Posts

Showing posts from November, 2014

TAARIFA YA PUNGUZO LA 40% YA MATIBABU KWA WATANZANIA

Image
Konseli Mkuu, Bw. Omar Mjenga wa Konseli Kuu ya Dubai kwa niaba ya Serikali ya Tanzania na Mkurugenzi Mkuu wa Hospitali ya Irani iliyopo Dubai (Iranian Hospital Dubai), wakiweka saini makubaliano ya pamoja ambayo yatatoa punguzo la asilimia 40 ya matibabu kwa Mtanzania yeyote yule atakayetibiwa katika hospitali hiyo. Makubaliano hayo yamewekwa saini katika hospitali ya Irani iliyopo Dubai, maeneo ya Jumeirah. Konseli Mkuu Omar Mjenga wa Tanzania, Dubai pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa Hospitali ya Irani, Dubai wakionyesha makubaliano mara baada ya kumaliza kutiliana saini.

POLISI ALIYEMUUA MICHAEL BROWN AJIUZULU

Image
Michael Brown (kushoto); Darren Wilson (kulia) Darren Wilson (28), askari polisi wa kituo cha Ferguson huko St. Louis nchini Marekani ambaye alimpiga risasi iliyomwua kijana wa asili ya Afrika, Michael Brown (18) takriban miezi minne iliyopita, ameacha kazi. Uamuzi huo wa Wilson ulitanganzwa jana Jumamosi na mmoja wa mawakili wake, Neil Bruntrager ambaye amesema hatua hiyo inaanza mara moja. Kabla ya hapo, Wilson alikuwa katika likizo ya kikazi tangu Agosti 9. "I, Darren Wilson, hereby resign my commission as a police officer with the City of Ferguson effective immediately. I have been told that my continued employment may put the residents and police officers of the City of Ferguson at risk, which is a circumstance that I cannot allow. For obvious reasons, I wanted to wait until the grand jury made their decision before I officially made my decision to resign. It was my hope to continue in police work, but the safety of other police officers and the community are of param

MAGAZETI YA LEO JUMAPILI NOVEMBER 30 YAPO HAPA

Image

DIAMOND PLATNUMZ ABEBA TUZO TATU KATI YA NNE ZA CHOAMVA14 HUKO AFRIKA KUSINI

Image
Diamond Platnumz ameiwakilisha vema nchi ya Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla katika tuzo za CHOAMVA 14 zinazoandaliwa na kituo kikubwa cha runinga cha Channel O kilichopo nchini Afrika kusini. Diamond ameweza kuondoka na tuzo tatu usiku huu kati ya nne alizokuwa akiwania, tuzo alizoshinda ni Most gifted East African, Most gifted new comer na Most gifted Afro Pop. Tuzo ambayo ameikosa imenda kwa mwanamuziki Doc Shebeleza inayojulikana kama Most   gifted video of the year. Katika tuzo hizi Diamond ameongozana na mama yake mzazi Bi sandra, pamoja na Management yake akiwepo babu Tale na Mkubwa Fela, lakini kilichokuwa cha kuvutia Zaidi na kutawala mazungumzo mengi katika mitandao ya kijamii ni baada ya kumuona mwana dada zaritheboss kutoka Uganda akiwa ameambatana naye na kupiga baadhi ya picha huku Zari akiwa na mama Diamond kwenye gari la kifahari, watu wamezidi kujiuliza maswali je ndo ile project aliyoisema kwenye vyombo vya habari bado inaendelea? Kwani k

[picha] Wananchi wanavyofuatilia mjadala wa 'escrow' Bungeni

Image
Wakazi wa jiji la Mbeya wakifuatilia michango ya wabunge kuhusu sakata la Escrow mjini Dodoma jana. picha: Christopher Nyenyembe, Mbeya Mbunge wa Hai na Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe akichangia mjadala wa sakata la Escrow mjini Dodoma juzi. Mbunge wa Simanjiro, Christopher Ole Sendeka akichangia mjadala wa sakata la Escrow mjini Dodoma jana. Kangi Alphaxard Lugola, mbunge wa Mwibara, Mara.

