Taasisi mpya ya binafsi inayotoa mikopo kwa wanafunzi wa elimu ya juu imeanzishwa, kwa wale ambao ndugu zao wamekosa mikopo kupitia taasisi ya serikali ya utoaji wa mikopo ya elimu ya juu HESLB wanaweza kuwashauri waombe huko. taasisi hiyo inaitwa HLSSF ( Higher Learning Students Supporting Fund) kwa maelezo zaodi tembelea tovuti hii hapa http://www.hlssf.org/ Taasisi hii inatoa huduma zingine kama ifuatavyo Inatoa mikopo kwa wanafunzi wa elimu ya juu kwa ajili ya kuwasaidia kulipa karo,kununua chakula,kulipia gharama za malazi,kununua vitabu na kufanya utafiti pamoja na mafunzo kwa vitendo. Inawatafutia scholarship za kusoma ndani na nje ya nchi wanafunzi wote ambao wanasifa za ufaulu stahili kadiri ya masharti ya wafadhili. Inawatafutia kazi wahitimu wote wa vyuo vikuu.Hii inafanywa kwa kuwakutanisha wahitimu na waajiri kadiri ya fani zao. Inatoa fursa ya kuwasaidia wahitimu wa vyuo na vijana wengineo wanaotaka kujiajiri katika fani za kiso...
Reince Priebus alionekana na Donald Trump usiku wa siku ya uchaguzi Rais mteule wa Marekani, Donald Trump, amemteua mwenyekiti wa kamati ya taifa ya chama cha Republican, Reince Priebus, kutumika kama mkuu wa wafanyakazi. Bwana Priebus ana uhusiano wa karibu na spika wa baraza la wawakilishi Paul Ryan. Wandishi wa wa habari wanaarifu kwamba uteuzi wa Piebus unaweza kuwaudhi wafuasi wake wa hali ya chini na hii inaashiria kwamba uongozi ujao unalenga kufanya kazi kwa karibu na baraza la Congress kujihakikishia ushindi wa mapema wa baraza hilo. Stephen Bannon aliacha kazi yake ya awali na kuwa kampeni meneja wa Donald Trump Stephen Bannon, alikuwa ni mwenyekiti wa taasisi ya Breitbart News, ambayo ni tovuti yenye maoni ya mrengo wa kulia , naye ameteuliwa kwa nafasi ya mkuu wa mipango na mshauri mwandamizi. Mkuu wa wafanyakazi ambaye anafanya kazi kama mruhusu na mtengeneza ajenda kwa rais, na kwamba ni mmoja wa chaguo muhimu la mapema kwa rais ajae. Katika taarifa yak...
Comments
Post a Comment