Leo imetimia mwaka mmoja tangu mama yetu kipenzi atutoke mnamo tarehe kama yaleo na mwezi kama huu mwaka jana,wanao bado tunakukumbuka sana mama,upumzike kwa Amani.
Zao la pareto ni miongoni mwa mazao ambayo wakulima wamekuwa wakipunguza na kuacha kuyalima kabisa, huenda ni kutokana na bei yake kuwa chini au soko sumbufu. Kamera ya Benjamin Kaminyonge ilipita maeneo ya wilaya ya Makete, kata ya Matamba na kuona zao hilo likiwa kwenye shamba la ekari moja ndani ya kijiji kizima huku kukiwa na mazao kama mahindi, ngano, maharage na alzeti kwa wingi. (picha: benjaminkaminyoge.blogspot.com)
Taasisi mpya ya binafsi inayotoa mikopo kwa wanafunzi wa elimu ya juu imeanzishwa, kwa wale ambao ndugu zao wamekosa mikopo kupitia taasisi ya serikali ya utoaji wa mikopo ya elimu ya juu HESLB wanaweza kuwashauri waombe huko. taasisi hiyo inaitwa HLSSF ( Higher Learning Students Supporting Fund) kwa maelezo zaodi tembelea tovuti hii hapa http://www.hlssf.org/ Taasisi hii inatoa huduma zingine kama ifuatavyo Inatoa mikopo kwa wanafunzi wa elimu ya juu kwa ajili ya kuwasaidia kulipa karo,kununua chakula,kulipia gharama za malazi,kununua vitabu na kufanya utafiti pamoja na mafunzo kwa vitendo. Inawatafutia scholarship za kusoma ndani na nje ya nchi wanafunzi wote ambao wanasifa za ufaulu stahili kadiri ya masharti ya wafadhili. Inawatafutia kazi wahitimu wote wa vyuo vikuu.Hii inafanywa kwa kuwakutanisha wahitimu na waajiri kadiri ya fani zao. Inatoa fursa ya kuwasaidia wahitimu wa vyuo na vijana wengineo wanaotaka kujiajiri katika fani za kiso...
Comments
Post a Comment