Posts

Showing posts from January, 2011

MSANII PABLO AMEFARIKI LEO

Image
Pablo kwa ambae hamfahamu alichana katika wimbo wa daz baba, nipe tano, ukiitizama utamsikia akijitaja jina lake, kavaa t shirt ya mistari.pole kwa wale woote wanaharakati wa mziki wetu kwasababu tumempoteza mmoja wa wanaharakati. mungu ailaze roho ya marehemu mahala pema peponi . RIP

Msiotahiriwa Kagera Jiandaeni'

Midume ya kisiwa cha Goziba wilayani Muleba mkoani Kagera ambayo haijatahiriwa imetakiwa kujiandaa kushiriki uzinduzi wa tohara kwa wanaume Januari hapo 22 heheeeee. Taarifa iliyotolewa jana na Ubalozi wa Marekani nchini, ilisema uzinduzi huo ni wa aina yake na utafanywa katika maeneo ya vijijini na watu wanaotarajiwa kuhudumiwa ni zaidi ya 3,500 katika miezi kadhaa ijayo. Tohara hiyo na huduma mbalimbali zinazohusu virusi vya Ukimwi zitatolewa bure visiwani humo ambako mahema yatasimikwa kutoka Serikali ya Marekani. Kampeni hiyo inakwenda pamoja na kanuni za msingi, kwamba tohara kwa wanaume ni sehemu ya kinga dhidi ya maambukizi ya Ukimwi na ilishathibitishwa katika maeneo ambako kuna maambukizi makubwa ya ugonjwa huo na idadi ya waliotahiriwa iko chini. Visiwa hivyo vilivyoko ndani ya Ziwa Victoria, vinatambulika kwa kuwa na kiwango cha juu cha vitendo vya ngono kutokana na asili ya biashara ifanyikayo hapo ya uvuvi wa samaki ambayo inamlazimu mvuvi kusafiri huku

FURAHI DAY.................

Image
NAWATAKIA WEEKEND NJEMA WAPENZI WOTE WA BLOG HII

NGOMA TIME

Image
SIKILIZA SAUT FM 96.1 FM LIVE FROM ST.AUGUSTINE UNIVERSITY OF TANZANIA KIPINDI CHA NGOMA TIME SAA 8:00 MCHANA MPAKA 10:00 JIONI DON'T MISS THE SHOW

MAPANKI BADO YAPO?

Image
Kuna baadhi ya sehemu bado mapanki yanaendelea kutumika kama kitowewo ,nilipita maeneo ya mazami nikaona mapanki yakiuzwa...........minofu iende ulaya watanzania waendelee kula mapanki stuka....chukua hatua

MBUNGE WA JIMBO LA MUSOMA MJINI ATEMBELEA WAGONJWA NA KUTOA VITABU KWA SHULE ZA MSINGI NA SEKONDARY KATIKA JIMBO HILO

Image
Mbunge wa jimbo la Musoma mjini Vincent Nyerere ametembelea wagonjwa katika Hospital ya Mkoa wa Mara ambapo baadhi yao walitekwa na kukatwa mapanga juzi. Mheshimiwa Nyerere akimjulia hali mgonjwa katika hospital ya mkoa wa Mara ambaye ni mmoja ya wahanga ambao walitekwa na majambazi kisha kunyang'anywa fedha na mali zao Mheshimiwa Nyerere akimjulia hali mgonjwa katika hospital ya mkoa wa Mara leo,mzee huyu ana umri wa miaka 67 lakini cha ajabu ameshindwa kupata huduma stahiki kwa kile kinachosemekana hana fedha lakini wadau sera ya wazee inasemeaje? kilio chake kimefika kwa mheshimiwa Nyerere Mheshimiwa Nyerere akimjulia hali mgonjwa katika hospital ya mkoa wa Mara leo,huyu aliwahi kuwa katibu wa mbunge wa jimbo la Musoma vijijini na katika maelezo yake anasema kuwa majambazi waliomvamia kwake walikuwa zaidi ya nane na walipofanikiwa kuingia walimkata panga kama uonavyo picha hiyo na kisha kuchukua redio na fedha kiasi cha laki nane lakini baadaye redio zilipatika

NGOMA TIME

Image
Usikose kusikiliza kipindi cha NGOMA TIME kuanzia saa 8:00 mpaka saa 10:00 jioni radio SAUT FM,96.1 nitakuwepo na wana DIDAS,NYANDA,MAZIKU,MLEI Tukisababisa kwenye MC.DONT MISS THE SHOW

New video of AY ft. Ms. Triniti - Good Look

Joti - Jibwa Koko

MBAGALA (REMIX)....KAFARA - TANZANIGHT

Ali Kiba Feat Chidi Benz - Far Away

KONGAMANO LA KATIBA

Image
JUMUIYA YA WANATAALUMA CHUO KIKUU CHA DAR ES SALAAM (UDASA) inawaletea: KONGAMANO LA KATIBA MADA KUU: MCHAKATO NA MAUDHUI YA KATIBA MPYA WAZUNGUMZAJI WAKUU: Prof. ISSA SHIVJI Ndg. JENERALI ULIMWENGU TAREHE: Jumamosi, 15 Januari 2011 UKUMBI: Nkrumah, Chuo Kikuu cha Dar Es Salaam MUDA: SAA 4:00 AsubuhiI hadi SAA 8:00 Mchana NYOTE MNAKARIBISHWA

OOH DO U LOVE ME!

