Posts

Showing posts from June, 2012

BBM PARTY 2012 @Mbalamwezi Beach

Image

WALIOCHAGULIWA KUFANYA USAILI WA POLISI HADHARANI

Na Thomas Dominick Musoma JESHI la Polisi Mkoa wa Mara limetoa majina ya vijana ambao wamechaguliwa kwa ajili ya kufanya usaili wa kujiunga na jeshi hilo ambapo kanda ya ziwa utafanyika Julai 2 hadi 4 mwaka huu katika ofisi ya Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mwanza. Akizungumza na waaandishi wa habari ofisini kwake jana, Kamanda wa Polisi wa Mkoa huo, Absalom Mwakyoma alisema kuwa majina hayo yatabandikwa kwenye mbao za matangazo zilizopo katika ofisi za Mkoa na wilaya zote. “Mwaka huu tumeamua kuchukua vijana watakaojiunga na jeshi letu kutoka mashuleni ambao wamemaliza kidato cha nne mwaka jana na cha sita mwaka huu hivyo tunawaamba vijana wote waende wasome na wajue kama jina lake lipo katika orodha yetu,” “Hii tumerahisisha ili kupunguza msongamano wa vijana kufika katika ofisi zetu na kuulizia ajira hizo na kama unatumia mtandao tafuta katika mtandao wetu wa www.policeforce.go.tz na utaona jina lako na vituo vya usaili,”alisema. Alisema kuwa vijana ambao

TANESCO YATANGAZA NEEMA KWA WATEJA

 SHIRIKA la Umeme Tanzania(Tanesco), limesema ifikapo kesho litakuwa limeshawaunganishia umeme wateja wake wote walioomba kupata huduma hiyo kwa muda mrefu. Hayo yalisemewa jana na meneja uhusiano wa Tanesco, Badra Masoud alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam. Alisema kwa sasa shirika hilo lina vifaa vya kutosha na kwamba ndicho kitu ambacho kilikuwa kikiwakwamisha kutekeleza majukumu yao. “Mteja wetu yeyote ambaye ameomba anapaswa kuwa ameunganishiwa umeme ifikapo Juni 30, mwaka huu,”alisema Badra. Alisema wateja ambao walikuwa wameomba wafike katika ofisi za Tanesco katika maeneo yote zilizopo ofisi zao ili waweze kupatiwa huduma hiyo. “Tutatoa namba maalum ili wateja ambao watakuwa wanasumbuliwa na wafanyakazi wetu waweze kutupigia moja kwa moja na sisi tutashughulika nao,”alisema.

KUWAONA YANGA V EXPRESS J'MOSI TAIFA BUKU TATU TU

Image
WAKATI mabingwa wa ligi kuu soka nchini Uganda,  Express wakiwasili leo tayari kwa mchezo wao wa kimataifa wa kirafiki dhidi ya Yanga, kiingilio cha juu cha mchezo huo utakaoipgwa jumaosi katika uwanja wa Taifa kimepangwa kuwa shilingi 20,000 kwa VIP A. Ofisa habari wa Yanga Louis Sendeu amesema kwamba mashabiki watakaokaa VIP watalipa shilingi, 15,000 kwa VIP B na C ,shilingi 5,000 ni kwa watakaokaa biti vya  kijani na wale watakaokaa viti vya rangi ya bluu na chungwa watalipa shilingi 3,000. source  http://dinaismail.blogspot.com/

VODACOM KUWAZAWADIA MABINGWA WA LIGI KUU BARA J'MOSI

Image
         Simba Sc ndiyo mabingwa wa VPL         AZAM FC (washindi wa pili)            Yanga SC (Washindi wa tatu) John Bocc wa Azam FC (Mfungaji bora wa VPL) Kampuni ya Vodacom itakabidhi zawadi kwa washindi wa Ligi Kuu ya Vodacom msimu 2011/2012 katika hafla itakayofanyika Juni 30 mwaka huu kwenye hoteli ya Double Tree Hilton jijini Dar es Salaam.   Hafla hiyo itakayohudhuriwa na wawakilishi wawili kutoka katika klabu ya Ligi Kuu itaanza saa 12 jioni. Katika hafla hiyo washindi mbalimbali wakiwemo bingwa, makamu bingwa na mshindi wa tatu.   Wengine watakaozawadiwa ni mfungaji bora, kipa bora, timu bora yenye nidhamu, mchezaji bora wa ligi, refa bora na kocha bora.   Chanzo http:// dinaismail.blogspot.com

