Posts

MAGAZETI YA LEO ALHAMIS, OCTOBA 2

Image

ARSENAL YAUA, WELBECK AGONGA HAT-TRICK

Image
Mshambuliaji Danny Welbeck akishangilia baada ya kupiga 'hat-trick'. Alexis Sanchez akiifungia Arsenal bao la tatu dhidi ya Galatasaray. Welbeck akitupia bao la nne. Kocha wa Arsenal, Arsene Wenger ametimiza miaka 18 akiwa meneja wa klabu hiyo leo. KLABU ya Arsenal imetoa kichapo cha mabao 4-1 dhidi ya Galatasaray kwenye mechi ya Ligi ya Mabingwa Ulaya iliyopigwa Uwanja wa Emirates jijini London usiku huu. Mshambuliaji Danny Welbeck ametupia kambani mabao matatu 'hat-trick' huku bao la nne likiwekwa kimianai na Alexis Sanchez. Katika mtanange huo, kipa wa Arsenal, Wojciech Szczesny alizawadiwa kadi nyekundu baada ya kumfanyia madhambi mshambuliaji wa Galatasaray, Burak Yilmaz. Ushindi wa leo wa Arsenal umeongeza furaha kwa Meneja wa timu hiyo, Arsene Wenger aliyetimiza miaka 18 akiwa kocha wa klabu hiyo leo. VIKOSI: Arsenal: Szczesny, Chambers, Mertesacker, Koscielny, Gibbs, Flamini, Cazorla,

MHADHIRI UDSM APIGWA RISASI NA KUFARIKI

Image
Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Profesa Athuman Livigha Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Profesa Athuman Livigha, amefariki dunia baada ya kupigwa risasi na watu wanaosadikiwa kuwa ni majambazi nyumbani kwake, jijini Dar es Salaam. Taarifa za kifo hicho zilithibitishwa na Makamu Mkuu wa UDSM, Profesa Rwekaza Mukandala, alipozungumza na NIPASHE kwa njia ya simu jana. Profesa Mukandala alisema Profesa Livigha alikutwa na masaibu hayo akiwa nyumbani kwake Bunju, Wilaya ya Kinondoni, jijini Dar es Salaam, usiku wa kuamkia jana na kwamba, mwili wake umechukuliwa na polisi kwa uchunguzi zaidi. “Ni kweli, na mimi hizo habari tumezipata na watu wote wamekwenda nyumbani kwake. Mwili umechukuliwa na polisi, tunasubiri taarifa kutoka polisi,” alisema Profesa Mukandala bila kufafanua zaidi na kuongezaa: “Mimi nilikuwa mjini, wenzangu wamekwenda nyumbani kwake Bunju. Tumesikitishwa sana kwa kupotelewa na mwalimu wetu mwingine katika mazin

TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI SEKRETARIETI YA AJIRA, KWA NIABA YA MKAGUZI MKUU WA SERIKALI NA MAMLAKA ZA SERIKALI ZA MITAA

Katibu wa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma kwa niaba ya Ofisi  ya  Mkaguzi  mkuu  wa  Serikali  (NAO),  Wakala  za  Serikali  na Mamlaka  za  Serikali  za  Mitaa  (MDAs  &  LGAs)  anatarajia  kuendesha usaili na hatimae kuwapangia vituo vya kazi waombaji kazi watakaofaulu usaili. Wasailiwa walioitwa kwenye usaili wanapaswa kuzingatia yafuatayo: 1. Usaili utaanza saa moja kamili asubuhi (1:00) na utafanyika mahali na tarehe kama inavyoonesha katika nafasi husika. 2.  Kuja  na  kitambulisho kwa  ajili  ya  utambuzi  mfano:  kitambulisho  cha mkazi, kupigia kura, kazi, hati ya kusafiria n.k 3. Kuja na Vyeti Halisi (original certificates) vya kuanzia kidato cha nne, sita,  Stashahada,  Stashahada  ya  Juu,  Shahada  na  kuendelea kutegemeana na sifa za mwombaji. 4.  “Testmonials”,  “Provisional  Results”,  “Statement  of  results”,  hati matokeo za kidato cha nne na sita (FORM IV AND FORM VI RESULTS SLIPS) HAVITAKUBALIWA. 6. Kila msailiwa atajigharamia kwa chakula,

NAFASI MPYA 87 ZA KAZI KUTOKA SERIKALINI

Sekretariati  ya  Ajira  katika  Utumishi  wa  Umma  ni  chombo  ambacho  kimeundwa  kwa mujibu wa Sheria ya Utumishi wa Umma Na. 8 ya mwaka 2002 kama ilivyorekebishwa na Sheria Na. 18 ya mwaka 2007 kifungu 29(1). Kwa mujibu wa Sheria hiyo, chombo hiki, pamoja na kazi zingine kimepewa jukumu la kutangaza nafasi wazi za kazi zinazotokea katika Utumishi wa Umma kwa niaba ya Waajiri (Taasisi za Umma).   Katibu  wa  Sekretarieti  ya  Ajira  Katika  Utumishi  wa  Umma  anakaribisha  maombi  kwa Watanzania wenye sifa na uwezo wa kujaza nafasi  87  za kazi kwa ajili ya  wakala wa vipimo kama zilivyorodheshwa katika tangazo hili. Bofya link hapo chini kufungua nafasi hizo za kazi. BOFYA HAPA

