CHUO KIKUU CHA DAR ES SALAAM CHAFUKUZA WANAFUNZI 43.
Askari wakikabiliana na mwanafunzi huyu wa kike kwenye yaliyotoke mwezi 11, 2011, Maandamano yaliyopelekea wanafunzi 43 wa UDSM kufukuzwa Chuo. CHUO Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), kimewafukuza wanafunzi 43 na kuendelea kufuatilia nyendo za wengine tisa, baada ya kubainika kuwa walihusika katika matukio mbalimbali ya vurugu na uhalifu chuoni hapo. Kati ya wanafunzi hao, wanane walikuwa wamesimashiwa masomo kwa muda wa miezi tisa na 35 walisimamishwa ili kusubiri kumalizika kwa kesi zao zilizopo mahakamani. Uamuzi huo umekuja ikiwa zimepita siku mbili tangu baadhi ya wanafunzi chuoni hapo, kuvamia jengo la Ofisi za utawala la chuo hicho na kuwazuia maofisa na wafanyakazi wa chuo kutoka au kuingia ndani, hadi watakapoletewa taarifa za pesa zao kutoka Bodi ya Mikopo(TCU). Wanafunzi hao waliokuwa wanaendeleza mgomo wao ulioanza Jumatatu wiki hii wakidai taarifa za kwa nini pesa zao zinachelewa wakati bodi ya mikopo, ilishasema wamezileta chuoni hap