R. KELLY’S NEW BOOK THAT TALK ABOUT INABILITY TO REMAIN FAITHFUL TO HIS WIFE.

Image
Even though it doesn’t go into detail on all the juicy stuff that ‘s come to be associated with R. Kelly, his new memoir, “Soulacoaster The Diary of Me,” looks to be one very satisfying page turner. Yes, Kelly’s sex life looms large over the book. He is frank about his inability to remain faithful to his girlfriends or wife. And there are brief paragraphs where he discusses the “supposed sex tape,” but they feel legally sanitized. And well-known stories about who leaked the tape and why are never addressed. “Certain episodes could not be included for complicated reasons,” Kelly writes in the author’s note at the beginning of the book

TAMKO LA JUMUIYA YA MADAKTARI KUHUSIANA NA TUME ILIYOUNDWA NA JESHI LA POLISI KUCHUNGUZA TUKIO LA DR. ULIMBOKA

Image
KAMATI YA JUMUIYA YA MADAKTARI TANZANIA                                                                                              YAH: TAMKO FUPI LA JUMUIYA YA MADAKTARI KWA WAANDISHI WA HABARI LEO TAREHE 28.06.2012  Madaktari wote hatuna imani na tume iliyoundwa na Jeshi la polisi nchini yenye lengo la kuendesha uchunguzi juu ya kutekwa, kunyanyaswa na kupigwa vibaya kwa Dr. Ulimboka Stephen na tunataka chombo huru kiundwe ili kupata ukweli wa tukio hilo. Pia tunakemea na kuonya juu ya vitisho vyote vinavyotolewa na baadhi ya watawala katika taasisi mbalimbali dhidi ya madaktari mfano Hospitali ya Rufaa ya Dodoma, Bugando, Mbeya na kwingineko ambapo wametishwa na kufukuzwa kwa kutumia mabavu. Madaktari tunazidi kusisitiza kuwa hakuna njia nyingine yeyote ya kusuluhisha mgogoro huu isipokuwa ni kwa kutekeleza madai na hoja za msingi za madaktari kwa njia ya mazungumzo ya dhati. Madaktari tumechoka kuona hudum

PROFESA MAJI MAREFU ACHAFUA HALI YA HEWA BUNGENI DODOMA

Image
Mbunge wa Jimbo la Korogwe Vijijini, Steven Ngonyani maarufu kwa jina la Profesa Maji Marefu (pichani), leo amesema bungeni kuwa kipigo alichopata Mwenyekiti wa Jumuiya ya Madaktari, Dk. Steven Ulimboka, kinastahili ili naye apate machungu wanayopata wagonjwa wengine mahospitalini. Profesa Maji Marefu aliitoa kauli hiyo wakati akichangia hoja katika bajeti ya Ofisi ya Waziri Mkuu, Bungeni Dodoma. Kauli hiyo ilisababisha tafrani kidogo bungeni, ambapo  Spika wa Bunge, Mhe. Anne Makinda  alilazimika kuingilia kati kumzuia Profesa Maji Marefu asiendelee kutoa kauli hiyo kwani jambo la madaktari bado liko mahakamani.

LISA JENSEN KUWA MGENI RASMI REDD'S MISS MARA 2012

Na Shomari Binda Musoma, Mnyange anayekwenda kuiwakilisha Nchi katika mashindao ya miss world 2012 Nchini China mapema mwezi wa nane na miss Mara mwaka 2006 ambaye ni mshindi wa tatu katika miss Tanzania mwaka 2006 Lisa Jensen amewasili Mkoani Mara kwa ajili ya kushuhudia kinyang'ang'anyiro cha kumpata miss Mara 2012 akiwa kama mgeni rasmi. Akizungumza na Waandishi wa Habari katika uwanja wa ndege Musoma Lisa alisema anawashukuru waandaji wa miss Mara kampuni ya Homeland kwa kumpa heshima ya kuwa mgeni rasmi katika shindano hilo na kueleza kuwa hiyo ni heshima kubwa kwake na ameshukuru kupata heshima hiyo. Alisema hiyo imeoonyesha mashindano ya urembo sio uhuni kama ambavyo bado kuna watu wenye mawazo kuwa urmbo ni uhuni na kudai kuwa hurka ya uhuni na ya mtu mwenyewe na unaweza kufanya mambo mengi ya kujiletea maendeleo kutokana na fani ya urembo. Alidai kuwa kwa upande wake tangu aingie kwenye masuala ya urembo mwaka 2006 amepata faida kubwa

