Posts

Vigogo wazidi kubwagwa CCM

MATOKEO ya kura za maoni kwa nafasi za ubunge kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM) yamezidi kutolewa nchini huku yakiwatupa nje ya bunge baadhi ya waliokuwa wakishikilia majimbo mbalimbali, jambo linaloashiria kuwa bunge lijalo litakuwa na sura nyingi mpya. Mkoa wa Dar es Salaam Katika Mkoa wa Dar es Salaam walioibuka kidedea na kuwamwaga wapinzani ni, Dkt. Makongoro Mahanga Jimbo la Segerea (2,148) akifuatiwa na Bw. Joseph Kessy (1,435), Jimbo la Ukonga aliyeoongoza katika matokeo ya awali ni Bi. Eugen Mwaiposya (1,885) akifuatiwa na Bw. Godwin Barongo (1,394), Jimbo la Kinondoni aliyeongoza ni Bw. Iddi Azan) akifuatiwa na Bi. Shy-Rose Bhanji, Jimbo la Ubungo aliyeibuka mshindi ni Bi. Hawa Ng'umbi ambaye amewamwaga Bw. Nape Mnauye na Bi. Shamsa Mwangunga. Mkoa wa Dodoma Mkoani ambao umetoa matokeo ya awali katika majimbo yote na matokeo hayo yanaweza kubadilika mara baada ya kukamilika kuhesabiwa kura katika vituo vyote. Jimbo la Dodoma Mjini Bw. Peter Chiwanga (3,183), Bw. David Mal

CHADEMA wampitisha Mbilinyi kuwania ubunge

Image
JOSEPH MBILINYI MWANAMUZIKI wa kizazi kipya nchini, Bw. Joseph Mbilinyi maarufu kwa jina la Mr.II jana aliibuka kidedea kuwa mgombea ubunge Jimbo la Mbeya mjini baada ya kuwashinda mhandisi wa mitambo ya simu, Bw. Daud Mponzi na mwandishi wa habari wa Tanzania Daima, Bw. Christopher Nyenyembe. Katika uchaguzi uliofanyika katika ukumbi wa Kiwira Motel ulishirikisha wapiga kura 362 kutoka katika kata zote 36 wa jijini Mbeya. Mwanamuziki huyo alishinda kwa kura 175 akifutiwa na Bw. Daud Mponzi aliyepata 122, mwandishi wa habari mndawamizi wa Tanzania Daima, Bw. Christopher Nyenyembe kura 54 na mwanaharakati Gwakisa Mwakasendo aliyeambulia kura 9. Akifungua mkutano huo, Mwenyekiti wa CHADEMA Mkoa, Bw. Sambwee Shitambla aliwataka wanachama wa chama hicho kuhakikisha wanachagua mgombea atakayeweza kukiuza chama hicho kupambana na CCM na hatimaye kushinda jimbo hilo. Alisema kuwa chama hicho hakitaki mgombea atakayepita kwa mbinu za kifisadi kama ilivyo kwa wagombea wengi wanaodaiwa kufan

Kocha Stars aja leo, kuanzia kibarua

KOCHA mpya wa Taifa Stars, Jan Poulsen anatua nchini leo kuanza kibarua chake kipya ambacho kitaanzia rasmi Cairo, Misri dhidi ya mabingwa wa Afrika, Mafarao, Agosti 11. Poulsen, raia wa Denmark atawasili nchini leo usiku kuinoa Stars iliyoachwa na Marcio Maximo aliyemaliza muda wake mwanzoni mwa mwezi. Kulingana na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), mechi hiyo ambayo ni ya kirafiki ya kimataifa ilipangwa kwa mujibu wa kalenda ya Shirikisho la Soka la Kimataifa,Fifa. Ofisa Habari waTFF, Florian Kaijage, alisema jana kuwa baada ya kuwasili nchini Poulsen atakuwa na jukumu la kuanza mchakato wa kuteua wachezaji wa Stars na kuwaandaa kwa mechi hiyo siku kumi baadaye. Kaijage alisema kuwa ni matarajio ya shirikisho hilo kuwa mechi hiyo itakuwa sehemu muhimu ya matayarisho ya Stars kuanza harakati za kusaka tiketi ya kufuzu kwa fainali za mataifa ya Afrika za mwaka 2012 zitakazoandaliwa kwa pamoja na Gabon na Guinea ya Ikweta. "TFF imekuwa ikifanya jitihada kubwa kuhakikisha St

