Posts

KATUNI YA LEO................HATARI TUPU

Image
Rais Jakaya Kikwete amekemea vurugu zilizotokea jana mkoani Mtwara baada ya kusomwa bungeni kwa Bajeti ya Wizara ya Nishati na Madini. Akizungumza katika eneo la Kizota, Dodoma wakati wa kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa Barabara ya Dodoma kwenda Iringa, Rais Kikwete alisema rasilimali inayopatikana mahali popote pale nchini inatakiwa kutumiwa na Watanzania wote, “Hivi watu wa Nyarugusu wadai dhahabu ya pale au kinachopatikana Chalinze basi kisitumiwe na watu wa Morogoro! Hivi tutakuwa na taifa kweli?,” alihoji kwa ukali Rais Kikwete. Rais alisema wote waliohusika na vurugu hizo, Serikali itawasaka ikiwa ni pamoja na viongozi wa vurugu hizo na ili kuwawajibishwa: “Tutawasaka hawa watu na viongozi wao hata kama wana mapembe kiasi gani, tutayakata.” Source:  http://www.wavuti.com/#ixzz2U6Em1STi

BUNGE LIMEHAIRISHWA TENA MPAKA KESHO SAA 3 ASUBUHI.

Image
Spika wa Bunge la Tanzania, Mh. Anna Makinda amehairisha Bunge mpaka kesho saa 3 asubuhi ,ili Kamati tofauti za bunge zikajadili kuhusu hali inayoendelea huko mkoani Mtwara

DOWNLOAD NA KUSIKILIZA WIMBO MPYA WA MALFRED- "PIGANA"

HAPPY BIRTHDAY CLASSMATE ONESMO FAUSTINE

Image
wish all da best in ur life bro

Msanii Joseph Haule (Prof. Jay) ajiunga CHADEMA

Image
what I expected have become true......ndani ya GWANDA.

TANGAZO KUTOKA BARAZA LA MITIHANI LA TANZANIA

Katibu Mtendaji Baraza la Mitihani la Tanzania anapenda kuwatangazia watu  wote wanaotaka kufanya Mtihani wa Kidato cha Sita (ACSEE) mwezi, Mei 2014 kama Watahiniwa wa Kujitegemea kwamba kipindi cha usajili kitaanza  rasmi tarehe 1 Julai, 2013 kwa ada ya Shilingi 35,000/=. Kipindi cha malipo  bila adhabu kitaishia tarehe 31 Agosti, 2013. Kuanzia tarehe 1 Septemba, 2013 hadi tarehe 30 Septemba, 2013 waombaji watajisajili kwa ada ya  Shilingi 50,000/- (ada pamoja na faini). Waombaji wote watajisajili kwa njia ya mtandao kupitia tovuti: www.necta.go.tz. ya Baraza la Mitihani la Tanzania. Kabla ya kujisajili  kwenye mtandao waombaji watapaswa kwenda kwenye vituo vya mitihani  kuchukua namba rejea (reference number) watakazotumia kujisajili.  Hakuna  mtahiniwa atakayeweza kujisajili bila kupata namba rejea kutoka katika kituo  anachokusudia kufanyia Mtihani. Wakuu wote wa vituo nchini watakabidhiwa  namba rejea hizo kabla ya muda wa usajili kuanza na watazig

WASANII WATAKAOTUMBUIZA KATIKA SHOW YA UFUNGUZI WA BIG BROTHER WATAJWA

Image
Show ya ufunguzi wa msimu mpya wa shindano la Big Brother Africa itafanyika Jumapili hii, May 26 nchini Afrika Kusini.  Usiku huo utawaonesha washiriki wote 28 watakaoanza safari ya miezi mitatu ya kuzisaka dola laki tatu za msimu wa nane wa Big Brother Africa, The Chase. Miongoni mwa wasanii watakaotumbuiza kwenye ufunguzi huo ni pamoja na STL wa Kenya, Don Jazzy, D’ Prince na Wande Coal kutoka Nigeria na kundi la Mafikizolo la Afrika Kusini. Pia mchekeshaji wa Kenya Daniel Ndambuki, maarufu kama Churchill atapanda kwenye stage kuwavunja mbavu watazamaji wa show hiyo katika nchi 50 barani Afrika.  Show hiyo itaonekana live pia kupitia website ya Big Brother

