Posts

KILICHOANDIKWA NA MAGAZETI YA LEO JUNE 3,

Image

PICHA NA VIDEO:WAZIRI MKUU MSTAAFU FREDERICK SUMAYE ATANGAZA NIA YA KUWANIA URAIS KUPITIA CCM

Image
 Waziri Mkuu Mstaafu Frederick Sumaye, akiingia ukumbini katika Hoteli ya Hyatt Regency Kilimanjaro Dar es Salaam leo asubuhi akiwa ameongozana na mke wake Ester Frederick Sumaye kwa ajili ya kutangaza nia ya kuwania nafasi ya urais wakati ukifika iwapo jina lake litapitishwa na chama chake cha CCM.       Waziri Mkuu mstaafu  Sumaye akiwa na mke wake  Ester Sumaye wakati wa mkutano huo wa kutangaza nia.   Waziri Mkuu mstaafu Sumaye  (kulia), akizungumza na wanahabari na wadau wengine wakati akitangaza nia hiyo .  Waziri Mkuu mstaafu Sumaye (katikati), akiwa meza kuu. Kutoka kulia ni Katibu Mwenezi wa CCM Kata ya Kiluvya, Juma Semendu Nauchiwa. Kada wa CCM, Shabani Uronu, Mama Ester Sumaye na Aliyekuwa Mbunge wa Ubungo, Charles Kaenja.  Mwanahabari Ibrahim Yamola akimuuliza swali Waziri mstaafu Sumaye baada ya kutangaza nia ya nafasi hiyo.     Mwanahabari Mariam Mziwanda akimuuliza swali Waziri mstaafu Sumaye baada ya kutangaza nia ya nafasi hiyo.  W

Rais Kikwete aanza ziara ya nchi tatu Ulaya.

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI Rais Kikwete aanza ziara ya nchi tatu Ulaya . Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete leo, Jumatatu, Juni Mosi, 2015 ameanza ziara rasmi ya wiki moja katika nchi tatu za Ulaya kwa mwaliko wa viongozi wa nchi hizo. Rais Kikwete ambaye aliondoka nchini usiku wa jana, Jumapili, Mei 31, 2013 baada ya kumaliza kuendesha Mkutano wa Wakuu wa Nchi Wanachama wa Jumuia ya Afrika Mashariki (EAC) kuhusu Burundi ameanzia ziara yake katika Finland ambako atakaa kwa siku tatu.    Baadaye, Rais Kikwete atatembelea nchi za Sweden na Uholanzi kabla ya kurejea nyumbani. Katika Finland, Rais Kikwete miongoni mwa mambo mengine kesho Jumanne, Juni 2, 2015, atafanya mazungumzo rasmi ya Kiserikali na Rais wa nchi hiyo na baadaye atatembelea Bunge la nchi hiyo ambako atafanya mazungumzo na Wabunge. Imetolewa na: Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais, Ikulu, DAR ES SALAAM. 1 Juni, 2015

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumanne ya Tarehe 2 Juni 2015

Image

HABARI ZILIZOTAWALA MAGAZETI YA LEO JUNE 1

Image