Posts

MAGAZETI YA JUMANNE, APRIL 5

Image

RAIS MAGUFULI AIHIRISHA SHAMRA SHAMRA ZA MUUNGANO,AAMURU FEDHA ZAKE ZITUMIKE UPANUZI WA UJENZI BARABARA YA AIRPOT- MWANZA

Image

HESLB yasaini mkataba na CreditInfo kwa ajili ya mabenki kupata taarifa za wadaiwa

Image
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa HESLB Bw. Jerry Sabi (kushoto) na Bw. Davith Kahwa, Mtendaji Mkuu wa CreditInfo Tanzania Ltd wakibadilishana nakala za mkataba. Wengine ni Bw. Robert Kibona na Bw. Frimat Tarimo kutoka HESLB na Bw. Van Reynders, Meneja wa CreditInfo Tanzania. (Picha: HESLB) Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) mwishoni mwa wiki imesaini mkataba na Kampuni ya CreditInfo Tanzania Ltd utakaowezesha taarifa za wadaiwa wa mikopo ya elimu ya juu kufikishwa katika Kitengo Uratibu za Taarifa za Mikopo (Credit Reference Bureau) kilichopo katika Benki Kuu ya Tanzania (BoT).     Kampuni ya CreditInfo Ltd ina leseni iliyotolewa na Benki Kuu ya Tanzania kwa ajili ya kufanya kazi hiyo.  Hivyo basi, mnufaika wa mikopo ya elimu ya juu ambaye ataomba mkopo kutoka kwenye taasisi yoyote ya kifedha hapa nchini, taasisi hiyo itakuwa na uwezo wa kuhakiki kama mwombaji huyo ni munufaika wa mkopo wa elimu ya juu na ikiwa ana nidhamu ya kurejesha mikopo.  Kwa mujibu wa m

HabariLeo: Mizigo yapungua bandarini Dar tofauti na matarajio

Image
source WAKATI Mamlaka ya Bandari (TPA) ikithibitisha ufanisi katika upakuaji na uondoshaji mizigo na usalama wa mali katika Bandari ya Dar es Salaam, imebainika idadi ya mizigo katika bandari hiyo, imepungua tofauti na matarajio. Akizungumza wakati akifunga warsha ya Wahariri wa Habari mwishoni mwa wiki, Kaimu Meneja wa Bandari ya Dar es Salaam, Hebel Mhanga, alitoa mfano wa shehena ya magari yanayokwenda Jamhuri ya Demokrasia ya Congo (DRC). Kwa mujibu wa Mhanga, shehena ya magari yanayokwenda katika nchi hiyo kutoka Januari 2015 mpaka Januari 2016, imepungua kwa asilimia 50 huku shehena ya Zambia ikipungua kwa asilimia 46. Beira Mhanga alisema walipochunguza sababu ya kupungua kwa shehena hizo, walibaini sehemu ya shehena hiyo hasa iliyokuwa ikienda Zambia, DRC na Malawi, inashushwa katika Bandari ya Beira nchini Msumbiji. Sababu za kushushwa katika Bandari ya Msumbiji, badala ya Bandari ya Dar es Salaam ambayo ndiyo yenye unafuu wa umbali kutokana na jiografia yake, Mhan

"Mshahara wangu haufiki hata nusu ya hizo"- Wakuu wa NHC, EWURA wazungumza na Kamati ya Bunge

3:00 PM MABOSI wa mashirika mawili ya Serikali nchini, wanaodaiwa kulipwa mshahara wa Sh milioni 36, wamekanusha madai hayo, huku wakielezea kushangazwa na taarifa hizo wakati hata nusu ya fedha hizo, hawapati. Akizungumza mbele ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma (PIC), mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), Nehemia Mchechu, halipwi mshahara huo. Akijibu hoja za wajumbe wa kamati hiyo kuhusu taarifa ya utekelezaji na utendaji wa shirika hilo kwa mwaka 2014/15, Mchechu alisema shirika hilo pamoja na kutekeleza majukumu yake, bado lina changamoto za uhaba wa fedha. “Katika ujenzi wa nyumba zetu, Serikali haigharamii masuala ya miundombinu kama vile maji, umeme, barabara hilo ni jukumu letu na linatugharimu fedha nyingi. “Sasa nashangaa wako watu wanasema mimi nalipwa mshahara mkubwa, sielewi wametoa wapi huo mshahara kwa sababu silipwi mshahara huo, mimi nalipwa chini ya huo walioutaja,” alisema

OBAMA:TRUMP HAELEWI SERA ZA KIGENI

Image
Mgombea wa kiti cha urais wa Marekani kwa tiketi ya chama cha Republican Donald Trump, hana ufahamu wowote wa sera za kigeni wala maswala ya ulimwengu! Haya ni kulingana na rais wa Marekani Barrack Obama. Obama ameyasema haya kufuatia matamshi ya Donald Trump kuwa wanajeshi wa Marekani wanafaa kuondoka Japan na Korea Kusini, na mataifa hayo yanafaa kutengeneza zana zao za kinyuklia. Mataifa hayo mawili pia hayakufurahishwa na matamshi ya bwana Trump.

