Posts

KISWAHILI CHAZIDI KUSHIKA KASI MPAKA MTONI

Image
Nas Damian Marley: Watupia Kiswahili kwenye ngoma yao Katika kile kinachoonesha kwamba Lugha yetu ya Taifa a.k.a Kiswahili inaendelea kupasua anga ulimwenguni, mastaa wawili wa muziki wa Hip Hop Marekani, Nas Escoba na mtoto wa Hayati Bob Marley, Damian Marley wameitupia lugha hiyo kwenye ngoma yao yenye jina la As We Enter. Washkaji hao ambao wamesimama vyema kwenye kolabo hiyo ya ukweli ambayo wameimba kwa kupokezana wametumia maneno ya kiswahili kama “Habari gani”, “Nzuri sana” na kuifanya lugha yetu kutambulika na mataifa mbalimbali duniani. Zaidi icheki ngoma hiyo hapo pembeni huku maneno ya kiswahili yakiwa yamewekewa mishale.

Wanachuo DSJ wabakwa kwa zamu

Kundi la vibaka zaidi ya 15 limevamia wanachuo wa kike wanaolala katika hosteli ya Chuo cha Uandishi wa Habari Dar es Salaam (DSJ) iliyoko Ilala, Dar es Salaam na kuwabaka kwa zamu. Wakizungumza na MTANZANIA kwa sharti la kutotaja majina yao, baadhi ya wanachuo waliovamiwa walisema kuwa, vibaka hao waliwavamia juzi majira ya saa nane usiku. “Sisi tulikuwa tumelala kama kawaida, ilipotimia majira ya saa nane za usiku, tukasikia kelele nje ya geti ambazo zilionyesha kuwa mlinzi wetu Mmasai alikuwa ametekwa na hao vibaka. “Baada ya vurugu za muda mrefu kidogo, inaonekana mlinzi alizidiwa nguvu, akafungwa kamba miguuni na mikononi na kulazwa chini. Walipomalizika zoezi hilo, wakaja chumbani kwetu, mimi nilikuwa nilelala na mwenzangu, wakagonga mlango kwa nguvu wakitutaka tufungue. “Sisi tukakataa kufungua, wakaanza kututishia kwamba kama tumegoma kufungua mlango basi watauvunja na wakiingia ndani watatuua ama watatufanyia kitendo kibaya sana ambacho hatutasahau maishani. “Tuliposikia hivyo

FACEBOOK INTRODUCES 'LIKE' FEATURE IN COMMENTS TOO

Until yesterday, we were used to have the "like" feature only in the status message but not in the comment section. Starting today, Facebook has introduced "like" feature in both the statuses and comments. Why cheer up for this? Well, if there one thing or two that I disliked was having to reply to every single comment that came under my status message; or having to write back a comment to 'thank' as an appreciation for someone leaving a comment on my status message or comment. It reached a time I'd wait and give it time to see how many people responded before I could thank them all in one post. What else? Remember when you liked one's comment but didn't really want to say anything and wished you could just click under their comment to show that you liked it? With this feature we are going to see less repetitive comments thus less 'inbox notification' and therefore a bit cleaner 'inbox'. You only have to click "like" on

BIASHARA YA LUNINGA ZA KOMBE LA DUNIA

Image

HAPPY BIRTHDAY SHABAN CHINA

Image
SHABANI CHINA KATIKA POZI Tunakutakia maisha mema na marefu mwana,miaka unayofikisha leo si haba ila take care Aids kills bro.....WISH ALL DA BEST

Jinsi ya kuomba kushiriki katika tamasha la Sauti za Busara 2011

Sauti za Busara ni tamasha la muziki la kimataifa,ambalo hufanyika kila mwezi wa pili Zanzibar,kuonyesha muziki kutoka sehemu zinazo zungumza kiswahili, katika bara la Afrika na pande zote. Miaka iliyopita ,zaidi ya vikundi 280 vimekwisha shiriki baadhi yao ni Jose Chameleone, Samba Mapangala, Saida Karoli, Natacha Atlas, Didier Awadi, Bassekou Kouyate,Banana Zorro & the B Band, Joh Makini, Nako2Nako Soldiers, Nyota Ndogo,Thandiswa, Culture Musical Club na wengineo wengi. MWISHO wa kupokea maombi 31 July 2010 Kwa wasanii watakao shiriki katika tamasha, kwa kawaida hulipwa pesa kwa ajiri ya onyesho na matumizi yao wakiwa Zanzibar, ikiwa ni usafiri , malazi,chakula na matumizi madogo madogo.Kwa wasanii kutoka nje kawaida wanatakiwa kutafuta wadhamini wao wenyewe kwa ajili ya usafiri Jopo la uchaguzi litakutana mwanzoni mwa mwezi wa nane kuchagua wasanii watakao shiriki katika tamasha la Sauti za Busara 2011. Wasanii wote watajulishwa maamuzi ya jopo kwa kupitia barua pepe mnamo mwezi

