WATUMISHI WA UMMA SHEREHE ZA MWENGE SIMIYU WAJITOKEZA KWA WINGI KUSAJILIWA VITAMBULISHO VYA TAIFA
Baadhi ya Watumishi wa Umma wakiendelea kupata huduma ya usajili na Utambuzi katika viwanja vya Sabasaba ambako maonesho ya kilele cha mbio za Mwenge wa Uhuru yanafanyika. Wakati wa zoezi hilo mbali na kjaza fomu za maombi ya Vitambulisho, watumishi hao wamepata fursa ya kupigwa Picha, kuchukuliwa alama kumi (10) za vidole pamoja na saini ya Kielektroniki na hivyo kuwa wamekamilisha taratibu zote muhimu za usajili Mmoja wa Watumishi akiendelea na taratibu za usajili na kuchukuliwa alama za kibaiolojia wakati wa usajili watumishi wa Umma, zoezi linaloendelea mkoani Simiyu Mmoja wa Maafisa Usajili wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa ofisi ya Wilaya ya Bariadi (mwemye kofia nyeupe), akiendelea kuingiza taarifa za mmoja wa Watumishi wa Umma aliyejitokeza kusajiliwa wakati zoezi la Usajili watumishi wa Umma likiendelea mkoani Simiyu. Wengine waliomzunguka ni Watumishi kutoka Idara, Taasisi na Wizara za Serikali wakiendelea kusubiria huduma hiyo ...