JOSE CHAMELEONE KUTUA BONGO KWA SHOO YA UWANJA WA TAIFA SIKU YA SABASABA

Image
Msanii wa Uganda, Jose Chameleone (pichani juu) leo amekamilisha taratibu zote za kusaini mkataba wa kufanya shoo kali Uwanja wa Taifa mpya, jijini Dar es salaam, siku ya sabasaba baada ya Meneja Mkuu wa Global Publishers, Abdallah Mrisho, kutia timu Entebe mapema leo. Pichani chini ni Chameleone akijigamba kufanya shoo na akisaini mkataba wa mwisho huku akishuhudiwa na meneja wake. Chameleone ametoa onyo kwa Diamond kuwa atamchakaza na Valuvalu!

TASWIRA YA JIJI LA ARUSHA HIVI LEO

Image
. Hili ni godoro kwa mtu huyu ambaye hakujulikana jina lake akiwa amelala katikati ya rundo la taka katika jalala la soko kuu la jijini Arusha kama alivyokutwa na kamera yetu wachuuzi katika soko hilo na wananchi wapitao pembeni ya jalala hilo wameilalamikia kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa kwa kufumbia macho vitendo vya uhalifu vinavyofanywa na vijana wakao na kupekua taka kwenye dampo hilo kila uchwao na kutochukukiwa hatua yeyote . .Mama huyu sawa katandika mfuko kisha akatandaza mchicha wake lakini majimaji aliyonyunyiza kwenye bidhaa yake yamepenya hadi chini kuungana na ardhi ambayo si salama kwa uwekaji chakula hali inayohatarisha afya ya mlaji. Malalamiko ya jiji hilo kuendelea kuwa chafu yamekuwa yakipuuziwa na viongozi wa halmashauri hiyo kwa visingizio vya kuwa bize na ripoti ya mkaguzi wa serekali CAG na kulitelekeza jiji katika hali hii .sehemu ya wafanyabiashara almaarufu machinga wakiwa wamepanga bidhaa zao mbele ya m

FIESTA 2012 HIYOOOOOOOOOOO BHAAASSS!!!!

Image

WAHAMIAJI 42 WAFA DODOMA

Image
WAHAMIAJI haramu 42 raia wa Ethiopia wamekufa katika Kijiji cha Chitego Tarafa ya Zoisa Wilayani Kongwa mkoani Dodoma wakiwa safarini kutoka Ethiopia kwenda Malawi. Kamanda Zelothe Stephen Taarifa za awali kutoka eneo la tukio zinasema kuwa wengine 74 hali zao ni mbaya sana kutokana na kukosa chakula na maji hivyo wanaendelea kupatiwa matibabu. Baadhi ya mashuhuda ambao hawakutaka kutaja majina yao wamesema wahamiaji hao waligunduliwa na wananchi wa kijiji hicho waliokuwa wakienda katika shughuli zao za kilimo jana asubuhi. Taarifa hiyo inadai kuwa wahamiaji hao walikutwa porini wakiwa hoi usiku wa kuamkia leo (jana)baada ya kushushwa katika lori ambalo bodi lake ni la Kontena Taarifa hizo za awali zinasema kuwa wahamiaji hao walikuwa 116 ambao walikuwa wamefungiwa katika kontena hilo na hivyo kukosa hewa kutokana na kulundikana.  Mpaka sasa haijulikani gari hilo lina milikiwa na nani kwani wahamaji walionusulika wengi wapo katika hali mbaya.  Mpaka sasa hak

PLEASE VOTE FOR THIS BLOG

Image
Endelea kupiga kura katika shindano la kutafuta blog bora za kitanzania,ambalo linaendesha na mtandao wa www.tanzanianblogawards.com ,blog hii imewekwa katika category ya best Family/personal blog so kuvote ni rahisi sana tembelea hiyo website na uvote.

