Posts

Taarifa ya maamuzi 6 ya NEC: Watakaoruhusiwa na Watakaozuiliwa kupiga kura

Image

Marekebisho ya NEC 22.10.2015 ya Ratiba ya Kampeni za Uchaguzi Mkuu

Image

JESHI LA POLISI KUIMARISHA ULINZI SIKU YA KUPIGA KURA

Image
Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Ernest Mangu akionyesha waandishi wa habari jana (hawapo pichani) kitabu cha maadili ya uchaguzi kilichosainiwa na viongozi wa vyama vya siasa waliosimamisha wagombea katika uchaguzi mkuu utakaofanyika Oktoba 25. Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Ernest Mangu akionyesha waandishi wa habari (hawapo pichani) kitabu cha maadili ya uchaguzi kilichosainiwa na viongozi wa vyama vya siasa waliosimamisha wagombea katika uchaguzi mkuu utakaofanyika Oktoba 25 ambapo amewataka watu wote kutii sheria bila shuruti wakati wa uchaguzi. Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Ernest Mangu akifafan jam

Mahojiano maalumu: Lowassa @AzamTv - Afya, Tuhuma, Kampeni

Uchambuzi wa NIPASHE kuhusu ahadi za wagombea Urais Tanzania 2015

Image
Huku zikiwa zimebaki siku 10 kabla ya kufikiwa kwa siku ya uchaguzi mkuu Oktoba 25, wagombea urais wanaochuana kwa karibu kutokana na wingi wa watu wanaojitokeza katika kampeni zao, Dk. John Magufuli wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), na Edward Lowassa wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) wanaendelea kutoa ahadi nzito kadhaa kwa wapiga kura. Kadiri inavyoonekana, ahadi hizo zikitekelezwa kwa asilimia 100, zitafanya muujiza kwa kuibadili Tanzania kutoka katika hali duni ya upatikanaji wa baadhi ya huduma za jamii na kuonekana kama `Ulaya'. Uchunguzi uliofanywa na Nipashe kwa wiki kadhaa tangu kampeni za uchaguzi mkuu kuanza rasmi Agosti 22, mwaka huu, umebaini kuwa hadi sasa, Magufuli na Lowassa wameshatoa ahadi nyingi nzito na ambazo zikitekelezwa kwa ukamilifu pindi yeyote kati yao akishinda zitaibadili kwa kiasi kikubwa Tanzania itakayoachwa na serikali ya Rais Jakaya Kikwete. Uchunguzi huo wa Nipashe pia umebaini kuwa kati ya ahadi zote, zipo tano zinaz

DK MAGUFULI ASHIRIKI KUUPOKEA MWILI WA MAREHEMU DK KIGODA DAR

Image
 Mke wa mgombea urais kwa tiketi ya CCM, Janeth Magufuli (kulia) pamoja na Mkuu wa mkoa wa Tanga Mhe.Mwantum Mahiza wakiwa wamemshikilia mke wa aliyekuwa Waziri wa Viwanda na Biashara marehemu Abdallah Kigoda mara tu baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere.  Mgombea urais kupitia tiketi ya CCM Dk. John Pombe Magufuli akimsikiliza mtoto wa aliyekuwa Waziri wa Viwanda na Biashara marehemu Abdallah Kigoda, Omary Abdallah Kigoda mara baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.  Mgombea Urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli (kulia) akizungumza na Binti wa Marehemu Amina Kigoda ,katikati ni mkuu wa mkoa wa Tanga Mhe. Mwantumu Mahiza. Mgombea urais kupitia tiketi ya CCM Dk. John Pombe Magufuli akimpa pole mke wa marehemu.  Mgombea urais kupitia tiketi ya CCM Dk. John Pombe Magufuli (katikati) akiwa pamoja na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue pamoja na Balozi wa Tanzani

Tanzia! Dk Makaidi aaga dunia

Image
Emmanuel Makaidi Mwenyekiti wa chama cha siasa NLD, Dk Emmanuel Makaidi (74) amefariki dunia hii leo Oktoba 15, 2015  mchana katika hospitali ya Nyangao mkoani Lindi kwa kile kilichotaarifiwa kuwa ni shinikizo la damu. Kifo cha Makaidi kimethibitishwa na viongozi wa NLD ambao wanadai kupata taarifa kutoka kwa mjane wa marehemu, Modesta Ponera-Makaidi. Dk Makaidi ambaye alikuwa ni Mwenyekiti Mwenza wa vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA) unaoundwa na vyama vya NLD, CHADEMA, CUF, na NCCR Mageuzi, pia alikuwa akiwania Ubunge wa Masasi Mjini katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu. Marehemu Dk Emmanuel Makaidi, mhandisi aliyebobea, alizaliwa Aprili 10, 1941 huko wilayani Masasi mkoani Mtwara. Baba yake mzazi alikuwa ni katekista wa Kanisa la Anglikana. Alianza elimu katika Shule ya Msingi Namalenga wilayani Masasi kati ya mwaka 1948 – 1952, mwaka 1953 – 1954 alisoma katika Shule ya Kati (Middle school) iitwayo Luatala hukohuko Masasi. Baadaye al

