LIGI KUU; SIMBA KUANZA NA AFRICAN SPORTS TANGA, YANGA WAKO NA COASTAL TAIFA
Ratiba ya Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL) imetoka leo ambapo jumla ya timu 16 zinashiriki ligi hiyo itakayoanza kutimua vumbi Septemba 12 katika viwanja tofauti nchini na kumalizika Mei 7, 2016. TFF inazisisitiza klabu kukamilisha usajili wao wa wachezaji na viongozi kabla ya kufungwa kwa dirisha hilo la usajili kesho alhamisi Agosti 20, 2015. Baada ya kufungwa kwa usajili huo hakutakua na muda tena wa nyongeza. Kwa klabu ambayo haitawasilisha malipo ya ada ya mchezaji wa kigeni ya dola elfu mbili (U$D 2000) mchezaji huyo hataruhusiwa kucheza kwenye ligi hadi malipo hayo yatakapofanyika. Michezo saba itachezwa siku ya ufunguzi jumamosi katika viwanja tofauti ambapo Ndanda Vs Mgambo Shooting (Nang’wanda - Mtwara), African Sports Vs Simba SC (Mkwakwani - Tanga), Majimaji Vs JKT Ruvu (Majimaji - Songea), Azam FC Vs Tanzania (Azam Complex - Dsm), Stand United Vs Mtibwa Sugar (Kambarage - Shinyanga), Toto Africans Vs Mwadui (CCM Kirumba - Mwanza), na siku ya jumapili Yo...