Posts

MRADI WA KUKUZA TEKNOLOJIA KUPITIA WATOTO XPRIZE WAZINDULIWA DODOMA

Image
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi, Profesa Simon Msanjila (kulia) akitoa hotuba ya ufunguzi wa mradi wa kukuza teknolojia kupitia watoto XPRIZE uliofanyika mjini Dodoma mwishoni mwa wiki. Kutoka kushoto ni Mkurugenzi Mwandamizi wa Uendeshaji kutoka Taasisi ya XPRIZE, Matt Keller, Kaimu Mkurugezi wa Elimu ya Msingi wa Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Kassim Kaoneka na Mkuu wa Ofisi na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) nchini, Bi. Zulmira Rodrigues. (Picha na  Modewjiblog ) Kwa kutambua uwezo walionao watoto katika kubuni vitu mbalimbali, Taasisi ya XPRIZE iliyo na makazi yake nchini Marekani, imezindua mradi wa XPRIZE nchini ambao utahusisha watoto ambao hawapo shuleni ukiwa na malengo ya kukuza teknolojia ya dunia kwa kutumia uwezo walionao watoto wa miaka 5-12. Akielezea mradi huo, Mkurugenzi Mwandamizi wa Uendeshaji kutoka Taasisi ya XPRIZE, Matt Kelle

Aliyehoji dawa za MSD kuuzwa duka binafsi abambikiwa kesi ya ujambazi

Image
DAWA za kutibu binadamu zinazomilikiwa na Bohari Kuu ya Dawa (MSD), zimegundulika kuuzwa katika duka moja la mfanyabiashara binafsi lililoko eneo la Mwananyamala kinyume na agizo la Serikali. Hayo yalibainika wiki iliyopita baada ya mwandishi wa habari na mhariri sanifu wa gazeti hili, Dennis Luambano, kwenda katika Duka la Damaco lililoko nje ya Hospitali ya Mwananyamala na kununua dawa zenye nembo ya MSD huku akinyimwa risiti za kodi zinazotambuliwa na Mamlaka ya Mapato (TRA) na kupatiwa iliyoandikwa kwa mkono. Akizungumzia tukio hilo katika chumba cha habari cha gazeti la Mtanzania, Sinza Kijiweni, Luambano alisema dawa hizo zinauzwa kinyemela kwa wauzaji kutowapa risiti wanunuzi na kwamba mmiliki wa duka hilo anatumia nguvu ya fedha kuficha uovu anaoufanya. Luambano alisema baada ya kununua dawa hizo na kuanza kuhoji dawa za Serikali kuuzwa katika duka binafsi, alikamatwa na polisi waliokuwa na mmiliki wa duka hilo aliyemtaja kwa jina la Herman Manyanga na kubambikiwa kesi ya u

[video] Kipande cha Hotuba ya Rais Magufuli kilichowavika tabasamu Wafanyakazi siku yao, Mei Mosi, 2016

Image
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzannia, John Pombe Magufuli leo ametangaza kushushwa kwa kiwango cha kodi ya mapato ya mshahara (Pay As You Earn - PAYE) inayokatwa kwa wafanyakazi wa ngazi ya chini (lower bracket), kutoka asilimia kumi na moja hadi asilimia tisa. TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli ametangaza kuwa serikali yake itapunguza kodi katika mishahara ya wafanyakazi kutoka asilimia 11 hadi kufikia asilimia 9 kuanzia mwaka ujao wa fedha wa 2016/2017 ili kupunguza mzigo kwa wafanyakazi. Rais Magufuli ametangaza uamuzi huo leo tarehe 01 Mei, 2016 wakati akihutubia katika sherehe za maadhimisho ya siku ya siku ya wafanyakazi duniani, zilizofanyika kitaifa katika uwanja wa Jamhuri Mjini Dodoma. "Napenda kuwataarifa kuwa serikali yangu kama nilivyoahidi wakati wa kampeni zangu, nimeamua kupunguza kodi ya mapato ya mishahara kutoka asilimia 11 ya sasa hadi asilimia 9, kuanzia mwaka wa fedha wa 2016/

MAGAZETI YA LEO JUMATATU, MEI 2

Image