Posts

HABARI ZA MAGAZETI YA LEO JUMAMOSI, JULY 25

Image
. . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .

Kajala afungukia kuingia kwenye siasa

Image
CHANZO:GPL Staa wa sinema za Kibongo, Kajala Masanja ‘Kay’ amefungukia kuingia kwenye siasa kuwa ni bora abaki kwenye upenzi na chama fulani kwani hawezi kugombea.   Akizungumza juzikati, Kajala alisema kuwa, japokuwa wasanii wengi wakiwemo wa tasnia ya filamu Bongo, wamekuwa wakichukua fomu za kutaka kugombea nafasi mbalimbali za udiwani na ubunge lakini kwake hafikirii kitu kama hicho. “Mimi siasa siiwezi kabisa, kifupi haipo kwenye damu ndiyo maana unaona wenzangu wote wamechukua fomu za kugombea mimi wala sijajitokeza kuchukua,” alisema Kajala.

Mwigizaji mwenye jina kubwa Riyama Ally Alilia Ndoa!

Image
chanzo: GL Mwigizaji mwenye jina kubwa ndani ya sanaa ya maigizo Bongo, Riyama Ally amekiri kutamani maisha ya ndoa huku akishikilia alichokisema ‘nasubiri wakati wa Mungu’.     Akizungumza na  Gazeti la  Amani  kwa njia ya simu hivi karibuni, msanii huyo mwenye sifa za kuvaa uhusika wa huzuni na kulia katika filamu nyingi, alisema akiwa mwanamke aliyekamilika, anahitaji kuwa na mume wake katika ndoa takatifu lakini akaweka wazi kuwa kwa sasa ana mchumba ambaye anamuomba Mungu usiku na mchana ili awe mumewe.   “Kila mtu aliyekamilika anahitaji maisha ya ndoa, hakuna kitu chenye heshima katika maisha ya binadamu kama kuwa na ndoa na kuishi kwa amani, lakini kila kitu hupangwa na Mungu. Kiukweli kabisa natamani sana ndoa, nina mchumba ambaye namuomba Mungu amfanye kuwa mume wangu,” alisema Riyama.

SIMIYU EXPRESS LAPATA AJALI MKOANI DODOMA JULAI 22, 2015

Image
Taarifa kutoka mkoani Dodoma zinasema zaidi. Abiria 20 wamefariki dunia usiku huu, huku zaidi ya abiria 40 wakijeruhiwa vibaya baada ya basi la kampuni ya SIMIYU EXPRESS walilokua wakisafiria kutoka Mwanza kwenda DSM kupasuka tairi na kuacha njia na kugonga mbuyu na kisha kupinduka. Taarifa zinasema ajali hiyo ni mbaya sana kuwahi kutokea mkoani Dodoma, hadi hivi sasa bado kuna miili haijatolewa kwenye mabaki ya basi hilo kutokana na kuharibika vibaya na kubaki mithili ya nyama. MWENYEZI MUNGU AZILAZE MAHALA PEMA PEPONI ROHO ZA MAREHEMU NA KUWAPA NGUVU FAMILIA ZOTE ZA MAREHEMU AMEEN.

MAGAZETI YA LEO JUMATANO, JULY 22 YAPO HAPA

Image
 

MAGAZETI YA LEO JUMANNE, JULY 21

Image