Posts

Vyuo mbalimbali vyatangaza sifa na namna ya kutuma maombi

CHUO CHA UFUNDI ARUSHA (ATC) www.atc.ac.tz . Sifa za mwanafunzi ni kupata angalau (D) katika masomo ya sayansi ambayo ni Mathematic, Physics, Chemistry kwa mwanafunzi wa kike lakini kwa mwanafunzi wa kiume awe amepata (C) katika masomo mawili kati ya hapo juu baada ya hapo ataitwa katika "access course" ambayo inachua muda wa miezi miwili na wiki mbili. Mwanafunzi anatakiwa kupata alama hamsini katika kila somo ambayo ni Mathematic, Physics, Computer and Mechanic. Gharama za "Acc Ess course" ni shilingi laki mbili kula na kulala Chuo kwa "female only". DAR ES SALAAM INSTUTE OF TECHNOLOGY (DIT) www.dit.ac.tz Sifa ni nikupata angalau (D) katika masomo yote ya sayansi kwa kila "man and woman" Kuna "access course" kwa muda wa miezi miwili na wiki mbili kwa gharama za shilingi laki na nusu kulala chuo lakini kula kila mwanafunzi anajitegemea lakini wanafunzi wataofauru watadhaminiwa na Serikali kwa gharama za kulipa shilin

WEMA SEPETU AFUNGUKA MENGI KUHUSU DIAMONDS ARE FOREVER

Image

TBL WAFANYA UZINDUZI WA CHUPA MPYA YA BALIMI MKOANI MARA

Kampuni ya Bia Tanzania TBL leo watafanya uzinduzi wa muonekano mpya wa chupa ya Balimi ikiwa ni katika kuiweka katika muonekano kama zilivyo Bia nyingine za kampuni hiyo ikiwa na shingo ndefu maarufu kama "mwanamke nyonga". Akizungumza na mwakilishi wa blog hii kutoka mkoani Mara Bw.Shomari Binda, meneja mauzo wa kampuni hiyo Mkoani Mara Polycalipo Makunja amesema kuwa maandalizi yote kuhusiana na uzinduzi huo yamekamilika ikiwemi kuwasili kwa timu nzima ya uongozi wa TBL kanda kutoka mkoani Mwanza. Poly amesema kuwa uzinduzi huo utafanyika katika ukumbi wa bawalo la Magereza kuanzia majira ya saa 1 usiku huku kukiwa na burudani mbalimbali kutoka kwa wasanii mbalimbali wa Mwanza pamoja na musoma huku wakiongozwa na bendi ya Musoma jazz. Amesema kuwa muonekano wa chupa mpya ya Balimi hautabadilisha ladha ya kinywaji hicho kwani ladha itabaki ile ile iliyozoeleka kwa wateja wa Bia hiyo ambayo ni maalum kwa wakazi wa kanda ya ziwa. Meneja mauzo huyo wa

MATOKEO YA SEMISTER YA KWANZA CHUO CHA SAUT YAMETOKA

Kwa wale wanafunzi wa chuo kikuu cha mtakatifu Augustino (SAUT) matokeo ya semister ya kwanza yametoka leo mida ya saa 12 jioni,kwa wale ambao wako likizo ya Pasaka wanaweza kuyatazama kupitia website ya chuo www.saut.ac.tz

HAPPY EASTER AT NYUMBANI LOUNGE, APRIL 7, 2012

Image

CHEZEA WAZEE WA KOMBAT WEWEE..

Image

HOSPITALI YA MUSOMA YAKABILIWA NA TATIZO LA UPUNGUFU WA DAMU

HOSPITALI ya mkoa wa Mara mjini Musoma bado inakabiliwa na tatizo kubwa la upungufu wa damu jambo ambalo limetajwa wakati mwingine kuchangia vifo hasa vya wanawake wajawazito na watoto. Mganga mfawidhi wa hospitali ya mkoa wa Mara Dk Joseph Nyamagwira Amesema kupungua kwa damu katika hospitali hiyo kumetokana na mwamko mdogo wa wananchi katika kuchangia damu hiyo hivi sasa. Amesema ingawa hospitali imekuwa ikijitahidi kuhifadhi sehemu ya damu kwa ajili kukabiliana na dharura,lakini wakati mwingine benki ya damu ya hospitali hiyo imekuwa ikiishiwa kabisa ikiwemo damu ya kundi la O jambo ambalo limekuwa likisabisha wagonjwa wa kundi hilo kupoteza maisha. Hata hivyo Dk Nyamagwira,amesema pamoja na ndugu za wagonjwa kujitolewa kuchangia damu hiyo,lakini kutokana na magonjwa yaliopo hivi sasa damu hiyo imekuwa haitumiki kumuongezea mgonjwa wakati huo hadi ipelekwe kwenye vipimo vikubwa katika hospitali ya rufaa ya Bugando jijini Mwanza ambapo zaidi ya asilimia 50 ya da