Image
Thanks............

DOGO JANJA ASEMA YEYE NI MUZIKI NA SHULE

Image
MSANII mdogo kuliko wote wanaotamba kwa sasa hapa nchini Abduaziz Chende maarufu kama Dogo Janja amesema pamoja na umaarufu alioanza kuupata kamwe hawezi kulipa kisogo suala la elimu. Mwanahip hop huyo mwenye miaka 14 amesema kuwa anaamini eklimu ndiyo ufunguo wa maisha hivyo kutokana na umri wake kuwa mdogo hawezi kupoteza haki yake hiyo ya msingi sababu ya muziki. Kwa sasa msanii huyo aliyekuwa akiishi jijini Arusha yupo jijini Dar es Salaam na tayari ameshaanza kidato cha kwanza katika sekondari ya Makongo, huku akiendelea na muziki. Yatari msanii huyo ambaye anafanya kazi chini ya kundi la Tip Top Connection lenye maskani yake Manzese, Dar es Salaam amekamilisha yake ya pili iitayo I Get Money akimshirikisha Godzillah. Awali alitoka na wimbo unaoitwa "Anajua" aliowashirikisha Madee na Tundaman

HALMASHAURI YA JIJI LA MWANZA YAUNDA KIKOSI KAZI KUDHIBITI WEZI WA MIUNDOMBINU YA TAA ZA BARABARANI.

Image
Kutokana na kuwepo hujuma na wizi wa miundombinu ya taa za barabarani halmashauri ya jiji la mwanza kwa kushirikiana na Kikosi cha Polisi imechukuwa hatua ya kuunda kikosi kazi kwania ya kukamata wahalifu ili hatua za kisheria zipate kuchukuliwa dhidi yao. WILSON KABWE. Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake mwishoni mwa wiki, Mkurugenzi wa jiji la Mwanza bw. Wilson Kabwe amesema kuwa kufuatia wizi mkubwa uliofanyika kwa nyaya hizo umepelekea maeneo mengi ya barabara kuwa na giza nene hali iliyosababisha kuripotiwa kwa matukio mengi ya wananchi kuvamiwa na wezi, kuumizwa na hata kuporwa mali zao. habari hii ni kutoka www.gsengo.blogspot.com

A NEW COMPANY FOR IMPORTING AND EPORTING GOODS IN UK

Image
Welcome to Locus Impex-UK We are an import/export company currently based in the United Kingdom with global dealings. Unlike our competitors we like to develop a personal relationship with our clients and try to offer a specific service to suit each individual client. Whether you require a single service or an annual requirement Locus Impex will treat you with care, consideration and most of all the best solution for your requirements. We pride ourselves in our service and welcome any job regardless of size. We can ship to various global locations and our main expertise is importing and exporting between the United Kingdom , Tanzania , DR Congo , Kenya , Cameroon and many more.`` For more information contact Marketing Director Mr.Bernard Chisumo the contact is below Bernard Chisumo Market Director Reading Branch Locus International Ltd 14 Rothwell Walk,Caversham Reading,RG4 5DB Tel: +44 118 954 5890 ,07876126862 Email: bchisumo74@yahoo.com , reading@locusimpex.com OR Main H

KUMBUKUMBU YA KIFO CHA MZEE A. MUTARAGARA CHIRANGI

Image
MAREHEMU MZEE A. MUTARAGARA CHIRANGI Pamoja na Mwanafalsafa Friesrich Nietzsche (1844 - 1900) kuona na kusema kweli kwamba, kuwa na subira au uvumilivu ni ngumu sana, hata kwa Washairi Wazamivu kushindwa kuzuia hasira zao kutoa dhamira ya ushairi wao au kwamba shauku haitasubiri!, Tulimsikia na kumwona baba Mzee Mutaragara Chirangi (RIP), akionyesha uvumilivu katika anga za Siasa kwa hali isiyotegemewa. Ni siku nyingine tena leo, ikiwa imetimia takribani miaka minne tangu atutoke duniani, tunaendelea kupata kumbukizi la changamoto toka maisha ya huyu mzee wetu. Katika anga za ki- Siasa hususan baada ya chaguzi, uwezo wa Binadamu wengi kuweza kuvumilia au kunyenyekea au kuonyesha subira au kujizuia kusema au kufanya jambo ambalo halina tija wala maendeleo ya mwanadamu kwa leo na kesho, ni mdogo sana. Dhamira ya uvumilivu aliyoitangaza mzee Chirangi kwa vitendo, kamwe haikumaanisha kushindwa kudai haki