Posts

WAZIRI MKUU AHITIMISHA MAADHIMISHO YA SIKU YA SERIKALI ZA MITAA KITAIFA KATIKA UWANJA WA CCM KIRUMBA JIJINI MWANZA

Image
 Wazi mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mizengo Pinda akikabidhi zawadi ya cheti mshindi wa kwanza wa jiji lililofanya vizuri kwenye maonyesho hayo kwa mkurugenzi wa jiji la Mwanza Wilson Kabwe.  Waziri mkuu mh. Pinda akiwa ameongozana na mkuu wa mkoa wa Mwanza Injinia Ndikilo alipata fursa ya kutembelea mabanda ya maonyesho hayo toka halmashauri mbalimbali nchini zilizoshiriki.  Watumishi wa ofisi ya TAMISEMI wakiwa kwenye banda la maonyesho la ofisi hiyo katika viwanja vya CCM Kirumba wakisubiri kutoa maelezo kwa waziri mkuu ambaye alipita kutembelea mabanda ya maonyesho.  Picha ya mchoro wa Jengola kisasa la kliniki ya wajawazito na watoto lililokwisha anza ujenzi wake katika eneo la mtaa wa Utemini jijini Mwanza ambalo likikamilika ujenzi wake litakuwa na taswira hii. Jengo hili litakuwa mbadala wa jengo ambalo linatarajiwa kuvunjwa la Kliniki ya zamani  lililopo mtaa wa barabara ya Makongoro. kupisha ujenzi wa jengo la Benki kuu ya Ta

ASANTENI WADAU KWA KUNIPA USHINDI

Napenda kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kila jambo ambalo linatokea katika maisha yangu kila kukicha,pia na kuwashukuru Ndugu,jamaa na marafiki walioko katika mtandao wa facebook kwa kuweza kunipigia kura za kutosha na kuweza kufanikisha kuibuka mshindi katika shindano la kutafuta blog bora za kitanzania ambalo limefanyika zaidi ya miezi 2 katika kupata washindi. Shindano hili linaratibiwa na website ya www.tanzanianblogawards.com ambayo ilianzishwa mwaka jana na mwaka huu shindano  limefanyika kwa mara ya pili likiwa na nia ya kuweza kutangaza blogs mbalimbali ambazo zinamilikiwa na watanzania waliopo nchini na wale waishio ng'ambo lakini pia kuweza kuwathamini kwa kile wanachokifanya katika kuhabarisha jamii kwaa ujumla. Shindano ili lilianza miezi 2 iliyopita kwanza kwa kuweza kunominate blog ambayo inafaa kuingia katika category mbalimbali ambazo zilikuwa zimeanishwa na waratibu,kwa mwaka huu zaidi ya blog 600 za kitanzania zilipendekezwa kuingia katika shindano hili na

BBM PARTY 2012 @Mbalamwezi Beach

Image

WALIOCHAGULIWA KUFANYA USAILI WA POLISI HADHARANI

Na Thomas Dominick Musoma JESHI la Polisi Mkoa wa Mara limetoa majina ya vijana ambao wamechaguliwa kwa ajili ya kufanya usaili wa kujiunga na jeshi hilo ambapo kanda ya ziwa utafanyika Julai 2 hadi 4 mwaka huu katika ofisi ya Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mwanza. Akizungumza na waaandishi wa habari ofisini kwake jana, Kamanda wa Polisi wa Mkoa huo, Absalom Mwakyoma alisema kuwa majina hayo yatabandikwa kwenye mbao za matangazo zilizopo katika ofisi za Mkoa na wilaya zote. “Mwaka huu tumeamua kuchukua vijana watakaojiunga na jeshi letu kutoka mashuleni ambao wamemaliza kidato cha nne mwaka jana na cha sita mwaka huu hivyo tunawaamba vijana wote waende wasome na wajue kama jina lake lipo katika orodha yetu,” “Hii tumerahisisha ili kupunguza msongamano wa vijana kufika katika ofisi zetu na kuulizia ajira hizo na kama unatumia mtandao tafuta katika mtandao wetu wa www.policeforce.go.tz na utaona jina lako na vituo vya usaili,”alisema. Alisema kuwa vijana ambao