VYUO VIKUU 60 AFRIKA MASHARIKI KUSHIRIKI MAONYESHO JIJINI ARUSHA

Na.Ashura Mohamed-Arusha Vyuo vikuu 60 zikiwemo taasisi za elimu ya juu na wadau wa vifaa mbalimbali vya elimu kutoka   nchi za Afrika mashariki   wanatarajia kushiriki katika maonyesho   ya huduma na bidhaa zao yatakayofanyika mwezi ujao mjini Arusha. Mratibu wa maonyesho hayo Peter Oguwi amesema   maonyesho hayo yataka yoanza julai 10 hadi 14 yatafanyika katika viwanja vya nane nane njiro. Pia   nyatashirikisha vyuo kutoka nje ya afrika mashariki ikiwemo India maonyesho ambayo ameyaelezea kuwa ni ya kipekee na mara ya kwanza kufanyika na yanatarajia kuleta watu zaidi ya 500. Oguwi amesema lengo la maonyesho hayo ni kutangaza huduma zinazotolewa na vyuo hivyo zikiwemo program mbalimbali ilikuwafanya wananchi wanchi hizo kuthamini vyuo vyao badala ya kukimbilia nchi za nje hivyo maonyesho hayo yana   tarajia kufanya mapinduzi makubwa katika sekta ya elimu ya juu. Waziri wa elimu na ufundi Shukuru kawambwa anatarajiwa kufungua rasmi maonyesho hayo July 1

WEMA SEPETU AZINDUA FILAMU YAKE YA SUPER STAR

Image
Mwigizaji Wema Sepetu akiingia ukumbini wakati wa uzinduzi wa filamu yake ya Super Star aliyoizindua kwenye hoteli ya Hyyat Kilimanjaro jijini Dar es salaam usiku huu, ikihudhuriwa na watu maarufu pamoja na wanamzuziki na waigizaji, picha zaidi za tukio hili zitawajia baada ya muda Wema Sepetu akipozi kwa picha mara baada ya kukaa kabla ya kuanza kuchezwa kwa Demo ya filamu hiyo usiku huu kwenye hoteli ya Hyyat Kilimanjaro. Wageni waalikwa mbalimbali wakishuhudia uzinduzi wa filamu ya Super Star iliyochezwa na mwana dada Wema Sepetu kwenye hotli ya Hyyat Kilimanjaro Wanamzuiki, watangazaji  pamoja na waigizaji mbalimbali wa filamu walihudhuria katika uzinduzi huo kutoka kulia ni Charles Baba wa Mashujaa Band, Hatman, Mtangazaji Benny Kinyaiya, Mchekeshaji Steve Nyerere, Muigizaj Ramond Kigosi na Richie Mtambalike "Rich Rich" wakishoo Love. Mwanamuziki Mwinyi ambaye ndiye aliyemvisha pete ya Uchuma Wema Sepetu katika filamu hiyo ali

Kampeni ya Kubandika Stika Zenye Namba za Simu za Vituo Mbalimbali za vituo Vya Polisi Yazinduliwa Jijini Dar es Salaam

Image
 Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Posta Tanzania (TPB) Sabasaba Moshingi  akibandika stika hizo.  Mmoja wa Madereva waliokabidhiwa Stika hizo kwaajili ya kuzibandika kwenye magari.  Kamanda Mkuu wa Kikosi Cha Usalama Barabarani akizungumza na Waandishi wa Habari Mara baada ya kuzindua kampeni ya kubandika stika zenye namba za simu za vituo mbalimbali ambazo abiria watazitumia kwaajili ya kutoa taarifa za usalama na matukio ya uvunjifu wa sheria barabarani. Kampeni hiyo inadhaminiwa na benki ya posta (TPB) SOURCE www.freebongo.blogspot.com