HIVI NDO ILIVYOKUWA FIESTA KUJIPANGUSA MUSOMA

Image
Hivyo ndo ilivyokuwa jana katika swala zima la kujipangusa pande za Musoma,leo watu wa Mwanza wanajipangusa leo na kesho pia......... picha hizi ni kwa hisani ya michuzijr

DR. SLAA AWASILI MUSOMA MKOANI MARA KWA KISHINDO. MKUTANO WAKE KUFANYIKA LEO JIONI.

Image
MGOMBEA URAIS KWA TIKETI YA CHAMA CHA DEMOKRASIA NA MAENDELEO (CHADEMA) LEO MCHANA AMEPATA MAPOKEZI YA NGUVU SAMBAMBA NA MAANDAMANO TOKA UWANJA WA NDEGE MUSOMA HADI HADI HOTEL ALIPO FIKIA. MKUTANO WA CHAMA HICHO UNATARAJI KUFANYIKA LEO SAA 10:00 KATIKA VIWANJA VYA MUKENDO MSOMA MJINI. PICHANI WADAU WA CHAMA HICHO WAKIISUBIRI NDEGE INAYO MLETA IPATE KUTUA KIWANJA CHA NDEGE MUSOMA HUKU WAKIWA WAMEJIPANGA MSTARI KUMPOKEA MGOMBEA HUYO ALIYETANGAZA NIA. habari hii ni kwa hisani ya blog ya www.gsengo.blogspot.com

Clouds FM Live ndani ya musoma jioni hii

Image
Watangazaji wa Clouds FM 88.4 wakiruka hewani Live jioni hii kati kati ya mji wa Musoma kuhamasisha wakazi wa mji huo kujitokeza kwa wingi kwenye tamasha la Fiesta jipanguse 2010,ambalo linafanyika ndani ya Musoma hotel kwa kiingilia cha 5000/= tu kwa kila kichwa usiku wa leo,ambapo mdhamini mkuu wa tamasha hilo ni kampuni ya bia ya Serengeti a.k.a Mfalme wa raha kamili anayedumu zaidi.Kutoka kulia ni Ruben Ndege a.k.a Ncha Kali,Msanii wa kizazi kipya Godzila a.k.a mkali wa Salasala,Fatma Hassan a.k.a Fetty pamoja Mully B.

REST IN PEACE MOM

Image
MY MOM GODRIVER POTI NYANJA Leo imetimia mwaka mmoja tangu mama yetu kipenzi atutoke mnamo tarehe kama yaleo na mwezi kama huu mwaka jana,wanao bado tunakukumbuka sana mama,upumzike kwa Amani.

HaPpY bIrTHdAY Nyanja

Image
Nyanja kelvin Poti Leo ni siku yangu ya kuzaliwa nawashukuru wadau wangu wote tuko pamoja,natimiza robo karne. twendelee kushirikiana kwa pamoja kama kawaida

NAIPENDA SANA........

Image
Baada ya kombe la dunia macho na masikio yetu tunayarudisha katika ligi inayopendwa sana dunianI,na hii si nyingine bali ni ligi kuu ya Uingereza na mimi kama kawaida yangu huwa sifichi mapenzi yangu kwa timu yangu ninayoipenda sana ya Manchester United. soon ligi itaanza itakuwa ni mwezi wa 8...so info zaidi utazidi kuzipata kutoka katika blog yako.

