MHADHIRI DENIS MPAGAZE: KIGEZO CHA KUTUMWA NA WAZEE KUGOMBEA NAFASI YA UONGOZI NI HOJA DHAIFU
Kuna baadhi ya maandishi ukiyasoma basi kuna kitu lazima kitakugusa, na hii ndio inanisukuma kukichukua alichokiandika mwalimu wangu Mr. Mpagaze aliyenifundisha maswala ya mawasiliano ya umma mwaka wa pili nilipokuwa chuoni St. Augustine (SAUT) Denis Mpagaze Mtu unajijua kabisa uwezo wa kuwa kiongozi hauna. Kwa sababu ya tamaa na njaa zako unaamua kuwaadaa wananchi kwamba wazee wa mji wanakutaka ukagombee. Achana na hoja dhaifu! Kwanza kwa kauli hiyo ya kutumwa na wazee inaonesha jinsi unavyotegemea watu wafikiri kwa niaba yako na wakati kiongozi bora ni yule anayeonesha njia. Unaendeleza utamaduni wa kubebwa bebwa (Godfathers). Yaani ni ishara ya kwamba hata uk ipata madaraka hutakuwa na uwezo wa kufanya maamuzi, badala yake utawaachia wazee kufanya maamuzi kwa niaba yako na kuipoteza jamii. Nasema hivi kwa sababu wazee watakushauri uwe na hofu ya maisha na kuishia kuwaibia wananchi.Kama huamini ninachokisema, angalia mafisadi wakubwa na wahujumu uchumi nchi hii karibu wote ni waze...