Posts

VIDEO: HOTUBA YA RAIS JAKAYA KIKWETE YA MWISHO WA MWEZI WA FEBRUARI,2015

AFISA WA NEC ASEMA WANAVYUO WAJIANDIKISHE BILA HOFU YA WAPI WATAKUWA SIKU YA UCHAGUZI

Image
03 Mar20 Washiriki kutoka vyuo mbali mbali vya Mkoa wa Mbeya. Wasomi wa Vyuo vikuu Mkoa wa Mbeya wamesema ratiba ya uchaguzi si rafiki kwa wanafunzi na kuwa inawapa mashaka ikiwa wataweza kushiriki kwenye kupiga kura katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu. Wakizungumza na kwenye mdahalo wa vyuo vikuu uliofanyika mwishoni mwa wiki katika ukumbi wa Chuo kikuu cha Teofilo Kisanji (TEKU) ulioandaliwa na Chama cha Walimu wanaofundisha masomo ya Siasa (CETA), walisema masharti yaliyowekwa na tume ya uchaguzi kwamba ni lazima kila mtu apige kura katika eneo alilojiandikishia linawabagua wanafunzi kutokana na muda wa uchaguzi kuwa eneo tofauti na alipojiandikishia. Walisema asilimia kubwa ya wanafunzi hujiandikisha aidha akiwa chuoni ama nyumbani lakini siku ya uchaguzi huenda akawa sehemu tofauti na alipojiandikishia jambo ambalo linamnyima haki yake ya kupiga kura na kuchagua viongozi. Wanafunzi hao walishauri kuwa endapo tume itaendelea kusimamia msimamo wake ni bora wanafunzi wak

SHAMSA: SIPENDI WANAOLALAMIKA KUTENDWA

Image
Mrembo na mwigizaji wa filamu mwenye mvuto wa aina yake, Shamsa Ford jana mtandaoni ametoa mtazamo wake kuhusu swala la watu kulalamika muda wote kuwa  wametendwa kwenye maswala la mahusiano ya kimapenzi. “Huwa sipendi watu wanaolalamika kutwa kwamba wametendwa bila kuangalia nyuma yeye kawaumiza wangapi ambao waliamua tu kumnyamazia na kumpuuza”. Morning my people. Huwa sipendi watu wanaolalamika kutwa kwamba wametendwa bila kuangalia nyuma yeye kawaumiza wangapi ambao waliamua tu kumnyamazia na kumpuuza A photo posted by shamsa Ford (@shamsaford) on  Feb 28, 2015 at 9:47pm PST

CHADEMA Red Brigade wala kiapo Mwanza Mbele ya Mbowe

Image
02 Mar2015 Vijana wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA, al maarufu kama RED BRIGADE, wakila kiapo cha utii, mbele ya Mwenyekiti wa taifa wa chama hicho, Freeman Mbowe, jijini Mwanza siku ya Jumamosi Februari 28, 2015. Kiapo hicho kinafuatia kukamilika kwa mafunzo ya kiulinzi na usalama kwa vijana hao. Vijana hao wakila kiapo mbele ya Mbowe (kulia) Mkurugenzi wa Ulinzi na Usalama wa CHADEMA, Wilfred Rwakatare (kulia), akisoma taarifa ya mafunzo ya vijana wa chama hicho 'Red Brigade' huku mwenyekiti wa taifa wa chama hicho, Freeman Mbowe (kushoto) akisikiliza. Picha:  K Vis blog

LINAH & RECHO WAFANYA MAMBO YA AIBU KWEUPEE

Image
  Estelina Sanga ‘Linah’ na shostito wake, Winfrida Josephate ‘Recho’ wakilishana keki kwa mdomo. Na MUSA MATEJA/ijumaawikienda Hamnazo? Masistaduu wa Bongo Fleva, Estelina Sanga ‘Linah’ na shostito wake, Winfrida Josephate ‘Recho’, wamefanya mambo ya aibu mbele ya kadamnasi. Tukio hilo la aibu lililoshuhudiwa na Ijumaa Wikienda, lilijiri hivi karibuni usiku kwenye bwawa la kuogelea (swimming pool) ndani ya Hoteli ya Regency-Mikocheni jijini Dar ambapo kulikuwa na ‘bethidei’ ya Recho.Awali, mastaa hao walianza kwa kulishana keki kwa staili ya njiwa (kwa mdomo), jambo lililoibua minong’ono mahali hapo. Winfrida Josephate ‘Recho’. Kama haitoshi, baada ya tukio hilo, wawili hao waliweka mapozi tata wakipiga picha zilizowaonesha nusu utupu huku vinguo walivyovaa vikiacha wazi sehemu kubwa ya maumbile yao nyeti. “Duh! Hawa watoto sasa ni too much, waone walivyojiachia na vivazi vya aibu, yaani hawatazamiki mara mbili,” alisikika mmoja wa wahudhuriaji wa pati hiyo.Baada ya kunasa tukio