Utata ujenzi barabara ya Serengeti

NDOTO ya Serikali na Chama Cha Mapinduzi (CCM) kutumia mradi wa ujenzi wa barabara ya kuunganisha mikoa ya Arusha na Mara inayopita katikati ya Hifadhi ya Taifa ya Serengeti kama mtaji wa kuombea kura kwa wananchi wa mikoa ya Kanda ya Ziwa katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu iko katika hatari ya “kuyeyuka” kutokana na jumuiya za kimataifa kupinga ujenzi huo. Barabara hiyo yenye urefu wa kilomita takribani 421 inatarajiwa kuanza kujengwa mwaka 2012 na tayari watalaamu wa upembuzi yakinifu wameanza kazi wakitarajiwa kuikamilisha mwishoni mwa mwaka huu. Taarifa kwamba ujenzi wa barabara hiyo kuwa “ulimbo” wa kura kwa wapiga kura wa Kanda ya Ziwa zinathibitishwa na kauli ya hivi karibuni ya Waziri wa Maliasili na Utalii, Shamsa Mwangunga. Waziri huyo amekaririwa na vyombo vya habari akisema ujenzi wa barabara hiyo kupitia Hifadhi ya Serengeti uko palepale kwa kuwa ni sehemu ya utekelezaji wa Ilani ya uchaguzi ya CCM. “Barabara hiyo ni ahadi iliyoko kwenye Ilani ya CCM kwa wapiga kura wa Kand

Man United yambakisha Rooney

Image
wayne Rooney MKURUGENZI wa Manchester United, David Gill, atakutana na Wayne Rooney, kwa ajili ya kufanya mazungumzo ya kuongeza katika klabu hiyo. Wakati nyota huyo kabakisha miaka miwili katika mkataba wake, uongozi wa United, umepanga kumuongezea mkataba mchezaji huyo. Juzi, United, ilitangaza kukubaliana na Nemanja Vidic, kubaki klabuni hapo kufuatia taarifa kuwa angeweza kuhamia Real Madrid au AC Milan. Rooney, atafanya mazungumzo na United baada ya kurejea mapumzikoni na atakuwa mchezaji wa pili kusaini mkataba mpya na klabu hiyo. "Mpango wa sasa ni kukutana na Wayne na washauri wake pindi atakaporudi likizo kwa lengo la kuzungumzia mkataba mpya,” Gill, aliwaambia waandishi wa habari. "Aliwahi kusema na sisi tuliwahi kusema kuwa, tunahitaji kukutana na kulizungumzia suala hili, ili tuendelee kumpa maisha mapya hapa United. "Ukiangalia malengo yake na jinsi anavyojituma katika klabu hii ni wazi mpango huu utafanikiwa."?

Serikali kudhibiti wizi wa pamba Bunda

SERIKALI imesema katika msimu wa ununuzi wa zao la pamba ujao wa mwaka 2011, itaagiza mizani ya kisasa, ili kudhibiti udanganyifu kutoka kwa wafanyabiashara wa zao hilo ambao wamekuwa wakipunja wakulima kwa kutumia mizani ambayo haina ubora. Pia katika msimu ujao serikali itazikusanya mizani yote ya sasa kutoka kwa wanunuzi hao wa zao la pamba, ili zisitumiwe tena katika kupimia zao hilo. Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika, Stephen Wassira, alieleza hayo mwishoni mwa wiki katika Kijiji cha Kung’ombe wilayani hapa wakati akizungumza na wananchi kwenye mkutano wa kampeni za kuwania kuteuliwa kwenye kura za maoni za wananchama wa CCM katika Jimbo la Bunda. Alieleza hayo baada ya kuulizwa na mwananchi kuhoji serikali imejipanga vipi katika kukabiliana na tatizo la wanunuzi wa zao la pamba wanaotumia mizani mibovu kwa lengo la kuwapunja wakulima. Akijibu swali hilo, Wassira alisema serikali imeweka mipango madhubuti wa kuhakikisha wakulima wa zao la pamba hawafanyiwi udanganyifu wa aina