TANESCO YATANGAZA NEEMA KWA WATEJA

 SHIRIKA la Umeme Tanzania(Tanesco), limesema ifikapo kesho litakuwa limeshawaunganishia umeme wateja wake wote walioomba kupata huduma hiyo kwa muda mrefu. Hayo yalisemewa jana na meneja uhusiano wa Tanesco, Badra Masoud alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam. Alisema kwa sasa shirika hilo lina vifaa vya kutosha na kwamba ndicho kitu ambacho kilikuwa kikiwakwamisha kutekeleza majukumu yao. “Mteja wetu yeyote ambaye ameomba anapaswa kuwa ameunganishiwa umeme ifikapo Juni 30, mwaka huu,”alisema Badra. Alisema wateja ambao walikuwa wameomba wafike katika ofisi za Tanesco katika maeneo yote zilizopo ofisi zao ili waweze kupatiwa huduma hiyo. “Tutatoa namba maalum ili wateja ambao watakuwa wanasumbuliwa na wafanyakazi wetu waweze kutupigia moja kwa moja na sisi tutashughulika nao,”alisema.

KUWAONA YANGA V EXPRESS J'MOSI TAIFA BUKU TATU TU

Image
WAKATI mabingwa wa ligi kuu soka nchini Uganda,  Express wakiwasili leo tayari kwa mchezo wao wa kimataifa wa kirafiki dhidi ya Yanga, kiingilio cha juu cha mchezo huo utakaoipgwa jumaosi katika uwanja wa Taifa kimepangwa kuwa shilingi 20,000 kwa VIP A. Ofisa habari wa Yanga Louis Sendeu amesema kwamba mashabiki watakaokaa VIP watalipa shilingi, 15,000 kwa VIP B na C ,shilingi 5,000 ni kwa watakaokaa biti vya  kijani na wale watakaokaa viti vya rangi ya bluu na chungwa watalipa shilingi 3,000. source  http://dinaismail.blogspot.com/

VODACOM KUWAZAWADIA MABINGWA WA LIGI KUU BARA J'MOSI

Image
         Simba Sc ndiyo mabingwa wa VPL         AZAM FC (washindi wa pili)            Yanga SC (Washindi wa tatu) John Bocc wa Azam FC (Mfungaji bora wa VPL) Kampuni ya Vodacom itakabidhi zawadi kwa washindi wa Ligi Kuu ya Vodacom msimu 2011/2012 katika hafla itakayofanyika Juni 30 mwaka huu kwenye hoteli ya Double Tree Hilton jijini Dar es Salaam.   Hafla hiyo itakayohudhuriwa na wawakilishi wawili kutoka katika klabu ya Ligi Kuu itaanza saa 12 jioni. Katika hafla hiyo washindi mbalimbali wakiwemo bingwa, makamu bingwa na mshindi wa tatu.   Wengine watakaozawadiwa ni mfungaji bora, kipa bora, timu bora yenye nidhamu, mchezaji bora wa ligi, refa bora na kocha bora.   Chanzo http:// dinaismail.blogspot.com

R. KELLY’S NEW BOOK THAT TALK ABOUT INABILITY TO REMAIN FAITHFUL TO HIS WIFE.

Image
Even though it doesn’t go into detail on all the juicy stuff that ‘s come to be associated with R. Kelly, his new memoir, “Soulacoaster The Diary of Me,” looks to be one very satisfying page turner. Yes, Kelly’s sex life looms large over the book. He is frank about his inability to remain faithful to his girlfriends or wife. And there are brief paragraphs where he discusses the “supposed sex tape,” but they feel legally sanitized. And well-known stories about who leaked the tape and why are never addressed. “Certain episodes could not be included for complicated reasons,” Kelly writes in the author’s note at the beginning of the book

