HISTORIA YA PAPA WEMBA
Habari kuwa mmoja wa vigogo wa muziki wa kiafrika Papa Wemba ametutangulia mbele ya haki imepokewa kwa mshtuko mkubwa na mashabiki wake kote duniani. Video inayosambazwa katika mitandao ya kijamii inamuonesha Papa Wemba akiendelea na kazi yake anayoifahamu zaidi ya uimbaji kisha anaonekana akianguka ghafla jukwaani. Jules Shungu Wembadio Pene Kikumba 1949-2016. Wanabendi wake waliokuwa jukwaani naye huko Abidjan katika tamasha la muziki la #FEMUA wanaendelea kupiga densi tu kabla ya mmoja wao kukimbia kumuokoa baada ya kuona kasalia chini kwa sekunde kadhaa akiwa anatetemeka kisha akazirai. Shoo hiyo ya Papa Wemba ilikuwa moja katika mji mkuu wa Ivory Coast Abidjan. Msemaji wake Henry Christmas Mbuta Vokia, ameiambia Radio Okapi kuwa ''Marehemu Papa Wemba alikuwa ameingia muda mchache tu jukwaani kisha akacheza wimbo wa kwanza, mashabiki wakamuomba awaimbie tena wimbo mwengine akakubali. lakini dakika chache tu baada ya kuanza kupiga wimbo wa ke wa tatu Papa Wem...