Posts

MAGAZETI YA LEO ALHAMISI

Image

TRUMP ASEMA KAMPENI YAKE NI IMARA

Image
Donald Trump amekuwa akishutumiwa kwa kauli zake Mgombea urais wa chama cha Republican nchini Marekani Donald Trump amesisitiza kwamba hakuna mgawanyiko kwenye kambi yake ya kampeni, licha ya taarifa kudokeza kwamba kuna mzozo mkubwa katika chama hicho. Akihutubu katika mkutano wa hadhara Florida, Bw Trump amesema kampeni yake "inafanya vyema sana". Vyombo vya habari vya Marekani viliripoti kuwepo kwa mvutano baada ya Trump kurejea matamshi yake ya kushambulia wazazi wa Mwanajeshi aliyeuawa nchini Iraq. "Ningetaka kuwafahamisha tu kwamba kampeni inaendelea vyema sana," amewaambia watu waliohudhuria mkutano wake eneo la Daytona Beach. Awali, msaidizi mkuu wake Donald Trump Paul Manaford alikuwa pia amekana taarifa kuwa kuna mgawanyiko mkubwa kwenye kampeni baada ya kile kinachodaiwa mfululizo wa kauli za mgombea huyo wa chama cha Republican, zenye kukwaza. ''Kampeni ziko vizuri, tumejipanga, tunasonga mbele,'' aliiambia kituo cha runi

Kurasa za mbele na nyuma za baadhi ya magazeti ya Tanzania leo Agosti 4, 2016

Image

UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA WAANZA AFRIKA KUSINI

Image
Raia wa Afrika Kusini wanapiga kura katika chaguzi za serikali za mitaa ambazo huenda zikawa pigo kwa chama cha ANC ambacho kimeiongoza nchi hiyo tangu kumalizika kwa enzi ya ubaguzi wa rangi miaka 22 iliyopita. Jana saa moja asubuhi Wapiga kura walianza kupanga foleni katika vituo vya kupigia kura kukiwa na hali ya baridi kali. Takriban wapiga kura milioni 26.3 wamesajiliwa kushiriki katika chaguzi hizo. Kulingana na kura za maoni, chama cha ANC kiko katika hatari ya kupoteza viti katika miji muhimu nchini humo ukiwemo mji mkuu Pretoria, mji mkuu wa kibiashara Johannesburg na mji wa pwani wa Port Elizabeth ujulikanao pia kama Nelson Mandela Bay. Maendeleo nchini Afrika Kusini yamekuwa sio ya kasi iliyotarajiwa tangu Hayati Nelson Mandela aliposhinda katika uchaguzi wa kihistoria mwaka 1994 ambapo enzi ya ubaguzi rangi ilikoma nchini humo. Bado raia wengi weusi hawana maakazi mazuri, elimu bora na nafasi za ajira. Je ANC kitastahimili kishindo? Benki kuu nchini humo imes

Vichwa vya Magazeti ya AUG mosi kutoka Tanzania na Nje

Image
TANZANIA KENYA UK

Katuni: Thiwataki kabitha...Dodoma bila shurti

Image

Wizara ya Elimu yapanga kuwa Dodoma kwa awamu kati ya Agosti 15 na Septemba 15

WIZARA ya Elimu, Sayansi na Teknolojia imesema imejipanga kuhakikisha inahamia Dodoma kabla au ifikapo Agosti 15 mwaka huu. Kumekuwa na hekaheka kwa taasisi na wizara mbalimbali za umma kuhamia Dodoma ili kuunga mkono tamko la Rais John Magufuli ambaye Jumamosi ya wiki iliyopita aliuahidi Mkutano Mkuu Maalumu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kuwa Serikali yake itatekeleza ndoto ya siku nyingi ya Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere ya kuhamia katika mji mkuu huo. Jana Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia imekuwa ya tatu kutangaza kuhamia Dodoma baada ya ile ya Kilimo, Uvuvi na Mifugo na Wizara ya Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu. Wizara hizo zinaitikia wito wa Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa ambaye alitangaza kuhamia Dodoma ifikapo Septemba mwaka huu huku akiwataka mawaziri kumfuata. Tangazo lililotolewa na Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia kwa watumishi wake limeeleza kuwa Wizara hiyo itahama kwa awamu mbili. Awamu ya kwanza ambayo i