LEO NI KUMBUKUMBU YA MIAKA 17 YA KUZAMA MV.BUKOBA

Image
Mei 21,1996 katika ziwa Victoria,Mwanza Tanzania meli ya Mv Bukoba ilipata ajali na zaidi ya watu 800 kupoteza maisha yao.Meli ilizama kilomita 30 kukaribia kutua nanga kwenye bandari ya mwanza ikitokea Bukoba. Meli ikuwa na uwezo wa kubeba idadi ya watu 430. Kwenye first and second class orodha ya abiria ilikuwa 443 na kwenye third class hakukuwepo rekodi yoyote .Takribani 1000 walifariki kwenye ajali hiyo MUNGU AZIWEKE ROHO ZA MAREHEMU WOTE MAHALA PEMA PEPONI,NA PIA MUNGU AWAPE NGUVU WOTE AMBAO WALIPOTEZA NDUGU ZAO KATIKA AJALI HIYO. ASANTE KWA MDAU  Petter Isuti Mioyo   KWA KUTUKUMBUSHA KUPITIA ACCOUNT YAKE YA FACEBOOK

NAOMBA DUA ZENU WADAU WOTE

Napenda kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kunibariki kila kunapokucha na kuweza kunipa nguvu za kusimama na kufikiri vyema, ndugu zangu sasa wakati unakaribia kabisa wa kumaliza elimu yangu ya chuo kikuu nayosomea shahada ya mahusiano ya Umma na Masoko. Zimebaki takribani wiki 8 ambayo ni sawa na miezi 2 hivi kuhitimu elimu hii,jambo lililopo mbele yangu ni hapo kesho katika kutetea utafiti nilioufanya (Research defense) mbele ya jopo la wahadhili, si jambo ndogo waweza kuwa na confidence ya kutosha lakini linapofika swala la Maswali kila mhadhili huwa anauliza kwa jinsi anavyojisikia yeye na pengine hata kukuuliza kitu kisichohusiana na research pia,hivyo nawaomba ndugu zangu basi twendelee kushirikiana katika maombi na kuniombea kwa baba mwenyezi Muumba wa mbingu na dunia niweze kudefend vizuri. SALA ZENU NI MUHIMU SANA KUFANIKISHA SWALA HILI.

YANGA YASHEREHEKEA UBINGWA KWA KUMNYOA MTANI WAKE

Image
Nahodha wa Yanga, Nidir Haroub   'Canavaro' akiwa amenyanyua kombe la Ubingwa wa  Ligi Kuu ya Soka Tanzania Bara pamoja na wachezaji wenzake. Beki wa Simba, Musa Mudde (kushoto) akichuana na mshambuliaji wa Yanga, Didier Kavumbagu katika mchezo wa Ligi Kuu ya Soka Tanzania Bara uliofanyika kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, leo. Kikosi cha Simba. Makocha wa yanga wakipanga mikakati ya Ushindi. Timu zikiingia uwanjani. Beki wa Simba, Shomari Kapombe akimtoka mshambuliji wa Yanga, Simon Msuva Msanii Juma Nature akitumbuiza wakati wa mchezo huo. Mashabiki wa Yanga . Raha ya ushindi. Kocha wa Yanga, Ernst Brandts akiwa amebebwa na wachezaji wake. Mashabiki wa Yanga. Kipa wa Simba, Juma Kaseja akijaribu bila mafanikio kuokoa mpira wa kichwa  uliopigwa na mshambuliaji wa Yanga, Didier Kavumbagu katika mchezo wa kufunga  pazia la Ligi Kuu ya Soka Tanzania Bara uliofan

WALE WAPENZI WA MOVIE HIZI ZINAKUHUSU MWAKA HUU

Image
GI JOE 2 Retaliation Trailer 2 - 2013 Movie  The Wolverine Trailer 2013 Official - Hugh Jackman Movie [HD]  After Earth Trailer #2 2013 Will Smith Movie - Official [HD] Gallowwalkers Official Trailer #1 (2013) - Wesley Snipes Zombie Movie HD  Reincarnated Official Trailer #1 (2013) - Snoop Lion Documentary HD  The Frankenstein Theory Official Trailer #1 (2013) - Timothy V. Murphy Thrille

KILIO KUANGUKIA JANGWANI AU MSIMBAZI?

Image
Leo ndio leo uwanja wa Taifa wakati miamba miwili ya soka nchini, Yanga na Simba watakapoufunga rasmi msimu wa ligi kuu Tanzania Bara. Yanga ambao tayari wametawazwa kuwa mabingwa wataingia uwanjani huku wakiwa tayari wanajiandaa kwa sherehe rasmi za kukabidhiwa kombe wakati watani wao wa jadi Simba waliovuliwa ubingwa huo watakuwa wakitaka kulinda heshima yao. Katika mchezo uliozikutanisha timu hizi mbili katika mchezo wa kufunga pazia la ligi kuu, Simba ambao walikuwa tayari wametangaza ubingwa walitoa kipigo kikali cha 5-0. Je unadhani Yanga watalipiza kisasi? Msiba leo utakuwa wapi, Jangwani au Msimbazi