JESHI la Polisi Mkoa wa Mara litatoa zawadi ya shilingi laki sita

JESHI la Polisi Mkoa wa Mara litatoa zawadi ya shilingi laki sita pamoja na tuzo kwa Kikosi Kazi cha Askari wake waliokataa kupewa Rushwa ya shilingi laki tatu baada ya kuwakamata watu wawili wanaodaiwa kumtapeli Mwalimu mmoja shillingi Milioni tano. Akizungumza mwishoni mwa wiki, Kamanda wa Polisi wa Mkoa huo, Robert Boaz alisema kuwa kitendo kilichofanywa na askari hao ni cha kuigwa na wengine ili kupunguza kashifa zisizo za msingi pamoja kuwafanya wananchi kurudisha uaminifu ndani ya jeshi hilo. “Askari hawa kukataa rushwa ni kitendo cha kiungwana na wanahitaji pongezi na sisi kama Viongozi wao lazima tuwape tunzo mara mbili ya fedha walioikataa ili kuweza kuwatia moyo askari wetu kukataa rushwa,”alisema Boaz. Kamanda Boaz ametoa rai kwa askari wengine kuwa wakipewa rushwa wachukue lakini wamfikishe mtoa rushwa Polisi ili wazawadiwe mara mbili ya fedha waliopewa. Akielezea tukio hilo Kamanda Boaz alisema kuwa Machi 29 mwaka huu askari hao walimkamata Said Hami

SIMBA YAPAA ALGERIA NA MATUMAINI KIBAO

Image
Wawakilishi pekee wa Tanzania katika michuano ya Afrika, Simba SC wameondoka alfajiri ya leo Dar es Salaam kuelekea Algeria kwa ajili ya mechi ya marudiano, Raundi ya Pili Kombe la Shirikisho la Soka Afrika dhidi ya wenyeji ES Setif, wakipitia Algeria. Simba imeondoka ikisema ina matumaini makubwa ya kuitoa ES Setif katika mchezo huo utakaofanyika Ijumaa wiki hii. Ofisa Habari wa Simba, Ezekiel Kamwaga alisema wachezaji wapo katika ari nzuri na kwamba wimbo wao ni ushindi. Kamwaga aliwataja viongozi watakaofuatana na timu hiyo kuwa ni Mwenyekiti wa klabu hiyo, Ismail Aden Rage, Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya klabu hiyo Damian Manembe na Kamwaga. Alisema benchi la ufundi watakaokuwepo ni Kocha Mkuu Milovan Cirkovic, Kocha Msaidizi Amatre Richard, kocha wa makipa James Kisaka, daktari wa timu Cosmas Kapinga, Nyagawa na mtunza vifaa Kessy Rajab. Aliwataja wachezaji waliopo kwenye msafara ni Juma Kaseja, Ally Mustafa, Nassor Masoud, Shomari Kapombe, Amir Maftaha, Juma Nyos

HAPPY BIRTHDAY Wilhelm Oddo

Image
Thinking of you and the good times we spent make me smile! Happy birthday to a friend who is always close to my life..live longer bro

'NI NASARI NI CHADEMA ARUMERU MASHARIKI'

Image
                                  Kushoto ni Mkazi wa Arumeru Mkoani Arusha, akipiga kura katika kituo cha Ngaresero, uchaguzi wa Ubunge Jimbo la Arumeru Mashariki, jana. Picha na Edwin Mjwahuzi wa gazeti la Mwananchi.   Matokeo ya uchaguzi wa Ubunge wilayani Arumeru Mashariki yametangazwa rasmi asubuhi ya leo mara baada ya zoezi la kuhakiki uhesabu kura lililochukuwa muda mrefu kukamilika na matokeo yakimpa ushindi mgombea wa CHADEMA bwana Nasari Joshua; KURA HALALI: 60038 ZILIZOKATALIWA: 661 Wagombea: Mazengo Adam AFP 139 Charles Msuya UDP 18 TLP 18 Kirita Shauri Moyo 22 Hamisi Kiemi 35 Mohammed DP 77 Sumari Solomon CCM 26757 Nassari Joshua CHADEMA 32,972 Huu ni uchaguzi wa kwanza mdogo kwa CHADEMA kushinda katika jimbo lililokuwa likishikiliwa na CCM na uchaguzi wa pili kwa chama hicho cha upinzani, kushinda katika uchaguzi mdogo baada ya ule ul

BAADA YA MECHI YA PR 2

Image
  CHEKI VIDEO HIYO BAADA YA USHINDI WA PR 2 JANA KATIKA UWANJA WA NYEGEZI SEMINARY