Posts

TUKUTANE CCM KIRUMBA LEO KUSHUHUDIA AND 1

Image
Mida ya jioni leo hapa katika kiwanja cha CCM Kirumba itapigwa bonge moja ya game kutoka kwa wanyamwezi wa And 1 pamoja na wana Mwanza,so Don't Miss Ground nzima. Goli.

ROMA MKATOLIKI KUYAWEKA MAISHA YAKE YA MZIKI KWENYE DOCUMENTARY YAKE MPYA.

Image
Msanii anayeiwakilisha TANGA katika bongo fleva ROMA, baada ya kuchukua tuzo mbili za Kilimanjaro kama Msanii bora wa Hip Hop na wimbo wake Mathematics kuchukua kama wimbo bora wa Hip Hip hivi sasa anatengeneza Documentary yake inayoeleza maisha yake kimuziki toka alivyoanza mziki shida alizopitia mpaka kufikia hivi sasa alipofikia.   Roma akiwa katika studio ya Tongwe Rec akiitengeneza DVD hiyo ambayo amesema nimapema sana kusema itatoka lini ila haitochelewa kutoka na anaamini watu wataipenda na italeta utofauti kidogo maana story iliyomo ndani ya Documentary hiyo iko kitofauti na itamgusa kila mmoja. source djchoka.blogspot.com

Grooveback JUMAMOSI HII @ Nyumbani Lounge

Image

Veejay Tash Na Meccacheka kukisanua Arusha Leo

Image
Veejay Tash Na Meccacheka kukisanua live pande za Empire Sports Bar ndani ya Shoprite Complex Arusha Kesho kwa hisani kubwa ya Sister Tumaini wa Empire pamoja na Brother Erick wa MJ,Entry ni bure so come one come all tufurahie muziki wetu wa Arusha bila kukosa show kali toa kwa breakdancers wa ukweli..

BEYONCE NDIYE MWANAMKE MZURI KUSHINDA WOTE DUNIANI!?

Image
Tunaweza kubishana mpaka asubuhi.Iweje,kwanini…mbona yule, hata mimi namjua nk.Lakini malumbano yetu yanaweza kuwa porojo tu kwani kwa mujibu wa Jarida maarufu la People la nchini Marekani, mwimbaji/mwanamuziki na mshindi wa tuzo kadhaa za Grammy,Beyonce Knowles(ukipenda Mrs.Jay-Z) ndiye Mwanamke Mzuri kushinda wote DUNIANI kwa mwaka 2012. Nimeweka neno duniani katika herufi kubwa kwa sababu binafsi huwa nina tatizo na wamarekani wanapoiona Marekani kuwa dunia. Ukiwaambia kwamba kuna mwanamke fulani mzuri sana yupo Tanzania au Kenya au Uganda watakushangaa.Hawaijui hivyo dunia unayoiongelea wewe. Beyonce ambaye ana umri wa miaka 30 sasa na Mama wa mtoto mmoja,Blue Ivy Carter, ameelezea kufurahishwa sana na heshima hiyo aliyopewa na Jarida la People. Wanawake wengine ambao wamewahi kushinda heshima hiyo ya People ni Michelle Pfeiffer, Julia Roberts, Nicole Kidman, Halle Berry, Jennifer Aniston, Angelina Jolie na Jennifer Lopez ambaye alishinda mwaka ja

SSPRA GENERAL ELECTION ON 28 APRIL 2012

Image

HARAIKI YA WANAFUNZI YAPAMBA SHEREHE ZA MUUNGANO WA TANZANIA

Image
Haraiki ya   wanafunzi wapatao   1,727 kutoka shule za msingi mbalimbali Tanzania bara na visiwani   wameipamba vizuri sherehe ya maadhimisho ya miaka 48 ya Muungano wa Tanzania yaliyofanyika   leo katika viwanja vya Uhuru jijini Dar es Salaam. Kati ya wanafunzi hao, ni wanafunzi 727 ambapo 500 wanatoka Tanzania bara, 200 Tanzania visiwani na 27 ni mahodari wa kucheza sarakasi ambao waliingia uwanjani na kutengeneza maumbo mbalimbali pamoja na kuimba wimbo maalumu uitwao Uamuzi wa Busara. Maumbo yaliyotengenezwa na haraiki hiyo ni pomoja na bendera ya taifa, herufi zenye   umbo la miaka 48 ya Muungano, na maumbo ambayo ndani yake walicheza salakasi na ngoma za asili za ndalandala kutoka Tanzania bara na chaso kutoka Zanzibar. Maumbo mengine ni pamoja na madini ya Tanzanaiti ambayo hayapatikani sehemu yoyote duniani zaidi ya Tanzania na maumbo ya mazao ya uchumi ya katani na pamba yanayolimwa Tanzania bara na karafuu Tanzania vis

