Posts

Rose Ndauka: Nipo tayari kuolewa na yeyote!

Image
ROSE Donatus Anjelus Ndauka ‘mtata’ amesema kama mwanamke aliyekamilika na mwenye kuhitaji heshima katika jamii, yupo tayari kuolewa na kuishi kama mama na mwanaume yeyote. Akichonga  Rose alisema japo mume bora anatoka kwa Mungu na kwamba anangojea aliye chaguo lake, lakini amechoshwa na hali ya kuishi bila ndoa. “Mimi kama mwanamke ninayetoka kwenye familia yenye maadili, inafika wakati natamani kuishi katika ndoa, natamani kuwa na familia yangu na mume wangu na kwa sasa akitokea yeyote, nikajihakikisha kuwa anavyo vigezo ninavyovihitaji, hakika niko tayari kuanzisha naye safari ya maisha,” alisema Rose. Awali Rose alikuwa na uhusiano na msanii wa Bongo Fleva, Malick Bandawe ‘King Chiwaman’ na kufanikiwa kupata mtoto mmoja na mwishoni mwa mwaka jana waliachana.

Pedro wa Barcelona kutua Chelsea kukamilisha usajili leo

Image
Chelsea have beaten Manchester United in the chase to sign Pedro from Barcelona and Old Trafford manager Louis van Gaal faces more misery in his bid to prise Sadio Mane from Southampton. Jose Mourinho made a personal intervention to beat his old mentor Van Gaal to Pedro. Mourinho's personal call helped convince the 28-year-old Spain striker Stamford Bridge was the right destination. Chelsea struck a deal for £21.1million, with £19m paid up front, more than United offered. Pedro is expected to complete the transfer after a medical on Thursday and be available for Sunday's game at West Bromwich Albion if there are no complications. Manchester United were in pole position to sign Pedro but Chelsea made a late bid for the Barcelona attacker Jose Mourinho (left) made a personal call to Pedro in order to beat Louis van Gaal (right) to his signature Pedro, pictured in action against Athletic Bilbao this week, will undergo a

Mamilioni yatengwa kumpora Diamond Mtoto!

Image
Sakata la yule jamaa aitwaye King Lawrence, raia wa Uganda mwenye maskani yake nchini Afrika Kusini ‘Sauz’ anayedai kuwa mtoto wa staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ aliyempata kupitia kwa mwandani wake, Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’, Latifah Nasibu ‘Princes Tiffah’ siyo wa mwanamuziki huyo, limechukua sura mpya. Jamaa huyo amefunguka upya kwamba, ametenga mamilioni ya fedha kumpora Diamond bintiye Tiffah. KING LAWRENCE AMGEUKA IVAN Kabla ya kutenga mamilioni hayo, King Lawrence ambaye ni rafiki wa aliyekuwa mume wa Zari, Ivan Ssemwanga aliposti kwenye akaunti yake ya Instagram kile kinachoonekana ni barua ya kutaka kufanyika vipimo vya DNA ili kubaini Tiffah ni damu ya nani huku barua hiyo ikimtaja King Lawrence kuwa ndiye mhusika. Pia kabla ya barua hiyo iliyoandikwa na kusainiwa na kampuni ya wanasheria ya Uganda ya Web Advocates & Solicitors, King Lawrence alikaririwa akidai kwamba Tiffah ni damu ya Ivan hivyo kitendo cha kudai ni damu yake kimezidi

DK MAGUFULI "ATAMBULISHWA KWA WAZEE WA DAR"

Image
Mwenyekiti wa CCM Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimtambulisha Mhe Samia Suluhu Hassan, mgombea mwenza wa Urais kwa tiketi ya Chama hicho tawala leo Agosti 19, 2015 katika ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam. Mgombea Urais kwa tiketi ya CCM, Dkt John Pombe Magufuli akiongea na wazee wa Dar es Salaam leo Agosti 19, 2015 katika ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam. (P.T) Mwenyekiti wa Wazee wa CCM wa Dar es Salaam akipeana mikono na Mgombea Urais kwa tiketi ya CCM tawala Dkt John Pombe Magufuli baada ya kuongea na wazee wa Dar es Salaam Mwenyekiti wa Wazee wa CCM wa Dar es Salaam akipeana mikono na Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM Samia Suluhu Hassan. Picha: Ikulu

