SEMINA SIKU YA MSANII KUFANYIKA KESHO
SEMINA ya wasanii mbalimbali iliyoandaliwa na Kamati ya Siku Ya Msanii itafanyika kesho Alhamisi katika ukumbi wa Makumbusho ya Taifa Mjini Dar es Salaam. Ofisa Uhusiano wa Siku Ya Msanii, Petter Mwendapole alisema maandalizi yote kwa ajili ya semina hiyo yamekamilika na kwamba wasanii 400 mpaka jana walikuwa wameshajiandikisha. “Lengo letu ni kuwaelimisha wasanii katika kazi zao, lakini pia kuweza kuwapa nafasi ya kupata mafunzo yatakayowasaidia uzeeni wakati ambapo hawatakuwa wakifanya tena sanaa,” anasema. Mada zitakazowasilishwa ni pamoja na Urasimishaji wa Tasnia ya Sanaa nchini itakayowasilishwa na mtaalamu kutoka Mamlaka ya Mapato nchini (TRA) na Umuhimu wa hifadhi ya jamii kwa wasanii itakayowasilishwa na Mfuko wa Pensheni wa PSPF. “Mada hizi zimelenga kuongeza uelewa wa wasanii kuhusu umuhimu na ushiriki wao katika sekta ya hifadhi ya jamii na vilevile umuhimu wa kurasimisha sekta ya sanaa nchini. Wasananii kama wada