WATANZANIA WALIA NA MITANDAO YA SIMU KWA KUPUNGUZA VIWANGO VYA BUNDLE BILA KUTOA TAARIFA KWA WATUMIAJI

Kumekuwa na mabadiliko makubwa ya upunguzaji wa vifurushi vya internet kwa watumiaji wa huduma ya internet mfano kutoka MB 50 mpaka MB 8 kwa kifurushi cha sh. 500 kutoka mtandao wa vodacom, mabadiko haya yanakuja wakati ambao matumizi makubwa kwenye ulimwengu wa sasa yamekuwa kwenye internet na kuna baadhi ya APPs kama whatsapp., Viber, instagram na nyingine nyingi zinatumia internet ili kufanya kazi katika smartphone.

Miaka ya hivi karibuni matumizi ya kupiga na kutuma meseji za kawaida SMS yamepungua na nguvu kubwa kuamishiwa kwenye internet, swali la kujiuliza je kumpatia mteja kifurushi cha sms 500 au 1000 na kumpa MB 8 Je viwango hivi vinaendana?

Mitandao hii ya simu inapaswa kujichunguza sana kabla ya kuamua mabadiliko yoyote lakini pia yawapasa kuwajulisha wateja wao mabadiliko hayo kabla ya kuanza kutumika, mitandao hii ya simu bado imekuwa ikilalamikiwa na wateja kwa kutoa huduma zisizokidhi haja hasa kwenye upande wa internet kuwa slow sana kama mwendo wa konokono.

TCRA mko wapi? tafadhari tazameni swala hili kwa undani zaidi na kutupatia majibu ya kulidhisha wananchi wanaibiwa.

Vifushi vya masaa 24 voda kwenda voda
Tsh 150=10 sms
Tsh 500= dk 15+250sms+8mb
Tsh 650= dk 30+300sms+8mb
Tsh 1000= dk 50+300sms+8mb


vodacom kwenda mitandao mingine
Tsh 150= sms 10
Tsh 499= dk 7+300sms+8mb
Tsh 649= dk13 +450sms+8mb
Tsh 999= dk 20+1000sms+8mb


vifurushi vya wiki voda kwenda voda
Tsh 1050= sms 70
Tsh 2000= dk 60+150sms+60mb
Tsh 2800= dk 85+700sms+60mb
Tsh 4000= dk 140+1750 sms+60mb
Tsh 7000= dk 250+2100sms+60mb
Tsh 10000= dk 360+2500sms+60mb


vodacom mitandao yote kwa wiki
Tsh 1050= sms 70
Tsh 1999= dk 29+500sms+6omb
Tsh 3999= dk 49+500sms+60mb
Tsh 4999= dk 91+1000sms+60mb
Tsh 9999= dk 190+1000sms+60mb


Mabadiliko haya yameikumba pia kampuni ya Tigo ambayo viwango pia vinaendana. 
hizi ni baadhi ya comment za wateja wa vodacom kutoka katika ukurasa wao wa Vodacom uliopo facebook.



Comments

Popular posts from this blog

PATA UKWELI KUHUSU MWANAMALUNDI, MTU WA MAAJABU ALIYEWAHI KUTOKEA KATIKA HISTORIA YA KABILA LA KISUKUMA