Posts

LULU, WOLPER WAONESHANA JEURI YA MABWANA

Image
Staa katika tasnia ya filamu Bongo, Jacqueline Walper. Sakata la kupangishiwa nyumba za kifahari na wanaume linazidi kuchukua sura mpya kwa mastaa wa kike ndani ya tasnia ya sinema za Kibongo ambapo safari hii mastaa wawili, Elizabeth Michael ‘Lulu’ na Jacqueline Walper ‘ Wolper’ Massawe wanadaiwa kuoneshana jeuri ya mabwana wakipima ni yupi mwenye mshiko zaidi huku akina Wema Isaac Sepetu na Kajala Masanja ambao awali walikuwa juu wakipotezwa. Staa katika tasnia ya filamu Bongo, Elizabeth Michael ‘Lulu’. TAMBO ZA NANI ZAIDI? Uchunguzi wa Ijumaa umebaini kwamba, kumekuwa na kasumba ya baadhi ya mastaa hao kutambiana kuwa ni nani zaidi anayemiliki bwana mwenye mawe au mshiko kuliko wengine. Ilidaiwa kwamba, baada ya Lulu kuripotiwa kupangishiwa bonge la jumba la kifahari na milionea maarufu wa jijini Arusha lililopo maeneo ya Mbezi-Beach jijini Dar, Wolper naye anadaiwa kujibu mapigo kwa kupangishiwa mjengo wa maana na bwana’ke uliopo maeneo hayohayo. Kwa mujibu wa vyanzo vyetu amb

USHINDI WA CHADEMA SUMBAWANGA, VIGOGO CCM TUMBO JOTO

Image
Kufuatia ushindi wa kishindo walioupata Chama cha Demokrasia na Maendeleo  (Chadema) katika uchaguzi wa marudio wa serikali za mitaa uliofanyika wiki hii katika kata tatu za Manispaa ya Sumbawanga mkoani Rukwa, viongozi wa juu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) ngazi ya mkoa na taifa, wanadaiwa kuhaha huku na kule ili kujua chanzo cha kushindwa huko. Kwa mujibu wa chanzo chetu, ushindi huo umewavuruga mno viongozi wa CCM kwani wako tumbo joto na hawakutegemea kuanguka vibaya kama ilivyotokea na vikao mbalimbali vya chama vinaendelea mjini Sumbawanga, kujaribu kutafuta sababu na kurekebisha makosa kabla ya kufanyika kwa uchaguzi mkuu, Oktoba 2015. “Wameanguka vibaya mno, yaani katika mitaa 43, CCM wameambulia viti vitano tu wakati Chadema wamechukua 37 na mtaa mmoja uchaguzi utarudiwa tena, hii haijawahi kutokea. Hivi sasa hapa Sumbawanga hapakaliki, vikao vya CCM kila dakika, wamechanganyikiwa kwa kweli,” kilisema chanzo chetu kwa sharti la kutotajwa jina. Baada ya kupata habari hizo, m

MTAZAMO WA WASANII BONGO UCHAGUZI MKUU 2015

Image
Habari ya mjini kwa sasa ni Uchaguzi Mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani unaotarajiwa kufanyika Oktoba, 2015 ambapo Watanzania wote watatumia haki yao ya msingi ya kupiga kura, kuwachagua viongozi wanaowataka. Showbiz Plus imewatafuta wasanii wa tasnia tofauti Bongo na kuwauliza mtazamo wao juu ya uchaguzi huo na hali ya upepo wa kisiasa Bongo ambapo wamefunguka kama ifuatavyo: MRISHO MPOTO ‘MJOMBA’  Mkali huyu wa kughani na tungo za Kiswahili, yeye amefunguka: “Kwanza kabisa uchaguzi umegawanyika sehemu mbili, kuna viongozi ambao wanahitaji madaraka na kuna wengine wanahitaji kufanya biashara. “Vilevile hata wapiga kura nao wapo wanaojiandaa kufanya biashara kwa kujua kwamba wakimpigia kura kiongozi fulani, watanufaika na kitu fulani, tofauti na zamani ambapo utii na nidhamu kwa viongozi na wapiga kura ulikuwa mkubwa.“Sasa hivi hata wasanii nao wanafanya biashara kwa kutazama mgombea gani ana fedha ndiyo wanaenda kumfanyia kampeni, kwa hali hii tutegemee kuwa uchaguzi utak

SOMA MAGAZETI YA LEO IJUMAA

Image

SALOME KWEKA AFARIKI DUNIA USIKU WA KUAMKIA LEO

Image
Aliyekuwa mke wa Eng. James Kitiganda  Kirahuka, Salome Kweka au Manka amefariki dunia usiku wa kuamkia leo majira ya saa 4:30 usiku katika hospital ya Taifa ya Muhimbili alikokuwa amelazwa katika chumba cha watu mahututi (ICU).  Daima tutakukumbuka Salome umeondoka mapema sana. Kwa taarifa zaidi juu ya msiba utakuwa wapi na mazishi yake utazipata baadaye. Mungu kampenda zaidi.

BODI YA CHAKULA, DAWA NA VIPODOZI ZANZIBAR YATEKETEZA TANI 8.5 ZA DAWA NA VYAKULA.

Image
Wafanyakazi wa Bodi ya Chakula, Dawa na Vipodozi Zanzibar wakiteremsha baadhi ya maboksi ya dawa mbalimbali, vipodozi, mchele, na tende zilizoharibika kwaajili ya kuviangamizwa. Maboksi ya dawa yaliomaliza muda wake yakiangamizwa kwa kuchomwa moto katika eneo la kibele Wilaya Kati Unguja. Mchele ulioingia nchini ambao haufai kwa matumizi ya binaadam na tende vikiangamizwa kwa kuchomwa moto kijiji cha kibele Wilaya Kati Unguja. Mafisa wa  Bodi ya Chakula, Dawa na Vipodozi Zanzibar wakisimamia zoezi la uteketezaji wa dawa, vipodozi, mchele, na tende ambavyo vitu vyote hivyo havifai kwa matumizi ya binadam. ( Picha na Makame Mshenga-Maelezo Zanzibar ).

SOMA MAGAZETI YA LEO ALHAMISI

Image