Posts

Image
Jengo likiwaka moto. JENGO la ghorofa tatu lililopo Manzese-Bakhresa jijini Dar es Salaam ambalo linatumiwa kwa shughuli za utengenezaji wa soli za viatu na lina maduka, jana lilishika moto baada ya kutokea hitilafu ya umeme ambapo vitu kadhaa vilivyokuwemo ndani yake viliteketea. Walioshuhudia moto huo ulioanza kuwaka majira ya saa saba za mchana walivilaumu vikosi vya uokoaji na zimamoto ambavyo vilichukua zaidi ya saa moja tangu moto huo uanze kuteketeza vitu katika jengo hilo. Wafanyakazi wa Tanesco wakiondoka eneo la tukio baada ya kuhakikisha umeme hauleti tena madhara eneo hilo. Mashuhuda wakishangalia tukio hilo. Gari la polisi likiwasili eneo la tukio kulinda usalama. Gari la zimamoto la kampuni ya Ultimate Security likielekea eneo la tukio. picha hizi ni kutoka tovuti y a http:// www.globalpublishers.com

Geneviev Emanuel miss tanzania 2010

Image
Geneviev Emanuel akikabidhiwa rasmi usiku wa kuamkia leo gari yake aina ya Hyundai i10 lenye thamani ya shilingi milioni 12 pamoja na kitita cha shilingi Mil 10.watoa burudani walikuwa ni Mh Temba na Chege kutoka TMK Family, Ambwene Yessaya (AY) Mataluma, Mwasiti na kundi la THT.

SO SORRY

Samahani sana kwa wapenzi wa blog hii nilipata tatizo kidogo kwenye Internet yangu nikashidwa kupost taarifa mbalimbali katika blog yetu,lakini nimerudi tena ulingoni kama kawaida.

HAPPY BIRTHDAY 'J-RYDER

Image
'Jeremy J-Ryder Kyejo's Producer mkali toka Tongwe Records Jeremy aka J-RYDER leo anasherehekea siku yake ya kuzaliwa,wish all da best Bro on this special day

ME AND JAILES TUKICHIACHIA PANDE ZETU

Image
Kelvin nikjiachia pande fulani Me and Jailes chilin out this weekend

JAILES AKI SHOW LOVE KWENYE BLOG PIA

Image
Anapenda kuitwa JAY akishow love kwenye blog yako kama kawa ...tufurahi pamoja.

POZI LA WEEKEND

Image
POZI LA WEEKEND KAMA KAWAIDA

SHOW LOVE

Image
call him Robert Latonga aka 6 more base,aka Big R the real hommy boy akishow love kwenye blog ya lets Enjoy Together...kama kawa Big R akiwa pande za urafiki na wana wakibadilishana mawazo

REDDS FASHION SHOW

Image
Meneja wa kinywaji cha Redds kinachozalishwa na kampuni ya (TBL) Kabula Nshimo akikaribisha wageni mbalimbali walioalikwa katika onesho hilo lililoandaliwa na kampuni hiyo kama wadhamini wenza wa Vodacom Miss Tanzania linalofanyika kwenye ufukwe wa Mbalamwezi usiku huu, Shindano la Vodacom Miss Tanzania limepangwa kufanyika Septemba 11 mwaka huu jijini Dar es salaam. Mrembo Geneviva Emmanuel akipita na kivazi cha Redds wakati wa onesho la Redds fashion Show lililofanyika kwenye ufukwe wa Mbalamwezi usiku wa jana likishirikisha warembo wanaoshiriki katika shindano la Vodacom Miss Tanzania ambalo linatarajiwa kufanyika Septemba 11 jijini Dar es salaam. Warembo kutoka kanda ya Temeke wakipita na kivazi cha Redds. Warembo kutoka kanda ya kati ya wakipita na kivazo cha Redds. Warembo kutoka kanda ya Ilala wakipita jukwaani na kivazi cha Redds. Mashabiki mbalimbali wapo wakishuhudia onesho la Redds Fashion Show kwenye ufukwe wa Mbalamwezi. Mrembo anayemaliza muda wake Miriam Gerald wa pili

TIGO KUJENGA MINARA 8 MUSOMA VIJIJINI NA SERENGETI

Image
Kampuni ya simu ya Tigo inajiandaa kuanza ujenzi wa minara 8 itakayojengwa maeneo mbalimbali ya Musoma vijijini maeneo ya Suguti,Makojo,na Saragana kwa upande wa Serengeti ni maeneo ya Ngoreme,Isenye na Nyichoka hayo yamesemwa na Mkurugenzi mkuu wa kampuni hiyo , Dallon Kango dhumuni kubwa la kujenga minara hiyo ni kusogeza huduma zao katika maeneo hayo ,aliendelea kusema kuwa "tumeamua kujenga minara hiyo kwa sababu kwa muda mrefu sasa watu wa maeneo haya wamekuwa wakiangaika kupata huduma zetu ambazo ni nafuu sana hapa nchini ukilinganisha na mitandao mingine ya simu.

THT,AY,WAHU KUPAMBA MISS TANZANIA

Image
Wasanii wa kundi la Tanzania Houde Of Talent (THT) wanaotamba na jimbo mbalimbali hapa nchini na Wahu kutoka Kenya wanatarajiwa kupamba shindano la Miss Tanzania linalotarajiwa kufanyika tarehe Septemba 11 kwenye ukumbi wa Mlimani City. Mratibu wa shindano Hashim Ludenga alisema kuwa mbali na wasanii hao,pia kutakuwa na burudani kutoka kwa AY,Mheshimiwa Temba,Chege na Mataluma. Shindano hilo linawashirikisha warembo 30 kutoka mikoa mbalimbali ya Tanzania.

UPENDO NKONE AJIANDAA KUFUNGA NDOA

Image
Mwimbaji mashuhuri wa nyimbo za INJILI Bi Upendo Nkone ambaye amekuwa mjane kwa muda wa miaka tisa anatarajia kufunga ndoa na Mchungaji John Mbeyela oktoba 17 mwaka huu.Upendo Nkone anatarajia kuagwa oktoba 11 nyumbani kwao Kigoma,Tanzania na ndoa yake na mchungaji huyo ambaye ni mjane mwenye watoto watatu itafungwa katika kanisa la Naioth maarufu lililopo Mabibo Makuburi jijini Dar es salaam.Mwimbaji huyo aliyeanza kuimba miaka mitano iliyopita amefanikiwa kutoa albamu tatu ambazo ni Mungu Baba,Hapa Nilipo na Zipo faida .