Posts

Showing posts from May, 2012

Will Smith: Nina bahati Jada kuwa mke wangu

Image
Will Smith amemsifia mke wake Jada Pinkett kwa kuifanya familia yake kuwa pamoja. Muigizaji huyo wa Men In Black III na mke wake muigizaji wa series ya Hawthorne wana miaka 17 tangu waoane licha ya hivi karibuni kuwepo na fununu kuwa ndoa yao ipo matatani kuvunjika. “Nina bahati sana kuwa na mtu kama Jada. Ni mwanamke wa pekee, mke na mama… ni mgumu kwakweli, yaani ni kama vile huwa hashtushwi na uzito na pressure za maisha, “ Will ameliambia jarida la People. “Ni mtulivu sana na huchukulia rahisi kila hali. Anaweza kuvumilia lolote na napenda sana hilo kutoka kwake. Huwa tunaweka jitihada za kuitanguliza familia kwanza. Kuwepo kwa ajili yetu sote na kuwa karibu na watoto wetu ni jambo muhimu. Nachukulia serious sana suala la kuwa mzazi.”

Liberia's ex-President Charles Taylor has been sentenced to 50 years in jail

Liberia's ex-President Charles Taylor has been sentenced to 50 years in jail by a UN-backed war crimes court. Last month Taylor was found guilty of aiding and abetting rebels in Sierra Leone during the 1991-2002 civil war. Special Court for Sierra Leone judges said the sentence reflected his status as head of state at the time and his betrayal of public trust. Taylor, 64, insists he is innocent and is likely to appeal against the sentence, correspondents say. The appeal process could last up to six months, the BBC's Anna Holligan in The Hague reports. 'Savage crimes' During the sentencing, Judge Richard Lussick said the crimes in Sierra Leone were some of the most heinous in human history. The prosecution had wanted an 80-year prison term, but the judge said that would have been excessive - taking into account the limited scope of his involvement in planning operations in Sierra Leone.  

WAANDISHI WA HABARI MWANZA WATEMBELEA SAHARA MEDIA GROUP LEO

Image
Mkurugenzi wa Sahara Media Group bw. Anthony Dialo akiongea na waandishi wa (habari wataonekana katika picha nyingine) ambapo amesema kuwa kuanzia mwezi Septemba 2012 minara na mitambo ya king'amuzi kipya itawashwa rasmi kwaajili ya kuanza kufanya kazi. Star Tv pamoja na televisheni zote za IPP zitaingia katika mfumo wa digitali kupitia king'amuzi hicho. Serikali kupitia Tume ya Mawasiliano nchini imesema kuwa ifikapo Disemba 31 mwaka 2012 ndiyo itakuwa mwisho kwa vituo vyote vya televisheni kurusha mawasiliano yake katika mfumo wa analogy na kujiunga na mfumo wa digitali, hivyo basi kwa msingi huo kampuni ya Sahara Media Group na wadau shirika wako kwenye mchakato kuharakisha zoezi la kusimika minara na mitambo kwaajili ya kuingia kwenye masafa bora ya kisasa. Wadau wa habari kutoka vyombo mbalimbali waliopata mwaliko kutembelea Sahara Media Group na harakati za usimikaji mitambo mipya. Ujenzi unaendelea katika eneo la juu ghorofa lenye

MISS NYAMAGANA WATEMBELEA FURNITURE HOUSE

Image
 Mwanadada Joyce Rewben wa Furniture House akiwaonyesha warembo wa miss Nyamagana bidhaa zinazouzwa ndani ya duka hilo lililopo ghorofa ya kwanza ndani ya Jengo la CCM mkoa wa Mwanza.  Moja kati ya engo za furniture ndani ya duka hilo.  Furniture House ambao ni moja kati ya wadhamini kinyang'anyiro cha miss Nyamagana 2012 kitakachofanyika ijumaa hii ndani ya Gold Crest Mwanza, pamoja na zawadi kutoka kwa wadhamini wengine, Furniture House itatoa zawadi ya sofa hili lenye thamani ya shilingi Milioni mbili na laki mbili kwa mrembo atakaye valishwa taji la Miss Nyamagana.  Sofa at Furniture House.  Warembo wakiwa wamesimama pamoja na wadau wa Furniture House ambao ni moja kati ya wadhamini wa Miss Nyamagana 2012. Walioketi ni Joyce Reuben (L) na Timilo Mohamed (R). Mtangazaji wa Star Tv Abdalah Tilata (L) akiwa na Cameraman Baraka Samson wakiperuzi kwaliti' za view walizochukuwa eneo la tukio.  Didi-daaaah..!  D