AFRIKA YATIMIZA MIAKA MITANO, YABADILI MUONEKANO WA MAX MALIPO

Image
 Mkurugnezi Mtendaji wa Kampuni ya Kitanzania ya  MaxCom Africa, inayotoa huduma za Max Malipo,  Juma Rajabu  na Mwakilishi wa Manispaa ya Kinondoni, Richard Chagula wakikata utepe kuzindua muonekano mpya wa huduma ya Max Malipo, katika hafla iliyokutanisha uongozi wa kampuni hiyo ya Jukwaa la Wahariri, katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.  Mkurugnezi Mtendaji wa MaxCom Africa, watoaji wa huduma za Max Malipo, Juma Rajabu akizindua muonekano mpya wa huduma ya Max Malipo itakavyokuwa sasa kwenye ofisi za mawaakala wake.  Mkurugnezi Mtendaji wa Kampuni ya Max Com Africa, watoaji huduma za Max Malipo, Juma Rajabu akimkabidhi mfano wa hundi ya sh. milioni 10, kwa Mwakilishi wa Manispaa ya Kinondoni, Richard Chagula, kuashiria kampuni hiyo kutoa kiasi hicho cha fedha kwa ajili ya ujenzi wa maabara katika shule zilizomo katika Manispaa hiyo, wakati wa hafla ya kampuni hiyo kutimiza miaka mitano ambapo uongozi ulikutana na wadau wakiwemo Jukwaa la Wahariri katika ho

Baraza la Maaskofu lazungumzia 'mgawo wa escrow' kwa Makasisi wake

Image
Baraza la Maaskofu wa Kanisa Katoliki (TEC) limezungumzia sakata la maaskofu wa kanisa hilo, Methodius Kilaini na Eusebius Nzigirwa kudaiwa kupewa fedha za akaunti ya Tegeta Escrow na kusema kwa sasa hawawezi kuzungumzia suala hilo kutokana na kuwa linagusa watu binafsi. Limesema kuwa suala hilo halihusu baraza na inaweza kufanyiwa kazi kwa taratibu za kanisa kwa kadri uchunguzi unavyoendelea kufanyika, lakini sasa ni mapema mno. Msemaji wa Baraza hilo, Padri Anatoly Salawa alisema kwa sasa suala hilo wazungumzaji ni watu binafsi ambao wanahusika katika sakata hilo na siyo kama baraza. Alisema orodha inawahusu watu wengi na kwamba wakati mwafaka ukifika kanisa litatoa kauli, lakini suala hilo ni binafsi na askofu yeyote ana haki ya kufungua akaunti binafsi kama ilivyo kwa mtu yeyote. Alisema suala hapo linalohusu kanisa ni Benki ya Mkombozi, lakini hata hivyo benki haina mamlaka ya kumuuliza mteja alipopata fedha mpaka watilie shaka na kuto

LOWASSA AKANUSHA KUMILIKI AKAUNTI YA TWITA

Image
Toka bunge limeanza mjadala wa kadhia ya Escrow account,kuna mtu au kikundi kwa sababu wanazozijua wao wenyewe wameanzisha akaunti ya mtandao wa Twitter kwa jina la Edward Ngoyai Lowassa, @edwardlowasa. Kwa kutumia ukurasa huo, mtu huyo amekuwa akiandika masuala kadhaa kuhusiana na suala hilo la escrow account na kile kinachoendelea bungeni, ikionekana kama ni kauli ya Mh Lowassa. Tunawaomba wananchi  kupuuza yote yanayoandikwa katika ukurasa huo.Watanzania tuachane na tabia ya matumizi ya mitandao ya kijamii kupotosha umma,tutumie mitandao hiyo kwa kuhamasisha maendeleo,amani, umoja na mshikamano kwa taifa letu.   Imetolewa na ofisi ya Mh Edward Ngoyai Lowassa(Mbunge)