Posts

Showing posts from December, 2015

Rais mstaafu Kikwete, Waziri Lwenge wakagua mitambo ya maji Wami, Chalinze

Image
Rais mstaafu wa Awamu ya Nne, Jakaya Kikwete (katikati), akizungumza na Waziri wa Maji, Gerson Lwenge wakielekea kukagua mitambo ya kusafisha na kusafirisha maji Wami, katika Halmashauri ya Mji wa Chalinze, mkoani Pwani, Desemba 30, 2015. Rais Jakaya Kikwete na Lwenge wakiangalia mitambo ya kusafisha maji Wakiwa katika picha ya pamoja Rais mstaafu wa Awamu ya Nne, Jakaya Kikwete , akizungumza na Waziri wa Maji, Gerson Lwenge (kushoto kwake) wakielekea kukagua mitambo ya kusafisha na kusafirisha maji Wami, katika Halmashauri ya Mji wa Chalinze, mkoani Pwani leo.Wa pili kulia ni Mbunge wa Jimbo la Chalinze, Ridhiwani Kikwete. Rais mstaafu wa Awamu ya Nne, Jakaya Kikwete akionesha kitu walipotembelea mitambo ya maji Wami Mbunge wa Jimbo la Chalinze, Ridhiwani Kikwete akizungumza na Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Gerson Lwenge katika mitambo hiyo

WATAKAOFANYA FUJO MKESHA WA MWAKA MPYA KUKIONA

Image
Na Jacquiline Mrisho MAELEZO Jeshi la Polisi Kanda maalum ya Dar es salaam limewatahadharisha wananchi kutokufanya fujo wakati wa mkesha wa mwaka mpya kwa kuweka mikakati mikali kwa watakaokaidi amri hiyo. Akizungumza na Waandishi wa Habari leo Jijini Dar es salaam Kamishna wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam Suleiman Kova amepiga marufuku uchomaji wa matairi ya gari, upigaji baruti, risasi za moto na fataki ambazo zaweza kusababisha madhara wakati wa mkesha wa mwaka mpya. “ Ni baraka zaidi kusherekea sherehe kama hizi kifamilia na sio vizuri kuingia mwaka mpya ukiwa mahabusu, huo ni mkosi” Alisema Kamishna Kova. Kamishna Suleiman Kova aliongeza kuwa watashirikiana na wadau mbalimbali ikiwa ni pamoja na Jeshi la Zimamoto, kampuni binafsi za ulinzi, vikundi vya ulinzi shirikishi pamoja na kutumia ndege za Polisi kufanya doria ili kuhakikisha kuwa wanailinda amani na kudhibiti aina yoyote ya uhalifu utakaojitokeza. Aidha Kamishna Kova amesisitiza kuwa vituo vyote vya p

MBWANA SAMATTA APONGEZWA KWA KUJIUNGA NA KLABU YA GENK YA UBELGIJI

Image
Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Nape Nnauye(kushoto) akiongea na Mchezaji wa Timu ya TP Mazembe Mbwana Samatta(kulia) leo jijini Dar es salaam.Mbwana amemtembelea waziri Nape ofisini kwake na kuomba baraka za wizara katika kinyanganyiro cha kugombea uchezaji bora wa afrika anayechezea ligi za ndani na pia kumpa habari njema za yeye kutegemea kujiunga na timu ya Ubelgiji ya Genk.  M chezaji wa TP Mazembe Mbwana Samatta(wa kwanza kushoto)akiongea na waandishi wa habari(hawapo pichani) sababu za yeye kumtembelea Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo katika ofisi ya Wizara hiyo.Mbwana alisema kuwa amemtembelea waziri uyo kwa ajili ya kumfahamisha kuwa yumo katika kinyanganyiro cha kugombea uchezaji bora wa afrika anayechezea ligi za ndani na hivyo kuomba baraka za Wizara.Pia kumpongeza Mhe. Nape kwa kuchaguliwa kuwa waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo.Mbwana anategemea kujiunga na klabu ya Mpira ya Genk ya Ubelgiji kwa mkataba wa miaka minne.  Waz

Polisi 6 wapandishwa kizimbani Dar kwa tuhuma za kuua wafanyabiashara Sinza

ASKARI sita waliokuwa wanashikiliwa na Jeshi la Polisi kwa kuhusishwa na mauaji ya wafanyabiashara, jana wamefikishwa mahakamani kwa tuhuma za mauaji ya kukusudia. Washtakiwa hao walifikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu mbele ya Hakimu Mkazi, Thomas Simba. Mbele ya Hakimu Simba, Wakili wa Serikali Mkuu, Mutalemwa Kisheni, aliwataja washtakiwa kuwa ni Inspekta Bon Mbange mkazi wa Magomeni, F 919 Sajenti Filbert Nemes na Askari wa Kikosi cha Kuzuia Ujangili, Asubile Mwakyusa, Deogratius Mwageni na Joseph Jimmy. Kisheni alidai washtakiwa kwa pamoja wanadaiwa Desemba 19, mwaka huu maeneo ya Sinza, Wilaya ya Kinondoni, Dar es Salaam, waliwaua Yasin Rashid na Samson Msigale. Washtakiwa hawakutakiwa kujibu lolote kwa sababu mahakama hiyo haina mamlaka ya kusikiliza kesi za mauaji. Awali Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Kamishna Suleiman Kova, alieleza kukamatwa kwa washtakiwa hao wakihusishwa na utata wa mauaji ya wafanyabiashara hao. Kamanda Kova alidai taari