JK AONGOZA WATANZANIA KATIKA SHEREHE ZA MUUNGANO JIJINI DAR LEO

Image
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiwapungia wananchi wakati alipokuwa akiingia katika uwanja wa Uhuru jijini Dar es salaam kuongoza maadhimisho ya mika 48 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar leo asubuhi. Amiri jeshi Mkuu Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akikagua vikosi vya ulinzi na usalama wakati wa maadhimisho ya sikukuu ya miaka 48 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar katika uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam leo. Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Mama Maria Nyerere leo katika Uwanja wa Uhuru jijini Dar es salaam. Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Mwenyekiti wa CUF Profesa Ibrahim Lipumba wakati alipowasili katika uwanja wa Uhuru kuongoza sherehe za Muungano zilizofanyika leo jijini Dar es salaam

HOW TO DEVELOP IDEAS

1. Be a good observer. Keep your eyes and ears open to what is going on around you. 2. Let your mind play with ideas. Play with ideas by letting them bounce around in your mind in a nonsensical way. 3. Don't be critical during ideation. Be sure not to discard any ideas too soon. 4. Piggyback off others. Listen to the people around you and use their ideas to stimulate ideas of your own. 5. Be fluent. Remember that the more ideas you generate, the more probable it is that one of them will be a good idea. 6. Be open-minded. Don't allow narrow thinking to stop the development of your ideas. 7. Daydream. Set aside time during the day to exercise your imagination by daydreaming. 8. Know when to relax. When ideas are stale, get away from them by relaxing via tennis, biking, reading, etc. 9. Keep a notebook of ideas. Be sure to keep a small notebook handy at all times in which to record ideas so th

Leo ni siku ya kumbukumbu ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar

Mwalimu wa Historia skuli alinifunza kuwa ni ziliunda Jamhuri ya Muungano wa Tanzania tarehe 26 Aprili 1964. Unaweza kujipakulia nakala zifuatazo ili kuongeza maarifa kuhusu historia na mambo ya Muungano huu: INTELLIGENCE  STUDY ZANZIBAR:  T H E   HUNDRED  DAYS' REVOLUTION (ESAU  XXX) DIRECTORATE  OF INTELLIGENCE -  foia.cia.gov/CPE/ESAU/esau-28.pdf The Union between Tanganyika and Zanzibar  LEGALITY OF ADDITIONAL MATTERS OUTSIDETHE ARTICLES OF UNIONBY MUSSA, ALI. UBWA -  zanzinet.org/files/legality_union.pdf KWAHERI UKOLONI, KWAHERI UHURU! ZANZIBAR NA MAPINZUZI YA AFRABIA :  Dkt. Harith Ghassany -  kwaherikwaheri.com/download.htm Mohamed Said anjibu vipi "East African Muslim Welfare Society" ilivunjwa -  youtube.com/user/MzeeBarwani Baadhi ya maoni ya watu na vikundi kuhusu Muungano -  Muungano in site:mzalendo.net

Ofisi Ya Katibu UVCCM Arusha Yafungwa

Image
HALI ya Siasa Mkoa wa arusha hususan kwa Umoja wa Vijana (UVCCM) ni tete baada ya vijana hao  kuchukua uamuzi wa kufunga ofisi ya umoja huo pamoja na kubandika mabango usiku wa kumkia leo . Mabango hayo yalikuwa yakimshinikiza Katibu wa UVCCM Mkoa wa Arusha, Abdallah Mpokwa kuondoka na kumfuata aliyekuwa Mwenyekiti wa UVCCM ,James Ole Millya ambaye amehamia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) na mengine yakimtuhumu Millya kuwa ni fisadi . Wakizungumza na waandishi wa habari baadhi ya vijana wa umoja huo mkoani hapa ambao ni Ally Shabani maarufu kwa jina la Majeshi ambaye ni Katibu wa UVCCM Kata ya Moivo  pamoja na Masoud Rajabu ambaye ni Katibu wa UVCCM kata ya Lemara walisema wamechukizwa na kauli ya Mpokwa aliyoitoa janajuu ya kumsafisha Millya kwa madai hana ushahidi wa hela Sh. milioni 2 iliyotolewa kwa ajili ya  kuanzishwa kwa saccos hiyo. Shabani alisema kauli aliyoitoa  juzi Mpokwa kuwa  UVCCM haijawahi kuwa na mradi wa SACCOS na pia kukanusha suala la Millya kut

WATU WANNE (4) WAUWAWA KIKATILI ARUSHA.

Image
  Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Magesa Mulongo (kushoto) akiongea muda mfupi baada ya kuangalia miili ya watu wanne waliouawa kinyama na kutupwa maeneo tofauti. Wapi kushoto ni Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Thobias Andengenye akiwa na maofisa usalama katika eneo la kuhifadhia maiti katika Hospital ya Mkoa, Mount Meru jana   Maiti wakiwa wamelundikwa kwenye gari la polisi baada ya kugundulika wametupwa maeneo mbalimbali wilayani Arumeru jana. Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Magesa Mulongo (kushoto) akiangalia miili ya watu wanne waliouawa kinyama na kutupwa maeneo tofauti. Wapi kushoto ni Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Thobias Andengenye akiwa na maofisa usalama katika eneo la kuhifadhia maiti katika Hospital ya Mkoa, Mount Meru jana. Picha na Mdau Richard Mwaikenda   NAOMBA RADHI KWA KUZIONYESHA PICHA HIZI