CHELSEA YANG'ARA UGENINI LIGI YA MABINGWA, PSG YAIPIGA BARCA

Image
Kocha Jose Mourinho kulia akimpongeza Nemanja Matic baada ya kufunga bao pekee la ushindi usiku huu CHELSEA imepata ushindi wa ugenini katika Ligi ya Mabingwa Ulaya, baada ya kuifunga Sporting Lisbon ya Ureno bao 1-0, wakati Manchester City imelazimishwa sare ya 1-1 nyumbani na AS Roma ya Italia usiku huu. Katika mchezo wa Kundi G, bao la Nemanja Matic dakika ya 34 limemfanya kocha Jose Mourinho aitambie timu ya nchini kwake, Sporting. Fernandinho wa Manchester City (kushoto) akigombea mpira na Radja Nianggolan wa AS Roma (kulia) Uwanja wa Etihad, Sergio Aguero alitangulia kuifungia City kwa penalti dakika ya nne kabla ya mkongwe Francesco Totti kuisawazishia Roma dakika ya 23 katika mchezo wa Kundi E. Bao pekee la Thomas Mueller dakika ya 22 limeipa Bayern Munich ushindi wa 1-0 ugenini dhidi ya CSKA Moscow ya Urusi katika mchezo mwingine wa Kundi E. mchezo mwingine wa kundi hilo usiku huu, Schalke 04 imelazimishwa sare ya 1-1 nyumbani

NECTA KUTOA VYETI MBADALA KWA SH 100,000

Dar es Salaam. Baraza la Mitihani la Taifa (Necta) limetangaza kuanza kutoa vyeti mbadala kwa gharama ya Sh100,000 kwa wote ambao vyeti vyao vimeharibika kiasi cha kutofaa kwa matumzi. Tangazo hilo lililotolewa jana na Necta, linawalenga wote waliohitimu elimu zao kuanzia Oktoba 2008, ambao vyeti vyao vina picha za watahiniwa husika, huku likifafanua kuwa waliomaliza kabla ya hapo, utaratibu wa kuwatumia uthibitisho wa matokeo katika taasisi zenye mahitaji utaendelea. Kwa mujibu wa tangazo hilo: “Ombi la cheti mbadala litapokewa baada ya miezi mitatu kupita tangu upotevu wa cheti halisi kutangazwa gazetini. Uchunguzi wa uthibitisho utafanyika kwa siku 30 tangu kupokewa kwa ombi la cheti mbadala kwa kuihusisha polisi (kitengo cha uchunguzi wa picha).” Katika kukabiliana na udanganyifu unaoweza kujitokeza kutoka kwa watu wasio waaminifu, baraza hilo lilisema kuwa hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi ya watakaoshiriki katika uombaji wa vyeti hivyo vitakavy

EBOLA YATUA MAREKANI

Image
Mgonjwa wa kwanza wa ugonjwa hatari wa virusi vya Ebola amegundulika nchini Marekani, imethibitishwa katika mji wa Dallas, Texas. Maafisa katika kituo cha afya cha Texas katika hospitali ya Presbyterian wamesema mgonjwa ambaye hakutajwa ametengwa katika hospitali hiyo. Mgonjwa huyo anasemekana kuwa ni mtu anayeaminika kuambukizwa ugonjwa huo nchini Liberia kabla ya kuonyesha dalili za ugonjwa huo. Zaidi ya watu 3,000 tayari wamefariki dunia kutokana na ugonjwa wa Ebola huko Afrika Magharibi na idadi ndogo ya wafanyakazi wa Marekani wa mashirika ya misaada wamepata nafuu baada ya kupelekwa kutibiwa Marekani. Jumatatu, maafisa wa kituo cha afya cha Texas katika hospitali ya Presbyterian ya Dallas wamesema mgonjwa ambaye hakutajwa jina alikuwa akichunguzwa virusi vya Ebola na ametengwa katika hospitali hiyo. Shirika la Afya Duniani, WHO limesema mpaka sasa zaidi ya watu 3,000 wamekufa kutokana na virusi vya Ebola, wengi wa waliokufa ni kutoka Liberia.

DOGO ABAMBWA NA MKE WA KIGOGO GUEST

Image
Tukio hilo lilijiri Septemba 18, mwaka huu kwenye gesti moja maarufu iliyoko… Stori: Waandishi Wetu KABAANG! Kijana mmoja aliyefahamika kwa jina la Marck Costantine (24), mkazi wa mtaa wa Kitangiri jijini Mwanza amenaswa ‘live’ gesti akiwa na mke wa kigogo mmoja (jina kapuni), aitwaye Mwanaidi wakijiandaa kuvunja amri ya sita. Baada ya fumanizi kati ya Serengeti boy aliyefahamika kwa jina la Marck Costantine na mke wa kogogo. Tukio hilo lilijiri Septemba 18, mwaka huu kwenye gesti moja maarufu iliyoko mitaa ya Kitangiri baada ya kigogo huyo kupewa ‘ubuyu’ kwamba anaibiwa mali yake ndipo akaandaa mtego na kufanikiwa kumnasa kijana huyo alipokutwa kwenye chumba namba 4 cha gesti hiyo akijiandaa kuserebuka. “Kigogo alipopewa mchoro huo na wambea, siku ya tukio alimshtua Mwenyekiti wa Mtaa wa Kitangiri, Maginga Patroba, wakatia timu katika gesti hiyo, wakawakuta wachepukaji hao wakiwa kitandani huku Marck akiwa tayari ameshachojoa nguo, Mwanaidi akiwa bado,” kilisema

MAGAZETI YA LEO JUMATANO, OCTOBER 1 YAPO HAPA.

Image