Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Mhe. Philipo Mulugo Na Benedict Liwenga-Maelezo, Dodoma. SERIKALI imetenga shilingi Bilioni 326.0 katika mwaka wa masomo 2012/2013 kwa ajili ya kuwakopesha wanafunzi 95,902 wakiwemo wanafunzi wa mwaka wa kwanza, ikilinganishwa na kiasi cha Shilingi Bilioni 56.1 kilichokuwa kimetengwa mwaka wa masomo 2005/2006 kilichomudu kukopesha wanafunzi 42,729. Kauli hiyo imetolewa leo Bungeni mjini Dodoma na Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Mhe. Philipo Mulugo wakati akijibu swali la Mhe. Rashid Ali Abdallah Mbunge Jimbo la Tumbe alilotaka kujua kwanini Serikali imeshindwa kuwapatia mikopo baadhi ya Wanafunzi wenye sifa za kuendelea na masomo na Serikali ina mpango gani wa makusudi kuhakikisha kuwa Wanafunzi hao wanapata elimu. Alisema kuwa ongezeko hilo la fedha ni ishara tosha kuwa Serikali ina nia ya kuhakikisha kuwa wanafunzi wote wenye sifa za kusoma Vyuo vya Elimu ya Juu wanapata mikopo itakayowaw...