KOREA KASKAZINI NA BOMU NA HYDROGEN
Tangazo kuhusiana na jaribio hilo la bomu la Hydrogen la Korea Kaskazini Siku moja baada ya Korea Kaskazini kufanya jaribio la bomu la nyuklia aina ya Hydrogen, Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limekubaliana kuanza mikakati ya kuiwekea vikwazo kufuatia jaribio hilo. Hata hivyo baadhi ya Wataalam wameonyesha kuwa na wasi wasi kuhusu jaribio la sasa la Nyuklia la Korea Kaskazini ambalo ni la nne katika muongo mmoja kwamba nguvu yake inaweza kuwa ni bomu la hydrogen. Kwa faida yako tu bomu la hydrogen ni moja ya mabomu hatari ya jamii atomic au nyuklia yenye nguvu zaidi. Wataalam wanasema bomu hili la hydrogen lina uwezo mkubwa kiasi kwamba linaweza kulipua mji mmoja wote kwa mlipuko mmoja. Kufuatia jaribio hilo jamii ya kimataifa imendelea kulaani tukio hilo Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa ambaye pia ni Waziri wa zamani wa Mambo ya nje ya Korea Kusini Ban Ki moon yeye amesema jaribio hilo la bomu la nyuklia ni hatua ya kuogopesha. "Hili jaribio kwa mara nyingin...