Stanboi Theafricanchild

Flaviana Matata & Hasheem Thabeet named Russel Simmons' D.E.F Africa Ambassadors

Image
Teddy Kalonga-Haight | Hasheem Thabeet | Flaviana Matata The Diamond Empowerment Fund™ (D.E.F.), an independent organization founded in 2007 by Russell Simmons and members of the jewelry industry, is pleased to recognize Flaviana Matata, former Miss Universe Tanzania as D.E.F.'s new Africa's Angel Ambassador as well as NBA player for the Memphis Grizzlies Hasheem Thabeet as D.E.F.'s new Athlete for Africa Ambassador. In her first assignment, Flaviana visited with students at African Leadership Academy and CIDA City Campus in South Africa in the spring, and blogged about her experience for D.E.F. Flaviana intends to blog for D.E.F.'s website and Facebook page regularly, acting as a correspondent for D.E.F. in sharing the stories of the students at the programs D.E.F. supports. In his role, Hasheem will develop a program with D.E.F. to help raise awareness and support for the cause of empowerment through education for Africa, which will also highlight his is philanthropi

Ilianza Mara, ikaenda Kilimanjaro sasa ni Iringa...

Watu wasiofahamika wakazi wa kijiji cha Igowole wilayani Mufindi mkoani Iringa wamechoma moto ofisi ya Serikali ya kijiji hicho na moto huo umeunguza nyaraka zote za kijiji hicho toka kilipoanzishwa hadi sasa. Wakizungumza kwa njia ya simu na mwandishi wa habari juu ya tukio hilo, wakazi wa kijiji hicho wanadai kuwa tukio hilo limetokea usiku wa kuamkia leo Jumanne na kuwa jitihada za wananchi kuzima moto huo zilikwama baada ya moto huo kuongeza kasi kila wanapojaribu kuzima. Pia walisema kinachoonekana katika tukio hilo ni hujuma kutokana na siku za hivi karibuni wananchi wa kijiji hicho kufanya maandamano kupinga mwenendo wa viongozi wa Serikali ya kijiji hicho kwa hatua yao ya kuuza mali za wananchi pamoja na zile za kijiji bila kuwashirikisha malalamiko ambayo yalifikishwa kwa Mkuu wa Wilaya ya Mufindi na kuundiwa tume ambayo hadi sasa majibu na hatua haitatolewa kwa wahusika jambo linalotajwa kuwatibua zaidi wananchi hao. Picture YATOKANAYO Kwa mbayuwayu mwenye akili yake, baada

Poleni sana wapenzi wa blog yangu

Napenda kuwapa pole wapenzi wa blog hii kwa kukosa Habari kwa muda wa siku kadhaa kama wiki moja hivi,mwanablog wenu nilikuwa naumwa lakini namshukuru Mungu nimerejea tena na mambo yanaendelea kama kawaida na nitaendelea kuwashushia habari kama kawaida.

AY ashinda tuzo za MUSEKE

Image
Mwanamuziki Ambwene Yesaya aka AY, ameshinda kwenye kinyanganyiro cha Museke Online Africa Music Awards (MOAMAs) Award. Award hii imeandaliwa na wavuti wa www.museke.com ikiwa na dhamira ya kutambua vipaji na kazi za wanamuziki wa Afrika waliofanya vizuri kwa mwaka 2009/10. AY alikuwa kwenye kundi la East Africa Song of the Year. Hayo yamethibitishwa na AY mwenyewe kupitia status ya mtandao wa facebook “M happy:Nimeshinda Awards za Museke:East African Song of the Year (LEO)..mafans wangu nawashukuru sana coz mnafanya mambo kwa vitendo na matokeo yanaonekana..tonight nitaparty na watu wangu wa Kampala.Muuuuuuch RESPECT Brothers N’ Sistaz” alisema AY akiwaambia mashabiki wake.

Serikali yawaonya wenye 'blogs'

Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO), Clement Mshana amewataka wamiliki wa mitandao ya habari maarufu kama 'Blogs' na wale wa magazeti ya udaku kuacha mara moja kuweka picha na habari zinazodhalilisha jamii. Akizungumza katika mkutano ulioandaliwa na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) kwa wanahabari mjini Morogoro, Mshana alisema Tanzania imekuwa na ongezeko kubwa la vyombo vya habari tangu kuanza kwa mfumo wa vyama vingi. "Hilo ni jambo zuri katika kutoa habari za kuwaelimisha, kuwaburudisha na kuwahabarisha wananchi kuhusu masuala mbalimbali yakiwamo ya afya, siasa, maendeleo na ustawi wa jamii kwa ujumla hasa pale habari hizo zinapokuwa zimeandikwa kwa ufasaha bila udhalilishaji. "Lakini utakuta katika blog, badala ya kuwekwa habari na picha za kuelimisha jamii, zinawekwa picha za watu wakiwa uchi! Huku ni kuwadhalilisha watu. Ijulikane kuwa mitandao hiyo husomwa pia na watoto wadogo, hii inawafundisha nini?" alihoji Mshana. Hata hivyo, alisema si magaze