Wanavijiji 4 Hanang' vyapokea hati za umiliki wa kimila wa ardhi
Wenyekiti wa vijiji vinne vya wilaya ya Hanang’ wamepokea hati za hakimiliki za kimila za ardhi ya vijiji vyao baada ya kuwa vimepimwa na wao kupewa mafunzo ya matumizi bora ya ardhi kwa ufadhili uliotolewa na shirika la Oxfam kupitia shirika la Ujamaa Community Resource Team - UCRT. Vijiji hivyo vya Mureru, Ming'enyi, Dirma na Gehando vimekabidhiwa hati hizo na katibu tawala wa Wilaya ya Hanang’ John Gabriel aliyemuwakilisha mkuu wa wilaya hiyo katika hafla fupi iliyofanyika katika kijiji cha Mureru na kuhudhuriwa na wakazi zaidi ya 100 kutoka katika vijiji hivyo vinne. Akiongea kwa niaba ya wenyeviti wa vijiji hivyo vinne, Mbisha Gicharoda ambaye ni mwenyekiti wa kijiji cha Ming’enyi aliyashukuru mashirika ya Oxfam na UCRT kwa kuwapatia elimu ya matumizi bora ya ardhi na kuwasaidia kupata hati za hakimiliki za ardhi ya vijiji. "Sisi kama wafugaji tulikua hatujui thamani ya ardhi yetu, sasa tumeamka na kujua haki zetu na manufaa ya kuwa na cheti cha umil