MAGAZETI YA LEO ALHAMISI, DECEMBER 31

Image

NEMC yakataza hoteli kutoza fedha wananchi wanaobarizi 'beach'

BARAZA la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC), limewataka wawekezaji wa hoteli zilizopo pembezoni mwa bahari kuacha kuwatoza wananchi fedha za kiingilio wanapokwenda katika fukwe hizo kupunga upepo au kuogelea. Tamko hilo limekuja kutokana na baadhi ya hoteli katika Jiji la Dar es Salaam kubainika kutoza fedha kuanzia Sh 10,000 hadi 40,000 kwa mtu mmoja kama gharama za kuogelea. Uchunguzi uliofanywa na MTANZANIA umebaini kuwa wamiliki wa hoteli hizo wamekuwa wakifanya hivyo katika sikukuu mbalimbali na zile za mwisho wa mwaka, jambo ambalo limekuwa likileta kero kwa jamii. Akizungumzia suala hilo Mwanasheria wa NEMC, Manchari Heche, alisema kwa mujibu wa sheria, fukwe zote ni mali ya umma, hivyo wananchi hawatakiwi kutozwa fedha wakati wanapokwenda kutembea au kuogelea. “Kifungu cha 57 cha sheria ya mazingira kimeweka ukomo wa mpaka wa kila kiwanja kilichopo karibu na ufukwe. “Beach (fukwe) zote ni mali ya umma kwa sababu kuna mipaka yake, hivyo kitendo cha kuwatoza w

KATUNI YA LEO.

Image

Kampuni za simu zatozwa faini; Wavietnam wa Halotel wakamatwa

Image
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, (Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Watu wenye ulemavu), Bibi. Jenista Mhagama (Mb), akifuatilia maelezo ya wajumbe wa kikosi Maalum cha kukagua vibali vya Ajira za Wageni (hawapo pichani) wakati alipokutana nao Jijini Dar es Salaam tarehe 29 Desemba, 2015, (katikati) ni Naibu Waziri (Kazi, Ajira na Vijana), Anthony Mavunde na Katibu Mkuu (kazi na Ajira), Eric Shitindi. NAIBU Waziri wa Ofisi ya Waziri Mkuu, anayeshughulikia Kazi, Ajira na Vijana, Anthony Mavunde amebaini kuwepo kwa wafanyakazi wa kigeni, walioletwa na kampuni za simu za mkononi kufanya kazi zinazoweza kufanywa na Watanzania ikiwemo kufunga meza na viti vya kukalia. Aidha, amebaini kuwepo kwa baadhi ya wafanyakazi wa Kampuni ya simu ya Halotel, raia wa Vietnam, ambao wanaishi nchini bila kibali cha kazi wala cha kuishi. Mavunde aliyabaini hayo jana wakati alipofanya ziara ya kukagua vibali vya ajira kwa wageni, baada ya tangazo lililotolewa na Waziri wa Ofisi ya Waziri Mk

Prof. Ndalichako ataja atakakoanzia ili kufufua kiwango cha elimu

Image
Prof. Ndalichako (wa kwanza kushoto, nyuma ya Katibu Mkuu Kiongozi) katika picha ya pamoja na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzani Dkt. John Pombe Magufuli, Makamu wa Rais, Waziri Mkuu, Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Katibu Mkuu Wa Kiongozi (walioketi) na Mawaziri (wote waliosimama) baada ya kuwapisha Ikulu jijini Dar es salaam Desemba 28, 2015.  WAZIRI wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi, Prof. Joyce Ndalichako, amesema atafuatilia shule za Serikali ili kujua sababu za kufanya vibaya katika mitihani yao. Prof. Ndalichako ambaye aliwahi kuwa Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani (NECTA), amesema hayo juzi baada ya kuapishwa na Rais John Magufuli, kushika wadhifa huo. “Kwa kuwa lengo langu ni kuona elimu bora inatolewa, nitafuatilia kujua sababu ya shule maalumu za Serikali kushuka kiwango chake katika ufaulu wa mitihani,”  Kwa mujibu wa Prof. Ndalichako, shule hizo za Serikali hasa za vipaji maalum, ndizo awali kila mwanafunzi alipenda kwenda kusoma tofau

UFISADI MWINGINE WAIBULIWA BANDARINI DAR

Image
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa Serikali imepoteza jumla ya Sh. bilioni 48.47 baada ya makontena 11,884 na magari 2,019 kupitishwa badarini Dar es Salaam bila kulipiwa kodi. Hata hivyo, jumla ya watu saba wanashikiliwa na wengine nane wanatafutwa na Jeshi la Polisi kwa kuhusishwa na ukwepaji kodi huo uliolikosesha taifa mapato. Akizungumza na wanahabari leo jijini Dar es Salaam, Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa amesema ufisadi huo umebainika baada ya serikali kuzifanyia ukaguzi bandari zote za nchi kavu (ICDs) jijini Dar es Salaam. Akifafanua, Waziri Mbarawa amesema makontena hayo 11,884 yalikuwa na thamani ya Sh. bilioni 47.4 wakati magari gari 2019 zenye thamani ya Sh. bilioni 1.07 yalitolewa bandarini pasipo kulipiwa tozo.

MAGAZETI YA LEO JUMATANO, DECEMBER 30

Image