UFUNGUZI WA SAUT BUSINESS INCUBATION CENTRE

Image
  Kesho tarehe 31/05/2012 kuanzia saa 8:00 Mchana- 11:30 katika ukumbi wa M12 katika chuo kikuu cha Mt.Augustino kutakuwa na uzinduzi rasmi wa kituo cha ujasiliamali kitakachojulikana kwa jina la BUSINESS INCUBATION CENTRE (B.I.C). Centre hii ni mahususi kabisa katika kutoa elimu ya ujasiliamali kwa wanafunzi wote wa SAUT ambao watakuwa mwaka wa mwisho wa masomo yaani mwaka wa 3 na 4,baada ya kumaliza mitihani yao ya mwisho wa semister watapata fursa ya kuweza kupata mavunzo ya ujasiliamali kwa muda wa miezi 3 BURE kabisa,ambapo chuo kimejitolea kutoa majengo yake,kuleta walimu kutoka sehemu tofauti tofauti hapa nchini na nje ya nchi. Dhumuni la kuanzisha Centre hii ni kuweza kuwasaidia hususan wanafunzi wa SAUT na jamii kwa ujumla njia tofauti tofauti za kuweza kupata fursa za kujiajiri wao wenyewe kwa kuanzisha makampuni yao na pia kuweza kuwapatia mwanga juu ya jinsi gani wanaweza kutumia malighafi zilizopo nchini na kuweza kumiliki njia kuu za uchumi kwa maendeleo ya ja

HII NDIO ILE TWITTER BEEF YA CHRIS BROWN, DRAKE & MEEKMILL KUHUSU RIHANNA.

Image
. Radio Power 105 New York imeripoti kwamba Kuna baadhi ya beef kwenye twitter ambazo huwa ni raha kuzisoma na zinafurahisha, ila hii ya wasanii iliyoibuka ya Chris Brown, Meek Mill na Drake inakera. Kilichotokea ni kwamba inaonekana wasanii hao wote watatu wa kiume wanamgombania Rihanna.. na hicho kimeonekana kupitia walichikiandika kwenye page zao za twitter @Chrisbrown – aliandika, huyu dem anafata ndoto zake, na atazifuata milele @Meek Mill – akaandika hawa wanawake hawamilikiwi na mtu yeyote, wote wako kwenye game au sanaa, usichanganye ukajiona kwamba unawamiliki wewe, au kwamba wanakutizama wewe tu. @Drake – Ohhh… kwa hiyo ni kicheche wako? Pia sisi ni kicheche wetu. Mwishoni Rihanna akamaliza kwa kutweet mara mbili akisema… Inafurahisha sana, ila cha muhimu lile jicho ndilo litakalochagua lenyewe. . . . . . .

TANZANIA YAUNGANA NA NCHI NYINGINEZO DUNIANI KUADHIMISHA SIKU YA KIMATAIFA YA WALINDA AMANI WA UMOJA WA MATAIFA.

Image
 Brass Bendi ikiingia katika Uwanja wa Mashujaa Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam wakati wa Sherehe za Maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Walinda Amani wa Umoja wa Mataifa inayoadhimishwa kila Mwaka tarehe 29 Mei.  Juu na chini ni Baadhi ya Mabalozi, Maafisa wa Ubalozi, Wakuu wa vitengo mbalimbali vya Mashirika ya Umoja wa Mataifa, Wanadiplomasia, Maafisa wa Serikali na Maafisa kutoka jeshi la ulinzi la Wanachi wa Tanzania (JWTZ).  Baadhi ya Wanajeshi wa Kulinda Amani wa Umoja wa Mataifa katika maadhimisho hayo.  Baadhi ya Wanafunzi kutoka Shule ya Sekondari Benjamini Mkapa ya jijini Dar es Salaam.     "Mungu Ibariki Afrika, Wabariki Viongozi Wote.......!!!   Juu na chini  Mgeni rasmi Naibu wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mh. Mahadhi Juma Maalim akijongea na kuweka shada la maua katika mnara wa kumbukumbu ya mashujaa.     Naibu Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Kazi Duniani (ILO) hapa nchini Bibi. Hopolang Phororo akiweka Shada la Maua k

FARU WA JK AWANG'OA VIGOGO MALIASILI

WAZIRI wa Maliasili na Utalii, Balozi Khamis Kagasheki ameanza kutekeleza kwa vitendo kauli yake ya kuisafisha Idara ya Wanyamapori baada ya kuwasimamisha kazi wakurugenzi wanne na askari 28 wa Hifadhi ya Taifa Serengeti, Mara ili kupisha uchunguzi wa tukio la kuuawa kwa faru wawili na kung’olewa pembe. Faru hao ni miongoni mwa watano ambao Rais Jakaya Kikwete aliwapokea wakitokea Afrika Kusini, Mei 21, 2010 lakini Desemba 21, mwaka huo faru dume aitwaye george aliuawa na pembe zake zilinaswa Mwanza. Faru wengine wanne walipewa majina ya cleo, ethna, lunnar na dume pekee aliyebaki, benj. Wakati akipokea faru hao waliogharimu Sh7.5 bilioni kuanzia ununuzi hadi kuwasafirisha hadi nchini, Rais Kikwete alisema: “Afrika Kusini imeongeza uwezo kwa Tanzania kwa kuleta faru hao weusi na ongezeko hilo ni la manufaa kwa taifa. Hivyo, tutaimarisha huduma zao na ulinzi utakuwa wa kipekee zaidi yangu mimi.” Lakini tofauti na ulinzi huo alioahidi Rais, kumekuwa na taarifa za kua

MAGAZETI YA LEO JUMATANO

Image