Posts

Azam FC yatangaza 22: Wapya 8, Waachwa 10

Klabu ya soka nchini, Azam FC inayoshiriki ligi kuu soka ya VodaCom Tanzania Bara imetangaza usajili wa wachezaji ishirini na wawili, wanane kati yao wakiwa wapya huku kumi wa kikosi kilichopita wakiachwa. Picture Said Mohammed Abeid / Mwenyekiti - Azam FC Katika taarifa iliyomo katika tovuti ya klabu hiyo, wachezaji wapya waliosajiliwa na timu hiyo ni Mohamed Binslum (Huru), Jackson Chove (JKT Ruvu), Jabir Aziz na Ramadhan Chombo 'Redondo' (Simba), Mrisho Ngasssa (Yanga), Kalimangonga Sam Daniel Ongala Rampling 'Kali Ongala' (GIF-Sweeden), Patrick Mutesa Mafisango (APR- Rwanda) na Peter Senyonjo (Polisi-Uganda). Wachezaji waliobaki ni John Bocco, Erasto Nyoni, Jamal Mnyate, Salum Aboubakar 'Sure Boy', Vladmir Niyonkuru, Philip Alando, Luckson Kakolaki, Malika Ndeule, Aggrey Morice, Salum Swed, Ibrahim Shikanda, Ally Manzi, Seleman Kasim 'Selembe' na Ibrahim Mwaipopo. Wachezaji waliopanda toka timu ya vijana 'Azam Academy' ni sita ambao ni Sino A

Justin Bieber - Somebody To Love Remix ft. Usher

SPAIN MABINGWA WAPYA KOMBE LA DUNIA

Image
Rais Jacob Zuma wa Afrika Kusini pamoja na Rais wa Fifa,Sepp Blatta wakiwa na mabingwa wapya wa Dunia mara baada ya kuwakabidhi kikombe chao cha ubingwa walioupata kwa kuitungua timu ya Taifa ya Uholanzi bao 1-0 lililofungwa na mchezaji Andres Iniesta dakika nne tu kabla ya mechi kumalizika.

Ajali ya lori yaua watano mkoani Rukwa

Watu watano wamekufa papo hapo na wengine kujeruhiwa baada ya lori walilokuwa wakisafiria kushindwa kupanda mlima Lukangao na kupinduka. Ajali hiyo ilitokea juzi saa kumi na moja jioni katika kijiji cha Ntendo, Sumbawanga mkoani Rukwa. Gari hilo ni lori aina ya Scania lenye namba za usajili T 347 ATX ambalo ni mali ya mfanyabiashara Khalid Salum Abdallah, lililokuwa likiendeshwa na Abeid Said (32), mkazi wa Mazwi. Wakati likipata ajali, lori hilo lilikuwa limebeba zaidi ya magunia ya mpunga 80 pamoja na watu 10 waliokuwa wamekaa juu wakitokea kijiji cha Majimoto wilayani Mpanda. “Wakati likipanda mlima, lilipata pancha na hivyo kupoteza mwelekeo na kupinduka na watu kupoteza maisha,” alisema Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Rukwa, Isunto Mantage. Kamanda Mantage aliwataja waliokufa kwenye ajali hiyo kuwa ni mwanafunzi wa Sekondari ya Karema, Lucy Andrew (24), Fumbuka Elias (28), Mayunga Mathias (30), na wengine wawili ambao bado hawajatambuliwa. Majeruhi waliotajwa ni Athanas Choka (26), N

SHYROSE BHANJI KUGOMBEA UBUNGE KINONDONI • 2010

Image
Shy-Rose Sadruddin Bhanji Kada wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Shy-Rose Sadruddin Bhanji ametangaza kujitosa katika nafasi ya ubunge jimbo la Kinondoni jijini Dar es Salaam kupitia CCM na lengo lake kubwa ni kuwa kiungo muhimu katika jamii ya wanakinondoni. Akitangaza azma yake ya kuomba ridhaa kwa wanachama wa CCM katika taarifa yake kwa vyombo vya habari, Shy-Rose alisema kwa mtazamo wake neno ubunge kwa mwaka 2010 linahitaji tafsiri mpya kabisa. `…kwa sasa mbunge anatakiwa kuwa ni kiungo cha jamii badala ya kuwa mwakilishi wa jimbo kama ilivyozoeleka` alifafanua Shy-Rose. `Mwaka 2010 ni mwaka wa mabadiliko na ndio maana nimeona kwamba ili kila mwananchi kuweza kuwajibika, nafasi ya mbunge inahitaji kutafsiriwa upya ili iendane na wakati na matatizo ambayo yanayotukakabili wananch` alisema. Kwa maana hiyo amesema kwamba hata sifa za mbunge zinahitaji kutafsiriwa upya kabisa, kwani majukumu yake yamebadilika kuendana na wakati. Ametaja baadhi ya sifa hizo mpya ni kuwa mhamasishaji, kiung

WACHEZAJI 70 WACHAGULIWA KUUNDA TIMU YA SERENGETI BOYS

Image
Zaidi ya wachezaji sabini wateuliwa kuunda timu ya taifa ya vijana chini ya umri wa miaka 17. Zaidi ya wachezaji sabini wameteuliwa kuunda timu ya taifa ya vijana chini ya umri wa miaka 17 SERENGENTI BOYS kutoka katika mashindano ya COPA COCA COLA ambayo tayari yameingia katika hatua ya nusu fainali. Kocha masaindizi wa timu ya taifa ya vijana chini ya umri wa miaka 17 SLYVESTER MASHI amesema vijana wanaoshiriki mashindano ya mwaka huu ya COPA COCA COLA wameonyesha vipaji vya hali ya juu na ni hazina kwa taifa Mashindano ya COPA COCA COLA yameingia katika hatua ya NUSU FAINALI kwa mchezo mmoja kati ya KINONDONI na MJINI MAGHARIBI wakati kesho KIGOMA inateremka dimbani kuivaa TEMEKE

Anaswa akimlawiti mtoto wake Liveee!!