MAGAZETI LEO JUMATATU

Image

KIFO CHA KAPTENI JOHN KOMBA NA BAADHI YA KUMBUKUMBU ALIZOZIACHA

Image
Ni huzuni kwa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), Jimbo la Mbinga Magharibi, Taifa, marafiki na familia, baada ya kufikwa na msiba mkubwa wa kiongozi, Mbunge, Kapteni wa Jeshi, Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) na msanii mashuhuri wa Bendi ya Tanzania One Theatre (TOT), Kapteni John Komba. Msiba huo ulitokea jana wakati Kamati Kuu ya CCM, ikiwa katika kikao cha kawaida, kilichokuwa na ajenda muhimu, ikiwemo ya kujadili makada sita waliokuwa wakitumikia adhabu, baada ya kukiuka maadili ya chama na kuanza kampeni za urais mapema. Mbali na makada hao, kikao hicho pia kilikuwa na ajenda ya kujadili makada wengine watatu, waliokuwa wakikabiliwa na kashfa ya kupokea fedha zilizokuwa katika iliyokuwa akaunti ya Tegeta Escrow, iliyokuwa Benki Kuu (BoT). Lakini kabla hata uamuzi wa kikao hicho kutangazwa, Kapteni Komba aliaga dunia na taarifa za awali zilieleza kuwa alikuwa nyumbani kwake Mbezi Beach, akajisikia vibaya na kukimbizwa katika

AZAM TV: MAPITIO YA KURASA ZA MAGAZETI LEO MACHI MOSI 2015

Image

MAAMUZI YA KIKAO CHA KAMATI KUU YA CCM KILICHOFANYIKA JIJINI DAR

NAPE ATAMKA MAAMUZI YA CCM KUHUSU CHENGE,NGELEJA, PROF. TIBAIJUKA NA WASAKA URAIS

Image
Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete akiongoza kikao cha Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa huko Ikulu jijini Dar es Salaam siku ya Jumamosi ya Februari 28, 2015. Wa pili kulia ni Rais wa Zanzibar Dkt. Ali Mohamed Shein na wawatu kulia ni Makamu wa Rais Dkt. Mohamed Gharib Bilal.K ushoto ni Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana. Kamati Kuu ya CCM (CC) imewasimamisha uongozi wa vikao vya chama, vigogo watatu wa chama hicho, akiwemo Waziri wa zamani wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Profesa Anna Tibaijuka kutokana na kuhusishwa na sakata la Escrow. Wengine waliosimamishwa kuhudhuria vikao vinavyohusu uamuzi wa chama ni pamoja na Mbunge wa Bariadi Magharibi, Andrew Chenge na Mbunge wa Sengerema, William Ngeleja. Hatua hiyo inatokana na uamuzi wa Kamati Kuu iliyoketi Januari, mwaka huu Zanzibar, kuagiza Kamati ndogo ya Maadili kuwaita na kushughulikia suala la viongozi wa chama hicho, waliokuwemo katika vikao vya uamuzi ya chama hicho waliohusishwa na sak

MAONI YA MWALIMU MABALA KUHUSU LUGHA NA MFUMO WA ELIMU

Image
Ni dhahiri kwamba mabadiliko ya lugha peke yake hayatafufua mfumo wa elimu. Iwapo mtu ana kisukari, shinikizo la damu na UKIMWI, kupunguza sukari peke yake haitatosha. Pili kwangu mimi ni dhahiri kwamba watu wanashindwa kutofautisha kati ya umuhimu wa Kiingereza kama lugha kwa wanafunzi wetu na umuhimu wa Kiingereza kama lugha ya kufundishia. Nadhani hakuna anayebisha juu ya umuhimu wa Watanzania kujua Kiingereza. Lakini wengi tunabisha sana kwamba njia bora ya kufanya watu waelewe Kiingereza ni kukitumia kama lugha ya kufundishia. Mimi nimefundisha shule za sekondari na ninajua kwamba a) Wako wanafunzi wanaokataa mapema sana Kidato cha Kwanza kwa sababu hawaelewi kitu. b) Wapo wachache ambao waliweza kupambana vikali na lugha hadi waliweza kuwashinda waliotoka kwenye English Medium Schools. Lakini hawa ni wachache. c) Mimi kama mwalimu wa masomo mengine kama historia au fizikia nakereka sana kupata shida kufundisha somo langu na kueleweka kwa sababu ya kutumia lugha ambayo w

SOMA MAGAZETI YA LEO JUMAPILI

Image