Posts

SAMAHANI KWA USUMBUFU UTAKAO JITOKEZA

Samahani sana wapenzi wa Blog hii,napenda kuwafahamisha kuwa hakutakuwa na taarifa nyingi za mara kwa mara  kama mlivyozoea kwani nitakuwa katika kipindi cha Mitihani ya kumaliza semister ya 1 ambayo itaanza Jumatatu tarehe 28/01/2013 mpaka tarehe 8/02/2013 hivyo nitakuwa busy na Mitihani hiyo.

CCM KIRUMBA HAPATOSHI LEO, NI YANGA DHIDI YA BLACK LEOPARDS YA AFRIKA KUSINI.

Image
Yanga Africans. Kocha Mkuu wa klabu ya Yanga, Ernest Brandts amesema timu yake itafanya vizuri katika mechi ya marudiano ya kirafiki dhidi ya Black Leopards ya Afrika Kusini niliyopangwa kufanyika mapema jioni ya leo ndani ya uwanja wa CCM-Kirumba mjini Mwanza. Brandts alisema wachezaji wake wote wamefikia kiwango kile anachotaka na mchezo huo utakuwa muhimu sana kwake kwani ni wa mwisho kabla ya kuingia katika kampeni za kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara. Alisema kuwa Black Leopards ni timu nzuri na walipata mazoezi mazuri katika mechi ya kwanza iliyofanyika kwenye uwanja waTaifa jijini na kushinda kwa mabao 3-2.

MAFUNZO YA KWANZA YA U-DJ KUFANYIKA NCHINI

Image
ICHT DJ ACADEMY, ACADEMY YA KWANZA KUFUNGULIWA JIJINI DAR     YA KUFUNDISHA KUDJ PROFESSINALLY, KOZI ZITAKAZOFUNDISHWA NI:-   INTRODUCTION TO THE DJ INDUSTRY AMBAPO NDANI YAKE KUNA PACKAGE YA KOZI SABA (7) . 1.Set up Machine 2.Mixer Operation 3.Pioneer Operation 4.Basic Mixing 5.Beat Count 6. Beat to Beat mixing 7.Acapella Mixing NA     ADVANCE INTRODUCTION     TO THE DJ INDUSTRY:   AMBAPO NDANI YAKE KUNA PACKAGE YA KOZI (5). 1. Sound and Level 2. Turntable Operation 3. Perfect mixing 4. Scratching 5. Creative mixing and Techniques WALIMU WATAKAO FUNDISHA NI DJ PQ, DJ ZERO NA DJ D OMMY. ACADEMY IKO NYUMA YA BEST BITE KARIBU NA NYUMBANI LOUNGE. MAFUNZO YANATEGEMEA KUANZA TAREHE 4 FEB 2013.             KWA MASILIANO ZAIDI JINSI YA KUPATA FOMU ZA KUJIUNGA PIGA                                         NAMBA:         0712 58 08 59                                                Email :   itchdjacademy@gmail.com source : http://gsengo.blogsp

TAZAMA PICHA BAADA YA UKUTA KUANGUKA KATIKA KITUO CHA MABASI CHA UBUNGO ASUBUHI NA KUSABABISHA HASARA NA UHARIBIFU MKUBWA

Image
 Baadhi ya magari yaliyoangukiwa na ukuta.  Magari mbalimbali yakiwa chini ya kifusi.  Gari aina ya Noah likiwa limegandamizwa na zege.  Hii ndiyo hali halisi ya tukio lilivyokuwa.  Gari aina ya Toyota likiwa limebonyezwa na zege.  Watu wakiangalia magari yao.  Kenyela akiongea jambo juu ya ajali hiyo.  likuwa ni hasara tupu. .UKUTA WA ENEO  LA NDANI YA KITUO CHA MABASI UBUNGO BUS TERMINAL UMEANGUKIA MAGARI ZAIDI YA 24 YALIYOKUWA YAMEPAKI ENEO AMBALO HUTUMIKA KUPAKI WAKIWA WANASINDIKIZA ABIRIA NA NDUGU ZAO,CHANZO CHA AJALI HIYO NI MKANDARASI WA ENEO HILO ALIKUWA ANABOMOA UKUTA HUO,NA PIA IMERIPOTIWA KUWA KUNA BAADHI YA MAJERUHI source  http:// thegeebtz.blogspot.com