Wanavijiji 4 Hanang' vyapokea hati za umiliki wa kimila wa ardhi

Image
Wenyekiti wa vijiji vinne vya wilaya ya Hanang’ wamepokea hati za hakimiliki za kimila za ardhi ya vijiji vyao baada ya kuwa vimepimwa na wao kupewa mafunzo ya matumizi bora ya ardhi kwa ufadhili uliotolewa na shirika la Oxfam kupitia shirika la Ujamaa Community Resource Team - UCRT. Vijiji hivyo vya Mureru, Ming'enyi, Dirma na Gehando vimekabidhiwa hati hizo na katibu tawala wa Wilaya ya Hanang’ John Gabriel aliyemuwakilisha mkuu wa wilaya hiyo katika hafla fupi iliyofanyika katika kijiji cha Mureru na kuhudhuriwa na wakazi zaidi ya 100 kutoka katika vijiji hivyo vinne. Akiongea kwa niaba ya wenyeviti wa vijiji hivyo vinne, Mbisha Gicharoda ambaye ni mwenyekiti wa kijiji cha Ming’enyi aliyashukuru mashirika ya Oxfam na UCRT kwa kuwapatia elimu ya matumizi bora ya ardhi na kuwasaidia kupata hati za hakimiliki za ardhi ya vijiji. "Sisi kama wafugaji tulikua hatujui thamani ya ardhi yetu, sasa tumeamka na kujua haki zetu na manufaa ya kuwa na cheti cha umil

PPRA Yafungia Makampuni 7 Kwa Udanganyifu, Yatoa Ripoti ya Mwaka

Image
Mwenyekiti wa Bodi ya PPRA, Balozi Matern Lumbanga Mwenyekiti wa Bodi ya PPRA, Balozi Matern Lumbanga (Kulia) akiongea na waandishi wa habari, Kushoto ni Afisa Mtendaji Mkuu wa PPRA, Dk. Laurent Shirima. Mamlaka ya Ununuzi wa Umma (PPRA), imeyafungia makampuni 7 pamoja na wakurugenzi wake kutokana na vitendo vya udanganyifu. Akizungumza na waandishi wa habari leo katika makao makuu ya PPRA, Mwenyekiti wa Bodi ya PPRA, Balozi Matern Lumbanga amesema kuwa Mamlaka hiyo imeamua kuyafungia makampuni hayo kwa mujibu wa kifungu cha 62 cha Sheria ya Manunuzi ya Umma Na. 7 ya Mwaka 2011 na Kanuni ya 98 ya Tangazo la Serikali Na. 446 la Mwaka 2013. Aidha, Balozi Lumbanga alisema kuwa kati ya makampuni hayo, Gagaja Contractors Company Limited, limefungiwa kwa kipindi cha miaka 10 (kutoka tarehe 2 Oktoba,2015 hadi 1 Octoba, 2025) kwa kosa la kuwasilisha dhamana za zabuni za kughushi wakati wa michakato ya zabuni. Aidha, Balozi Lumbanga alisema kuwa m

Maonyesho ya Mavazi Kuhamasisha AMANI TANZANIA

Image

Magoli ya Mbwana Samatta katika mechi dhidi ya Al Merreikh na kuifikisha TP Mazembe fainali.

Image
          Klabu ya TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo imetinga hatua ya fainali ya Ligi ya Mabingwa barani Afrika baada ya kuibuka na ushindi wa goli 3-0 dhidi ya klabu ya Al Merreikh ya Sudan , huu ni mchezo wa pili wa marudiano baada ya ule wa awali kuchezwa Sudan wiki kadhaa nyuma. Mtanzania Mbwana Samatta amesaidia timu yake kupata ushindi wa goli 3-0 katika mechi hiyo ya marudiano baada ya kufunga goli mbili dakika ya 53 na 69 kabla ya Assale kupachika goli la tatu dakika ya 71. TP Mazembe inaingia hatua ya fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika baada ya kuifunga Al Merreikh  kwa jumla ya goli 4-2 idadi ya goli hizo ni pamoja na mechi ya kwanza Sudan . Mtanzania mwingine anayeichezea klabu hiyo Thomas Ulimwengu alipata nafasi ya kuingia dakika ya 58 ya mchezo baada ya kuchukua nafasi ya Kalaba , Ulimwengu hakupata nafasi ya kufunga goli ila alikuwa ni moja kati ya waliotengeneza goli la pili

Rais Kikwete ateua Wakuu wapya wa Wilaya 13 na kuhamisha 7

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amewateua wakuu wa wilaya wapya 13 na kuwahamisha vituo vya kazi wengine saba. Wakuu wa wilaya 13 walioteuliwa ni Shaaban Athuman Ntanambe ambaye anakuwa Mkuu wa Wilaya ya Chato, Mkoa wa Kagera; Thabisa Mwalapwa ambaye anakuwa Mkuu wa Wilaya ya Hanang, Mkoa wa Manyara; Richard Kasesera ambaye anakuwa Mkuu wa Wilaya ya Iringa, Mkoa wa Iringa, Ruth Msafiri ambaye anakuwa Mkuu wa Wilaya ya Kibondo, Mkoa wa Kigoma na Abdallah Njwayo ambaye anakuwa Mkuu wa Wilaya ya Kilwa, Mkoa wa Lindi. Wakuu wa Wilaya wengine wapya ni Asumpta Mshama ambaye anakuwa Mkuu wa Wilaya ya Wanging’ombe, Mkoa wa Njombe; Mohammed Mussa Utaly ambaye anakuwa Mkuu wa Wilaya ya Mpwapwa, Mkoa wa Dodoma; Dauda Yasin ambaye anakuwa Mkuu wa Wilaya ya Makete, Mkoa wa Njombe; Honorata Chitanda ambaye anakuwa Mkuu wa Wilaya ya Ngara, Mkoa wa Kagera; Vita Kawawa ambaye anak