Posts

UNI FASHION BASH AT ST.AUGUSTINE UNIVERSITY

Image

MIXTAPE YA UKWELI VOL 2: THE RETURN OF THE BILINGUAL BEAST

Image
MIXTAPE YA UKWELI VOL 2: THE RETURN OF THE BILINGUAL BEAST You Can Download WAKAZI Mixtape "Mixtape Ya Ukweli Vol. 2" for FREE at http://www.zshare.net/download/89996954ae254e79/

Miaka 50 ya Uhuru ona hali za hospitali zetu

Image
Tunaadhimisha miaka 50 tangu Tanganyika ipateuhuru wake kwa mkoloni,lakini licha ya kujivunia kwa mambo lukuki kuwa TUMETHUBUTU, TUMEWEZA NA SASA NCHI INASONGA MBELE lakini katika hili la afya hasa wodi za akina mama waja wazito bado hatujaweza kuondopa kero ya vitanda na wodi katika Hospitali zetu nyingi. Serikali haina budi kuamka sasa na kunadi shangingi 1 kila Wizara au Taasisi kubwa ili kununua hata vitanda na kujenga Wodi za akina mama hawa. Isipofanyika hili haraka itafikia hatua kiongozi fulani akitaka kujifungua atapelekwa India maana huduma zetu hazikidhi kiwango.

Dancehall Thursday @Runway Lounge

Image

Rap mkongwe katika game la HIP HOP marekani Heavy D amefariki dunia.

Image
Dwight Arrington Myers (May 24, 1967 - November 8, 2011), better known as Heavy D , was a Jamaican American actor, rapper, record producer, singer and former leader of Heavy D & the Boyz , a hip hop group which included G-Whiz (Glen Parrish), "Trouble" T. Roy (Troy Dixon), and Eddie F (born Edward Ferrell). The group maintained a sizable audience in the United States through most of the 1990s

MkasiTv itaanza Jumatatu ya tarehe 14/11/2011 "SALAMA JABIR"

Image
kutana tena na Salama Jabil katika ting'a namba moja la vijana katika kipindi kipya kabisa cha Mkasi kuanzia Jumatatu ya tarehe 14/11/2011

KWELI ZA MWIZI 40

Image
Mtu mmoja ambaye hajatambulika jina lake amenaswa na umeme wa transfoma usiku wa kuamkia leo katika eneo la Hospitali ya Bugando jijini Mwanza na kufariki dunia papo hapo. Taarifa za uchunguzi zinamtaja mtu huyo ambaye inasemekana kuwa alikuwa katika mchakato wa kuiba mafuta ya transfoma hilo, wakati akifanya wizi huo alinasa mara baada ya kuegemea bila kujua moja ya nyaya zilizokuwa na umeme. Mafundi wa umeme kutoka Tanesco wakipanda kuunasua mwili wa jamaa huyo. Kutokana wizi huo baadhi ya maeneo ya jiji la Mwanza hususani eneo la Hospitali ya Bugando na maeneo yake ya jirani yamekosa umeme usiku mzima hadi leo na baadhi ya shughuli kusimama kwa kukosa nishati ya umeme. Asubuhi ya leo mashuhuda kutoka sehemu mbalimbali walimiminika kwenye tukio hilo la kutisha na kuona hatua kwa hatua za ushushaji wa mwili wa mwizi huyo wa mafuta ya transfoma. TANESCO kupitia kitengo chake cha usalama, kimekuwa kikifuatilia kwa ukaribu hali hiyo, ili kupambana na wizi huo na lich

MASHINDANO YA PRO LIFE YAZIDI KUSHIKA KASI HAPA SAUT

Image
Mashabiki wa PR wakitoa burudani kwa kucheza style ya kisauzi mashabiki waliojitokeza uwanja wa Raila Odinga kuangalia mechi Mashindano ya PRO LIFE hapa chuoni SAUT yamezidi kushika kasi,leo zimechezwa mechi mbili ya kwanza ikiwa ni kati ya Public Relations team (PR) V/S Engineering Team ambapo team ya PR imewalaza Engineering magoli 6-0..hivyo timu ya PR imezidi kuendeleza ubabe wake. Mara baada ya mchezo wa kwanza kumalizika mechi iliyofuatia ni kati ya timu ya Mass communication v/s vijana wa certificate ambapo Certificate wametoka kifua mbele kwa ushindi wa magoli 2-1 na magoli hayo ya timu ya certificate yamefungwa na Kelvin Kilua ambaye anasoma certicate ya journalism,na Pheremon Kulwa anayesoma certificate ya Accountancy,na goli la mass communication limefungwa na Vincent Kedmund,hivyo vijana wa certificate wamejiweka katika nafasi nzuri ya kuendelea na mashindano.