LIGI KUU; SIMBA KUANZA NA AFRICAN SPORTS TANGA, YANGA WAKO NA COASTAL TAIFA

Image
Ratiba ya Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL) imetoka leo ambapo jumla ya timu 16 zinashiriki ligi hiyo itakayoanza kutimua vumbi Septemba 12 katika viwanja tofauti nchini na kumalizika Mei 7, 2016. TFF inazisisitiza klabu kukamilisha usajili wao wa wachezaji na viongozi kabla ya kufungwa kwa dirisha hilo la usajili kesho alhamisi Agosti 20, 2015. Baada ya kufungwa kwa usajili huo hakutakua na muda tena wa nyongeza. Kwa klabu ambayo haitawasilisha malipo ya ada ya mchezaji wa kigeni ya dola elfu mbili (U$D 2000) mchezaji huyo hataruhusiwa kucheza kwenye ligi hadi malipo hayo yatakapofanyika. Michezo saba itachezwa siku ya ufunguzi jumamosi katika viwanja tofauti ambapo Ndanda Vs Mgambo Shooting (Nang’wanda - Mtwara), African Sports Vs Simba SC (Mkwakwani - Tanga), Majimaji Vs JKT Ruvu (Majimaji - Songea), Azam FC Vs Tanzania (Azam Complex - Dsm), Stand United Vs Mtibwa Sugar (Kambarage - Shinyanga), Toto Africans Vs Mwadui (CCM Kirumba - Mwanza), na siku ya jumapili Yo

LOWASSA, BABU DUNI WASAINI HATI YA KIAPO YA KUGOMBEA URAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

Image
Mgombea urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa akisaini fomu za hati ya Kiapo kwenye ofisi za Jaji wa Mahakama ya Tanzania, Jijini Dar es salaam leo Agosti 19, 2015. Hati ambayo kila mgombea wa nafasi ya urais anatakiwa kusaini katika mahakama kuu jijini Dar es Salaam . Mgombea mwenza wa urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dkt. Juma Haji Duni akisaini fomu za hati ya Kiapo kwenye ofisi za Jaji wa Mahakama ya Tanzania, Jijini Dar es salaam leo Agosti 19, 2015. Kushoto kwake ni Mgombea urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama hicho, Mh. Edward Lowassa. Mgombea urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa na Mgombea Mweza wake, Dkt. Juma Haji Duni wakiwa kwenye ofisi za Jaji wa Mahakama ya Tanzania, Jaji Suleiman Said Komu (

HATIMAYE Mrembo Machachari wa Kenya Huddah Monroe Atulizwa Kwa Kuvishwa Pete ya Uchumba

Image
Huddah Monroe MREMBO kutoka nchini Kenya, Huddah Monroe, ameanza kuionesha pete ya uchumba aliyovishwa wiki iliyopita. Mwanamitindo huyo mwenye umaarufu mkubwa nchini humo, ameamua kuvunja ukimya wake na kuionesha pete hiyo kupitia akaunti yake ya Instagram. “Kila kitu kipo wazi, lakini muda ukifika watu watamjua nani aliyenivisha pete hii, lakini kwa sasa watu wanatakiwa wajue nina pete ya uchumba. “ Kwa sasa naweza kusema sihitaji usumbufu kutoka kwa mwanamume yeyote, huu ni muda wangu wa kutulia na kufanya maisha na mume wangu mtarajiwa, ” alieleza Huddah.

Hackers Waigeuza Akaunti ya Instagram ya Fid Q Kuwa ya Wema Sepetu!

Image
Kama unaitafuta akaunti ya Instagram ya Fid Q kuanzia jana bila mafanikio basi fahamu kuwa hackers wameitaifisha, kufuta picha zake zote na kuigeuza kuwa ya Wema Sepetu. Akaunti hiyo ina followers zaidi 160,000. “Account hii imekuwa hacked jana usiku ila mimi nimegundua leo asubuhi,” Fid ameiambia Clouds FM. “ Niligundua baada ya kuingia katika account ikawa inanigomea. Mimi nilikuwa nimeandika mwanaharakati, sasa naona wameamua kubadili na jina na kuandika jina la Wema Sepetu, ” alisema.

THAILAND: “UCHUNGUZI UMEANZISHWA KUJUA ALIYEHUSIKA NA MASHAMBULIZI”

Image
Baadhi ya raia kutoka China, Hong Kong, Malaysia na Singapore ni miongoni mwa watu waliouawa katika shambulio lililotokea katika mji wa Bangkok, Jumatatu Agosti 17, 2015. Na RFI Idadi ya watu waliouawa katika shambulio lililotokea katika mji wa Bangkok, imeongezeka na kufikia 21, huku watu 125 wakiripotiwa kujeruhiwa. baadhi ya raia kutoka China, Hong Kong, Malaysia na Singapore ni miongoni mwa waliouawa. Uraia wa baadhi ya miili iliyopatikana, haujafahamika. Hata hivyo, polisi imemtambua mtuhumiwa mmoja kupitia kamera za usalama ziliowekwa kwenye eneo takatifu kwa watu kutoka jamii ya Hindu ambapo bomu lililipuka. Wizara ya ulinzi ya Thailand inasema kuwa watu waliotega mabomu katika eneo takatifu jijini Bangkong waliwalenga watalii. Wizara hiyo imeongeza kuwa inawasaka waliotega mabomu hayo yaliyolipuka Jumatatu jioni wiki hii na kusabisha vifo vya watu 21 na wengine 120 kujeruhiwa. Eneo hilo lililongwa limekuwa kivutio kikubwa cha watalii na raia wa nchi hiyo amba

