Haki za watu wa jinsia moja zashinikizwa
Marekani imetangaza hadharani kuwa itapambana na ubaguzi dhidi ya wapenzi wa jinsia moja nchi za nje kwa kutumia msaada kutoka nchi za kigeni na diplomasia kushinikiza mabadiliko. Waziri wa mambo ya nje Hillary Clinton aliwaambia wanadiplomasia Geneva: "Haki za wapenzi wa jinsia moja ni haki za binadamu" Taarifa kutoka utawala wa Obama inayaelekeza mashirika ya serikali ya nchi hiyo kuangazia haki za wapenzi hao wanapofanya uamuzi wa kutoa misaada na uhifadhi wa kisiasa. Sera kama hizo tayari zinatumika kwa usawa wa kijinsia na ghasia za kikabila. "Isiwe jambo la uhalifu kwa mtu kufanya mapenzi ya jinsia moja," Bi Clinton alisema katika umoja wa mataifa Geneva, akiongeza kuwa utamaduni au dini siyo sababu ya kufanya ubaguzi. Wanadiplomasia hao pia ilihusisha wawakilishi kutoka nchi ambazo mapenzi ya jinsia moja ni uhalifu. Mabaloz...