TAMKO LA JUMUIYA YA MADAKTARI KUHUSIANA NA TUME ILIYOUNDWA NA JESHI LA POLISI KUCHUNGUZA TUKIO LA DR. ULIMBOKA

Image
KAMATI YA JUMUIYA YA MADAKTARI TANZANIA                                                                                              YAH: TAMKO FUPI LA JUMUIYA YA MADAKTARI KWA WAANDISHI WA HABARI LEO TAREHE 28.06.2012  Madaktari wote hatuna imani na tume iliyoundwa na Jeshi la polisi nchini yenye lengo la kuendesha uchunguzi juu ya kutekwa, kunyanyaswa na kupigwa vibaya kwa Dr. Ulimboka Stephen na tunataka chombo huru kiundwe ili kupata ukweli wa tukio hilo. Pia tunakemea na kuonya juu ya vitisho vyote vinavyotolewa na baadhi ya watawala katika taasisi mbalimbali dhidi ya madaktari mfano Hospitali ya Rufaa ya Dodoma, Bugando, Mbeya na kwingineko ambapo wametishwa na kufukuzwa kwa kutumia mabavu. Madaktari tunazidi kusisitiza kuwa hakuna njia nyingine yeyote ya kusuluhisha mgogoro huu isipokuwa ni kwa kutekeleza madai na hoja za msingi za madaktari kwa njia ya mazungumzo ya dhati. Madaktari tumechoka kuona hudum

PROFESA MAJI MAREFU ACHAFUA HALI YA HEWA BUNGENI DODOMA

Image
Mbunge wa Jimbo la Korogwe Vijijini, Steven Ngonyani maarufu kwa jina la Profesa Maji Marefu (pichani), leo amesema bungeni kuwa kipigo alichopata Mwenyekiti wa Jumuiya ya Madaktari, Dk. Steven Ulimboka, kinastahili ili naye apate machungu wanayopata wagonjwa wengine mahospitalini. Profesa Maji Marefu aliitoa kauli hiyo wakati akichangia hoja katika bajeti ya Ofisi ya Waziri Mkuu, Bungeni Dodoma. Kauli hiyo ilisababisha tafrani kidogo bungeni, ambapo  Spika wa Bunge, Mhe. Anne Makinda  alilazimika kuingilia kati kumzuia Profesa Maji Marefu asiendelee kutoa kauli hiyo kwani jambo la madaktari bado liko mahakamani.

LISA JENSEN KUWA MGENI RASMI REDD'S MISS MARA 2012

Na Shomari Binda Musoma, Mnyange anayekwenda kuiwakilisha Nchi katika mashindao ya miss world 2012 Nchini China mapema mwezi wa nane na miss Mara mwaka 2006 ambaye ni mshindi wa tatu katika miss Tanzania mwaka 2006 Lisa Jensen amewasili Mkoani Mara kwa ajili ya kushuhudia kinyang'ang'anyiro cha kumpata miss Mara 2012 akiwa kama mgeni rasmi. Akizungumza na Waandishi wa Habari katika uwanja wa ndege Musoma Lisa alisema anawashukuru waandaji wa miss Mara kampuni ya Homeland kwa kumpa heshima ya kuwa mgeni rasmi katika shindano hilo na kueleza kuwa hiyo ni heshima kubwa kwake na ameshukuru kupata heshima hiyo. Alisema hiyo imeoonyesha mashindano ya urembo sio uhuni kama ambavyo bado kuna watu wenye mawazo kuwa urmbo ni uhuni na kudai kuwa hurka ya uhuni na ya mtu mwenyewe na unaweza kufanya mambo mengi ya kujiletea maendeleo kutokana na fani ya urembo. Alidai kuwa kwa upande wake tangu aingie kwenye masuala ya urembo mwaka 2006 amepata faida kubwa

JOSE CHAMELEONE KUTUA BONGO KWA SHOO YA UWANJA WA TAIFA SIKU YA SABASABA

Image
Msanii wa Uganda, Jose Chameleone (pichani juu) leo amekamilisha taratibu zote za kusaini mkataba wa kufanya shoo kali Uwanja wa Taifa mpya, jijini Dar es salaam, siku ya sabasaba baada ya Meneja Mkuu wa Global Publishers, Abdallah Mrisho, kutia timu Entebe mapema leo. Pichani chini ni Chameleone akijigamba kufanya shoo na akisaini mkataba wa mwisho huku akishuhudiwa na meneja wake. Chameleone ametoa onyo kwa Diamond kuwa atamchakaza na Valuvalu!