Watoto wa kazi wa Afande Mwema,mkoani Pwani limemtundika nyuma ya nondo mpuuzi mmoja aliyetambulika Ally Salehe (36), mkazi wa Kibaha, kwa tuhuma za kukutwa akimlawiti mtoto wake wa kiume ambaye ni denti wa darasa la nne. Kwa mujibu wa bosi wa Polisi mkoani Pwani, Absalomon Mwakyoma, mtuhumiwa huyo alikamatwa juzi usiku baada ya kukutwa na majirani akifanya kitendo hicho cha kinyama. Amesema majirani walikuwa na tetesi kuhusiana na mtuhumiwa kumfanyia kitendo hicho mtoto huyo ambaye ni wa mkewe lakini walishindwa kumchukulia hatua. Amesema siku za mwizi ni arobaini kwani mtuhumiwa alikuwa akifanya kitendo hicho kwa muda mrefu hivyo juzi usiku majirani walimnasa live mtuhumiwa akimfanyia ukatili mtoto huyo pembeni ya mti karibu na nyumba wanayoishi. Baada ya majirani kumkamata mtuhumiwa huyo walianza kumpa kipigo kikali na kisha kumpeleka kituoni. Imedaiwa wakati mtuhumiwa huyo anafanya kitendo hicho mkewe alikuwa ndani akiendelea na shughuli nyingine. Hata hivyo imedaiwa kuwa mke wa mt

na huu ndio mpango mzima wa fiesta 2010.

Tamasha la kumi la burudani na michezo na sanaa nchini Tanzania, linalojulikana zaidi kwa jina la Fiesta limewadia, msimu unaanza tarehe 7 mwezi Julai ambapo utakuwa ni msisimko wa burudani kwa mwezi mzima, huku wasanii wakitembelea baadhi ya mikoa ya Tanzania yenye msisimko wa sanaa kujumuika na mashabiki wa sanaa, na kuonesha kazi zao. Kwa mwaka huu wa 2010, Fiesta imepewa msemo wa Jipanguse, ikiwa na mlengo wa kuhamasisha vijana, kuachana na tabia ya kulalamika kuhusiana na matatizo wanayokutana nayo katika maisha yao ya kila siku, na badala yake wachukulie matatizo hayo kama ni sawa na kuanguka, wajipanguse na kuendelea na safari ya maisha.. Kauli mbiu hii inamsisitiza kijana wa kitanzania kuachana na habari za kuhubiri matatizo yake huku akiomba msaada wa kuyatatua wakati akitumainiwa kama mjenzi wa Taifa, kupitia burudani kijana anaelimishwa kuhubiri jinsi ya kuutumia ujana wake kukabiliana na ugumu wa Taifa akiwa kama nguzo ya Taifa. Mikoa nane ya Tanzania itajipangusa kiburudan

2 IN 1.........FLAVA NITE Feat: LADY JAYDEE & MACHOZI BAND, DJ BONI LUV & DJ MACKAY

Image
Siku ya mkesha wa 77, Itakuwa ni Jumanne tar 6 July. Hapana kukosa kati pale mimi pia nitakuwepo habari hii ni kutoka kwa lady jaydee blog.

KUWA MAKINI

Image
Inasemekana kuwa ATM ni eneo ambalo linabeba vimelea vya magonjwa keypads ndizo hasaaa zenye vimelea vingi kwa sababu ni watu wengi wanatumia ambao hujui wametoka wapi wameshika nini hivyo na wewe kuja tu na kuanza kutumia unaweza beba vimelea vya magonjwa kwenye mikono yako.Nawa mikono mara kwa mara hasa kama umetoka kutoa hela kwenye Atm Machines kabla hujaanza kupeleka mikono kinywani,puani,machoni n.k...

BET AWARDS 2010 KUFANYIKA LEO

Image
WalE wapenzi wa burudani wanaopendelea kufatilia maswala ya burudani kwa ujumla,ile siku iliyokuwa ikisubiriwa kwa hamu ndo imefika leo NI Utowaji wa tuzo utaKAfanyika leo kwa majira ya Africa mashariki itakuwa saa 3 usiku so kaa karibu na Tv yako uweze kuona mpango mzima kwa wale wenye ving'amuzi vya DSTV.

NIGERIA'S PRESIDENT SUSPENDS NATIONAL SOCCER TEAM

News on the CNN website reads, "Nigeria's president Goodluck Jonathan has suspended the national soccer team from international competition for two years after their dismal performance at the World Cup." "President Goodluck Jonathan has directed that Nigeria withdraws from international competition for two years to enable the country to put its house in order," spokesman Ima Niboro told reporters. Nigeria's Sports Minister Ibrahim Isa Bio confirmed the decision in an interview with CNN. He said: "The government has taken a decision we believe is in the interests of Nigeria that we should for now, withdraw from international competition because our football since 1996 seems not to be growing. "The government spends a lot of money to encourage football in Nigeria and we need to go back to the drawing board the way Ghana did two years ago. "The president Goodluck Jonathan has endorsed this decision and the Nigerian people are excited about it. &q