OSCAR PISTORIUS KUACHIWA IJUMAA

Image
Mwanariadha Oscar Pistorius. Oscar Pistorius akiwa na mpenzi wake Reeva Steenkamp. Oscar Pistorius akiwa mahakamani wakati wa kesi yake. Mwanariadha mahiri wa nchini Afrika Kusini, Oscar Pistorius anatarajiwa kuachiwa Ijumaa hii baada ya kuonyesha tabia nzuri akiwa gerezani. Pistorius alihukumiwa kifungo cha miaka mitano gerezani mwaka uliopita kwa kosa la kumuua mpenzi wake, Reeva Steenkamp katika usiku wa Siku ya Wapendanao 'Valentine's Day'. Pistorius ametumikia kifungo cha miezi 10 pekee gerezani kati ya miaka mitano aliyohukumiwa. Baada ya kuachiwa, Pistorius anatarajiwa kuwa akitumikia muda wake uliobaki akiwa katika kifungo cha nje. Wakati akitoa hukumu ya staa huyo, Jaji Thokozile Masipa alisema kuwa kiongozi wa mashtaka nchini Afrika Kusini alishindwa kuthibitisha kuwa Pistorius alikusudia kumuua mpenzi wake Reeva Steenkamp alipompiga risasi nyumbani kwake akidhani kuwa ni mwizi.

Lulu ‘kajibebisha’ kwa Diamond Platnumz amchokonoa Zari

Image
Chanzo:GPL UCHOKOZI! Staa wa sinema za Kibongo, Elizabeth Michael 'Lulu' anatengeneza kichwa cha habari kwa mara nyingine baada ya kudaiwa ‘kujibebisha’ kwa staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul 'Diamond Platnumz', kitendo kilichotafsiriwa kuwa ni kumchokonoa mwandani wa jamaa huyo, Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’ . Tukio hilo lilijiri usiku mnene Jumapili iliyopita kwenye Ukumbi wa House Club uliopo Masaki, Dar ambapo kulikuwa na sherehe ya bethdei ya DJ wa Diamond, Rommy Jones. Kwa mujibu wa shuhuda wetu aliyeweka kambi ukumbini humo, Lulu, bila kujali kwamba, Diamond alimwacha Zari nyumbani akimnyonyesha ‘baby girl’ wao, Latifah Nasibu a.k.a ‘Princess Tiffah’, alionekana akijiachia naye kimahaba huku akionesha ‘kummisi’ kinoma jamaa huyo. ILIANZA HIVI Lulu, alikuwa wa mwishomwisho kuingia ukumbini ambapo baada ya kuzunguka kusalimiana na mastaa wengine alitua kwenye sofa alilokuwa amekaa Diamond ambapo walianza kufanya yao bila kujali ëwavimba machoí wa

TAYARI 3 WAMEFARIKI KWA KIPINDUPINDU DAR, 34 WAMELAZWA

Image
Watu watatu (wanawake 2, mwanaume 1) wamefariki dunia na wengine 34 wamelazwa katika hospitali ya Rufaa ya Mwananyamala na hospitali ya Mburahati jijini Dar es Salaam baada ya kuugua kipindupindu. Hospitali ya Sinza Palestina imeripotiwa kuwa na wagonjwa walio na dalili za ugonjwa huo zaidi ya 50. Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar, Mkuu wa wilaya ya Kinondoni Bw. Paul Makonda amezitaja Kata zilizoathirika na ugonjwa huo kuwa ni Kijitonyama, Kimara, Manzese, Tandale, Saranga, Makumbusho na Mwananyamala. Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Saidi Meck Sadiki, amesema kuna ripoti ya wagonjwa waliolazwa 71 hadi sasa, na kwamba Wilaya ya Ilala na Temeke bado hazijakumbwa na ugonjwa huo. Akizungumza na wanahabari Jijini Dar es Salaam, Mganga Mkuu wa Minispaa hiyo, Dk. Aziz Msuya, amesema kuwa mgonjwa wa kwanza aligunduliwa katika maeneo ya Kijitonyama kwa Ally Maua na kufia nyumbani kwake katika eneo hilo na kuambukiza ndugu zake wawili ambao walikufa wakati wanapelekwa