SOGGY DOGGY, BW. MISOSI & D KNOB KUFANYA HIP HOP TOUR KANDA YA ZIWA

Image
Soggy Doggy Mambo vipi wadau?Salama?Ni hivi,mwezi ujao wote Soggy Doggy, Bwana Misosi na D.Knob tunafanya Hip-hop tour Kanda ya ziwa,Ruvuma na Arusha lengo kubwa likiwa ni kutoa burudani kwa mashabiki wetu ambao huwa wanatuona mara chache sana kwani tunabanwa na majukumu mengine,katika ziara hizi tunaambatana na madansa wetu na tumedhaminiwa na PRO-24 Bwana Misosi D Knob

Redds' miss Mara 2012 kupatikana june 29

Image
Na Shomari Binda Musoma, Shindano la kumtafuta Redd's miss Mara 2012 litafanyika June 29 huku waandaji wa shindano hilo kampuni ya Homeland Entertainment$Promotion wakidai asilimia kubwa ya maandalizi ya shindano hilo yamekwisha kukamilika na kinachosubiliwa ni kumpata mrembo wa Mkoa huo atakaye shiriki katika shindano la Redd's miss Tanzania 2012. Akizungumza na waandishi wa Habari katika kambi ya mazoezi ya warembo wanaotarajiwa kushiriki katika kinyang'anyiro hicho,mkurugenzi wa kampuni ya Homeland Goldon Mkama alisema anawashukuru wale wote ambao wameshiliiki kwa namna moja ama nyingine kutaka kufanikisha shindano la mwaka huu. Alisema licha ya ugumu wa shughuli za kuandaa shindano hilo la warembo lakini anashukuru mpaka sasa kukamilika kwa asilimia kubwa ya maandalizi yake na kusema kuwa bado kuna nafasi kwa wale wanaohitaji kushiriki kwa namna moja ama nyingine ili kuweza kufanikisha shindano hilo. Mkama alidai kuwa mpaka sas

VITUKO VYA LEO NILIVYOKUTANA NAVYO NDANI YA FACEBOOK

Image

WATU WANNE WASHILIKIWA KUHUSIANA NA UJAMBAZI KATIKA HIFADHI YA TAIFA YA SERENGETI

Na Thomas Dominick, Musoma JESHI la Polisi Mkoa wa Mara linawashikilia na kuwahoji watu wanne wanaodaiwa kushirika katika tukio la ujambazi lililotokea June 20, mwaka huu majira ya saa 3:00 usiku Mivaro Campsite iliyopo katika Hifadi ya Taifa ya Serengeti. Taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari Mkoa hapa, Kamanda wa Polisi wa Mkoa huo, Absalom Mwakyoma alisema kuwa watuhumiwa hao walipatikana baada ya jeshi hlo kuendesha oparasheni kabambe ambayo ilifanikiwa kuwakamata watu hao. Kwa mujibu wa taarifa hiyo ilisema kuwa majambazi wapatao nane walivamia kambi hiyo ya watalii wakiwa bunduki na mapanga, na walipofika karibu na sehemu ya kulia chakula walikutana na Meneja Msaidizi Renatus Robert (42) ambapo walimfyatulia risasi kifuani na kuanguka chini akafariki Dunia. Baada ya hapo walikwenda kwenye hema namba 12 ambako walikuwepo Mholanzi Erick Paul (58) na kumtaka atoe fedha Uero au dola ambapo aliwaambia watoke ndipo walipompiga risasi ya paja na kumjeruhi kw

Ensuring Fair Trial in Cases of Children in Conflict with the Laws: The Tanzanian Paradox

Image
      BY Lucky Michael Mgimba ,A Student of   St. Augustine University of Tanzania Abstract The Issue of managing or dealing with children coming into conflict with the law has historically haunted nations and Tanzania is no exception. Although there have already been important headways, much remains to be done in ensuring a child friendly justice system in Tanzania. The problem has for ages risen when children come in contact with a justice system that is unresponsive to their needs, which not only deprives them of their liberty, but also accentuates or increases their vulnerability to abuse, violence, exploitation and health related risks such as injury and HIV infection. This work comes in place to analyze the legal and institutional framework under the International, regional and national (Tanzanian) levels; with a view of determining as to how much consistent are they with the accepted legal standards.