BUNGE KUJADILI HOJA YA KUMN'GOA ZUMA JUMANNE

Image
Bunge kujadili hoja ya kumn'goa Zuma Jumanne Bunge la Afrika kusini litajadili hoja ya kumng'oa rais Jacob Zuma madarakani siku ya Jumanne. Spika wa bunge la Afrika Kusini ametoa taarifa hiyo baada ya shinikizo kutoka kwa vyama vya upinzani vikiongozwa na kile cha Economic Freedom Fighters (EFF) kinachoongozwa na Julius Malema. Spika Baleka Mbete, amesema wakati umewadia wa kujadili wito wa kumfuta kazi rais Zuma kufuatia tuhuma za ufisadi ubadhirifu wa mali ya umma na matumizi mabaya ya madaraka yake. Spika Baleka Mbete, amesema wakati umewadia wa kujadili wito wa kumfuta kazi rais Zuma Vyama vya upinzani vilikuwa vimemtaka ajiuzulu baada ya kupatikana na hatia ya kutumia madaraka yake vibaya kwa kuidhinisha ukarabati wa makazi yake licha ya kushauriwa asifanye hivyo. Siku ya Alhamisi, mahakama kuu ya nchi, ilisema kuwa rais amekwenda kinyume na katiba, katika kashfa ya mamilioni ya dola, yaliyotumiwa kukarabati nyumba yake ya binafsi. Upinzani uliwasilish

MAGAZETI YA JUMATATU, APRIL 4

Image

Taarifa ya habari ChannelTEN, Machi 31

Image
Email This   BlogThis!   Share to Twitter   Share to Facebook  

HESLB YAANZA KUTEKELEZA MIKAKATI YA KUKUSANYA MALIPO YA WADAIWA

Image
Baadhi ya Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Maendeleo ya Jamii wakibadilishana mawazo na Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi Prof. Joyce Ndalichako (katikati) wakati Kamati hiyo ilipotembelea ofisi za Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) jijini Dar es Salaam Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) imesema imeanza kutekeleza mikakati mipya ya ukusanyaji wa mikopo ya elimu ya juu kutoka kwa wadaiwa ambayo itaongeza wastani wa ukusanyaji wa Tshs 2.6 bilioni za sasa hadi kufikia Tshs 8 bilioni ifikapo mwezi Julai mwaka huu. Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa HESLB Bw. Jerry Sabi ameyasema hayo (Jumatano, Machi 30, 2016) jijini Dar es Salaam alipokuwa akiongea mbele ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma za Jamii iliyotembelea ofisi za Bodi hiyo zilizopo Mwenge.  “Hadi mwezi uliopita (Februari, 2016) tulikuwa tunakusanya wastani wa shilingi bilioni 2.6 kwa mwezi, lakini sasa tumeongeza kasi na mikakati mipya ambayo itawez

MAGAZETI YA LEO TZ,APRIL MOSI

Image

WAZIRI WA RWANDA AFIA GEREZANI BURUNDI

Image
Miongoni mwa vurugu zilizotokea mji mkuu wa Bujumbura Waziri wa zamani wa Rwanda Jacques Bihozagara amefariki katika gereza moja nchini Burundi miezi minne baada ya kukamatwa kwa tuhuma za kufanya ujasusi. Rwanda imesema marehemu Jacques alikuwa ameshikiliwa kinyume cha sheria. Balozi wa Rwanda nchini Ubelgiji ameandika na kusema kifo cha Jacques ni "mauaji". Wafungwa katika gereza alipokuwa ameshikiliwa wanasema alionekana akiwa katika hali nzuri na kwamba alifariki dakika chache baada ya kuchukuliwa kutoka gereza kupelekwa hospitali baada ya kuugua. Umoja wa Mataifa umekuwa ukiishutumu Rwanda kwa kujaribu kuipindua serikali ya Rais wa Burundi Pierre Nkurunziza, madai ambayo Rwanda imekuwa ikiyakanusha. BBC