Posts

SABBY: BOB JUNIOR AMENIBADILISHA MAVAZI

Image
Na Imelda Mtema MSANII anayekuja kwa kasi katika tasnia ya Filamu Bongo, Sarbrina Omary ‘Sabby Angel’ amefunguka kuwa  mwanamuziki, Rummy Nanji ‘Bob Junior’ ambaye kwa hivi sasa ndiye mpenzi wake amembadilisha mavazi yake aliyokuwa akivaa awali kabla hawajawa pamoja. Msanii anayekuja kwa kasi katika tasnia ya Filamu Bongo, Sarbrina Omary ‘Sabby Angel’ akipozi. Akizungumza na Amani, Sabby alisema kuwa mpenzi wake huyo mara nyingi anapenda ajitande nguo na kuwa mtoto wa Kiislamu kama asipokuwa katika ishu za kurekodi kwani anaamini kuwa binti wa Kiislamu anapaswa kuvaa kiheshima. Mtoto ‘Sabby Angel’ akiwa na Nanji ‘Bob Junior’. “Nimekamatika sana, yale mavazi yangu ya awali nimeambiwa ‘stop,’ tukiwa katika mazingira ya kawaida ni lazima nijitande na nionekana haswa ni mtoto wa Kiislamu,” alisema  Sabby.

MAGAZETI YA LEO ALHAMIS, NOVEMBER 27 YAPO HAPA

Image