EPIC NATION YAFANA SANA CCM KIRUMBA

Image
Maelfu ya wakazi wa mwanza waliojitokeza katika tamasha la Epic Nation. Roma mkatoliki akiwajibika katika stage kuwarusha mashabiki wake waliofurika uwanjani hapo! Nami nikifatilia show inavyokwenda kwa ukaribu kabisa Katika Tamasha lililofanyika katika uwanja wa CCM kirumba linalojulikana kama EPIC NATION kupitia mtandao wa ZANTEL Leo limeweza kuwavuta vijana wengi kutoka sehemu mbalimbali za jiji la Mwanza na kuwakutanisha kwa pamoja katika uwanja wa CCM kirumba.kulikuw

NYAMALANGO NI KERO TUPU WAKATI WA MVUA

Image
Hili ni eneo maarufu sana kwa wanafunzi wanaolizunguka eneo la Chuo cha Mtakatifu Augustine,panajulikana kwa jina la Nyamalango,eneo ili ndipo zilipojaa stationary pia na migahawa ya vyakula,lakini eneo ili limekuwa ndio mahali pa uchafu pamoja na maji yaliotuama na yenye kutoa harufi mbaya na pia kuwa mazalia ya mbu,wanafunzi na wakazi wa eneo ili wamekuwa wakipata tabu sana hasa wakati wa mvua kwani njia hii kupitika inakuwa tabu…….. Serikali ya mtaa huu inatakiwa kuajibika juu ya swala ili!blog hii inawapa pole

JESHI KENYA LAZIMA SHAMBULIO AL-SHABAAB

Image
Msafara Serikali ya mpito ya Somalia imesema vikosi vyake vinavyosaidiwa na majeshi ya Kenya, vimefanikiwa kuzima shambulio la wapiganaji wa al-Shabaab. Msemaji wa vikosi vya Somalia ameiambia BBC kuwa wamewaua wapiganaji 36 wa al-Shabaab walipopambana eneo la kusini. Lakini kamanda wa al-Shabab amesema wanamgambo hao wameharibu magari ya kijeshi ya Kenya na kusababisha majeruhi wengi. Majeshi ya Kenya ambayo yaliingia Somalia mwezi uliopita, yametahadharisha kutoke kwa mashambulizi kwenye miji kumi nchini Somalia kwa kupitia mtandao wa jamii Twitter. Kenya inawalaumu wapiganaji wa al-Shabab kwa matukio ya utekaji nyara wageni katika ardhi yake. Lakini kundi hilo lenye uhusiano na al-Qaeada na linadhibiti sehemu kubwa ya kusini mwa Somalia, limekanusha kuhusika. Shehena ya silaha Kamanda wa al-Shabab katika eneo hilo Sheik Mohamed Ibrahim alisema msafara wa magari ya kijeshi ya Kenya ulivamiwa kwenye barabara kutoka mpaka wa mji wa Liboi wakati vikosi vya Kenya vikielek

Lema akataa dhamana, aenda rumande

Image
Mbunge wa Jimbo la Arusha Mjini, Godbless Lema (CHADEMA) jana aligoma kuwekewa dhamana katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha, hivyo kulazimika kwenda rumande katika Gereza la Kisongo kwa siku 14. Wakati washtakiwa wenzake 18 wakiachiwa kwa dhamana, Lema alikataa kudhaminiwa hata baada ya kujitokeza kwa wadhamini kutimiza masharti yaliyotolewa na mahakama. Badala yake mbunge huyo alisambaza waraka ulioeleza msimamo wake wa kukataa dhamana na kuwa tayari kwenda rumande akidai hivyo ni vita dhidi ya uonevu na ukandamizaji wa haki na utu wa binadamu. Lema katika waraka huo alisema amechoka kuishi kwa vitisho vya kila siku kutoka kwa polisi hao, na sasa hawezi tena kuogopa lolote linalotokana na msimamo wake wa kuwatetea wanyonge na maskini wanaoishi kwa kukandamizwa na utawala. ‘Leo nitakwenda jela kwa hiyari yangu binafsi kwa siku kadhaa na si kwa nia ya kutafuta utukufu wangu bali kwa kupinga uk