DARASA FT WINNIE -NISHIKE MKONO (OFFICIAL VIDEO)

Image

DAKTARI WA MAGONJWA YA WANAWAKE NA WATOTO HOSPITALI YA MKOA WA MARA AFARIKI DUNIA

Image
MAREHEMU DOCTA JOSEPH NYAMAGWIRA Na Shomari Binda DAKTARI Msaidizi Mkuu Daraja la kwanza wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mara,Joseph Nyamagirwa (59) amefariki Dunia juzi asubuhi katika Hospitali ya Rufaa ya Bugando Mkoa wa Mwanza kwa tatizo la uvimbe sehemu ya chini ya utumbo mpana. Daktari huyo ameacha pengo kubwa katika Hospitali ya Mkoa wa Mara kutokana na kuwa tegemeo kubwa hasa kwa kutibu watoto na wanawake pamoja na upasuaji ambapo kwa sasa hospitali hiyo inahitaji madaktari 12 na hivi sasa waliopo ni watatu tu.     Akitoa taarifa ya kifo hicho,Kaimu Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mara, Iragi Ngerageza alisema kuwa Marehemu alikuwa na tatizo la tumbo ambalo alikuwa akilalamikia kuwa linauma ambapo Jan.8 Mwaka huu alifika Hospitalini hapa kwa matibabu ambayo iliwalazimu kumpeka katika hospitali ya Rufaa ya Bugando na siku hiyo hiyo akifanyiwa upasuaji wa kina.   Alisema kuwa pamoja na jitihada za madaktari bingwa kuokoa maisha yake lakini hali yake

MWANZA FASHION WEEKEND MODELS SEARCH

Image
Kwa  mara ya kwanza katika jiji la Mwanza unaletewa Mwanza Fashion Weekend itakayofanyika mwezi March tarehe 2.  Msako wa models wa kike na kiume watakaopita kwenye runway siku ya onesho utafanyika jumamosi hii tarehe 19-1-2012 katika hoteli ya Goldcrest Ghorofa ya nane kuanzia saa 4 asubuhi mpaka saa 8 mchana.  Njoo upate nafasi ya kuonesha kipaji chako na kuonesha mavazi ya wabunifu maarufu Afrika Mashariki kama vile Mustspha Hassanali, Martin Kadinda na wengine wengi.

MEYA WA JIJI LA MWANZA ATEMBELEA HALMASHAURI YA MANISPAA YA ILALA

Image
Mstaiki meya wa jiji la Mwanza Mhe.Stanslaus Mabula na ujumbe wa kamati yake ya fedha wametembelea halmashauri ya manispaa ya Ilala kwa maagizo ya Mhe.Waziri Mkuu kuja kujionea mbinu za kisasa za kukusanya mapato. Mstaiki Meya wa Halmashauri ya manispaa ya Ilala Mhe Jerry Silaa amewakaribisha na kuwaeleza jinsi walivyoweza na wanavyoendelea kukusanya mapato. Jiji la Mwanza na Manispaa ya Ilala zinaanzisha Udada. WAHESHIMIWA WAKIMSIKILIZA MEYA WA MANISPAA YA ILALA MH.JERRY SILAA MH.JERRY SILAA AKITOA UFAFANUZI  JUU YA UKUSANYAJI MAPATO MH.JERRY SILAA KATIKATI AKIWA  PAMOJA NA AFSA HABARI WA JIJI LA MWANZA JOSEPH MLINZI(KUSHOTO) NA MH. STANSLAUS MABULA

TENGA ATANGAZA RASMI KUTOGOMBEA TENA URAIS TFF

Image
Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) Leodegar Tenga amesema hawezi kugombea tena nafasi hiyo katika Uchaguzi Mkuu wa Shirikisho hilo unaotarajia kufanyika February 24 mwaka huu. Akizungumza na Waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Tenga amesema wakati anaingia madarakani miaka minne iliyopita alikuwa na kazi ya kufanya, ambayo ilikuwa ni kujenga taasisi ya soka nchini, na kwamba hawezi kuendelea tena kwani uongozi ni kijiti na kwamba huu sasa wakati wa kukimbizwa na mtu mwingine. “Nimekaa madarakani kwa miaka minane kwakweli ni miaka mingi sana,tangu mwaka 2004 ambapo wakati huu kulikuwa na ajenda maalum ya kuleta mabadiliko ya msingi katika soka” alisema Tenga.

