Posts

UN: MAELFU YA RAIA WAMEUAWA IRAQ

Image
Takriban watu milioni 3.2 wamelazimika kuhama makwao nchini Iraq Umoja wa Mataifa unasema kuwa ghasia zinazowakumba raia nchini Iraq ni nyingi huku takriban watu 18,800 wakiuawa kati ya tarehe mosi mwezi Januari mwaka 2014 na 31 mwezi Oktoba mwaka 2015. Takriban watu milioni 3.2 wamelazimika kuhama makwao ndani ya nchi katika kipindi hicho kulingana na ripoti mpya ya UN. Umoja wa mataifa unawalaumu wanamgambo wa Islamic State kwa kuendesha ghasia na kuwashikilia watumwa watu 3,500, wengi wakiwa ni wanawake na watoto. Islamic state wanawashikilia watumwa 3,500 wengi wakiwa ni wanawake na watoto Kamishna mkuu wa Umoja wa Mataifa anayehusika na haki za binadamu Zeid Raad Al Hussein anasema ripoti hiyo inaonyesha kile wakimbizi kutoka Iraq wanatoroka wakati wanakimbilia Ulaya na maeneo mengine. Ripoti hiyo inatokana na mahojiano na wale waliohama makwao na ushuhuda wa moja kwa moja kutoka kwa waathiriwa au wale walioshuhudia ukiukaji wa haki za binadamu Ripoti hiyo i

MAGAZETI YA LEO JUMATANO,JANUARY 20

Image

BURKINA FASO: ZOEZI LA KUWATAMBUA WAHANGA LAENDELEA

Image
Polisi wa Ufaransa wanachunguza gari lililochomwa moto mbele ya hoteli ya Splendid katika mji wa Ouagadougou, Burkina Faso, Januari 17, 2016. Na RFI Baada ya mashambulizi dhidi ya hotli ya Splendid na mgahawa wa Cappuccino katikati mwa mji mkuu wa Burkina faso, Ouagadougou siku ya Ijumaa usiku, wachunguzi wanaendelea na kazi ngumu ya kuwatambua watu 29 waliouawa katika shambulio hilo. Mpaka sasa giza bado linatanda kuhusu namna operesheni ya vikosi vya usalama ilivyoendeshwa. Mwendesha mashitaka wa Mahakama Kuu ya Ouagadougou, Maïza Sérémé, ametoa sehemu ya orodha ya watu waliopoteza maisha katika mashambulizi hayo ya kigaidi yaliyolenga hoteli ya Splendid na migahawa ya Cappuccino na Taxi Brousse. Kati ya wahanga 29 waliohesabiwa, saba bado hawajatambuliwa, ikiwa ni pamoja na watu wanne weusi na wazungu watatu. Kati ya wahanga 22 waliotambuliwa, kuna wanne kutoka Canada, saba wa Burkina Faso, wawili kutoka Ukraine, Mfaransa mmoja mwenye asili ya Ukraine, Wafaransa waw

MGODI WA BUZWAGI WAPONGEZWA KWA KUZINGATIA SHERIA ZA MAZINGIRA

Image
Meneja wa kinu cha kuchenjua dhahabu wa Mgodi wa Buzwagi Festo Shayo (wa kwanza kulia) akitoa maelezo kwa Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais anaeshughulikia mazingira na Muungano, Luhaga Mpina namna mgodi wake unavyohifadhi maji yaliyotumika kusafishia dhahabu. Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais-Mazingira na Muungano Luaga Mpina (wa kwanza kushoto), akisikiliza maelezo ya Afisa Mazingira wa Mgodi wa Buzwagi bwana Frank Ngoroma (wa kwanza mkono wa kulia), aliyesimama katikati ni meneja mkuu wa mgodi wa Buzwagi Mhandisi Asa Mwaipopo. Mh Luhaga Mpina akisisitiza jambo wakati wa ziara hiyo katika eneo la kituo cha Uthibiti wa taka mbalimbali mgodini hapo. Naibu Waziri pamoja na wataalamu wake wakikagua moja ya maeneo ambayo NEMC yalitoa ushauri kuwa yafanyiwe kazi katika ziara zao, ambapo wakati wa ziara hii utekelezwaji wake ulikutwa umeisha kamilika kama walivyokuwa wameelekezwa Mmoja wa maafisa wa mazingira aliyekuwa ameandamana na naibu Waziri akiuliza jamb

MAGAZETI YA LEO JUMATATU, JANUARY 18

Image