijiuliza sana maswali mengi na kushirikisha watu wangu wa karibu kunishauri. Lengo ni kuwa sikutaka lengo langu langu la kuomba ridhaa ya kugombea lichukuliwe tof

ANGALIA MISHONO MIPYA YA KITENGE 2015!!! IKO BOMBA SANA INAWAHUSU WOTE, BADILIKA KUWA MPYA

Image
chanzo: hopeiringa.                  #Elimtaamitindo