MAVETERANI WA PR MWAKA WA TATU MNATAKIWA KUFIKA MAZOEZINI

Maveterani wote wa PR 3 mnatakiwa kufika mazoezini kesho kuanzia saa 10 Jioni kwa ajili ya maandalizi ya mechi kati ya Maveterani na  timu ya darasa (PR 3) itakayofanyika siku ya JUMAPILI, tarehe 20/01/2013,  katika uwanja wa Nyegezi Seminary kuanzia saa 1 asubuhi. FIKA KWENYE MAZOEZI BILA KUKOSA

WANACHUO IFM WAANDAMANA.

Image
Wanafunzi wa Chuo cha Usimamizi wa Fedha cha jijini Dar es Salaam (IFM) wameandamana leo majira ya adhuhuri hadi kwenye  Wizara ya Mambo ya Ndani wakiwa na madai ya kutopewa ulinzi na jeshi la polisi kwenye makazi yao ya hosteli za Kigamboni kutokana na kuvamiwa na majambazi mara kwa mara. Wanafunzi hao walidai kuwa, siku ya Ijumaa walifanya kikao na jeshi hilo ili wawape ulinzi lakini suala la ajabu ni kuwa, siku waliyofanya kikao na Jeshi hilo ndiyo siku wenzao wawili wakiume walipovamiwa na kulawitiwa. Majambazi hao wamekua wakidai wapewe laptops, simu na fedha na kama mwanafunzi anakataa, humlawiti. Rais wa Serikali ya wanafunzi ya Chuo cha IFM alizungumza leo na Kamanda wa Polisi wa Kanda maalumu ya Kipolisi ya jiji la Dar es Salaam Suleiman Kova mara baada ya kuwasili eneo la ofisi za Wizara ya Mambo ya ndani ambapo alisema, "Wanafunzi wenzetu wa kiume wamelawitiwa nyinyi tumewapa taarifa siku ya ijumaa kuwa hatunaulinzi tunaibiwa hovyo vitu vyetu halafu siku hiyo hiyo unafa

GODLISTEN MALISA RAIS WA SERIKALI YA WANAFUNZI AJIBU HOJA POTOFU ZILIZOSAMBAZWA MTANDAONI NA WAPOTOSHAJI JUU YA UTENDAJI WA SERIKALI YAKE.

By  kijungu jiko HIZI NDIZO HOJA ZA MPOTOSHAJI JUU YA UTENDAJI WA SERIKALI YA WANAFUNZI SAUTSO. MAJIBU YAKE YAPO CHINI. M alisa Godlisten Rais wa Serikali ya Wanafunzi SAUTSO Chuo kikuu cha St Augustine umetudharirisha mpaka tunaona aibu sasa na vuguvugu la  CHADEMA , tena tuliingia kwa mbwembwe kali kuwa tutakuwa wakombozi wa watu, waliotuchagua kwa kura nyingi richa ya kuwepo nguvu kubwa ya viongozi waliotangulia hasa Rais Bwana Cosmas Mataba na Anna Mushi, Spika wa Bunge Bw Maro Pius, na aliyekuwa Waziri mkuu Bw Leonard Mafuru, tukamchagua kijana huyu aliedaiwa machachari akitokea Baraza la vijana la  CHADEMA  yani BAVICHA kwa kishindo cha zaidi ya asilimia 75% licha ya hira za Mataba na Tume yake ya Uchaguzi, tukashinda uchaguzi kwa mbwembwe kabisa tukimtupilia mbali mgombea aliefadhiriwa kwa gharama kubwa na CCM Bwana Antony na Mgombea mwenza Bibie Alice, tuliingia huku wanafunzi wakiwa na matumaini makubwa ya kuona mabadiriko kufuatia manung’uniko ya serikari ilio tangulia ya