Posts

MAGAZETI YA LEO IJUMAA,FEBRUARY 19

Image

Waziri aagiza kusitishwa mkataba wa Mkurugenzi TCRA na kusimamisha wengine 2

Waziri wa Ujenzi wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Makame Mbarawa ameagiza Bodi ya Wakurugenzi wa Mamlaka ya Mawasiliano nchini, TCRA, kusitisha mara moja mkataba wa Mkurugenzi wa Idara ya Sheria wa mamlaka hiyo, Elizabeth Nzagi, kwa kushindwa kusimamia ugungwaji wa kifaa cha kufuatilia mapato ya simu ya ndani katika mitambo ya kuchunguza mapato katika mitandao ya simu (TTMS). Waziri Mbarawa amesema kutokufungwa kwa kifaa hicho kumeisababishia serikali hasara ya shilingi bilioni 400/= hivyo ameiagiza pia bodi hiyo ya TCRA kuwasimamisha kazi mara moja, Kaimu Mkurugenzi anayesimamia mfumo wa uhakiki na usimamiaji huduma za mawasiliano, mhandisi Sunday Richard na Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Sheria, Modestus Ndunguru ili kupisha uchugnuzi dhidi ya uhusika wao katika kusababisha kifaa hicho kutokufungwa. Aidha, Waziri Mbarawa ametoa onyo kali kwa Mkurugenzi Mkuu wa TRCA, Ally Simba kwa kutokuwa makini katika utendaji huo huku akimwagiza kuhakikisha kuwa kifaa hicho kinafungwa ndani

Nyumba za kifahari 160 Moshi kubomolewa

Nyumba za kifahari zaidi ya 160 za vigogo wa taasisi za Umma na wastaafu katika Manispaa ya Moshi mkoani Kilimanjaro zinatarajiwa kubomolewa kutokana na kujengwa maeneo ya hifadhi ya vyanzo vya maji. Nyumba hizo zimejengwa ndani ya meta 60 katika mto Karanga kuanzia eneo la Shanty Town na mto Rau huku nyingine zikijengwa katika vyanzo vya maji kata ya Njoro. Miongoni mwa nyumba zinazotajwa kujengwa ndani ya mita 60 ni za kigogo mmoja mstaafu wa Jeshi la Polisi, wafanyabiashara mashuhuri na nyingine ujenzi wake ukianza. Akizungumza kwa niaba ya mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Moshi, Jeshi Lupembe, Ofisa Mipango Miji wa Halmashauri, Speratus Rutagenya, amethibitisha kuanza kwa mchakato huo. “Zoezi la kwanza lilikuwa ni ku- identify (kutambua) watu walioingia ndani ya meta 60 na tumebaini nyumba zaidi ya 100 mto Karanga na nyingine 60 kule mto Rau na Njoro.”amesema. Ofisa Mipangao miji huyo amesema zoezi hilo limeingia hatua ya pili ambayo ni kuwabaini kwa majina wamil

BREAKING NEWS: MATOKEO YA KIDATO CHA NNE 2015 YATANGAZWA RASMI.

Image
BOFYA HAPA: MATOKEO YA KIDATO CHA NNE 2015 BOFYA HAPA  MATOKEO YA QT

WAZIRI WA AFYA MH. UMMY MWALIMU NA NAIBU WAKE WATEMBELEA HOSPITALI YA TAIFA MUHIMBILI KUKAGUA

Image
  Dk.Stanslaus Ntiyakunze (aliyenyoosha mkono) akiwaonyesha mawaziri namna jengo linavyokarabatiwa ikiwemo miundombinu yake inavyotakiwa kuwa pindi litakapokamilika ikiwemo suala la mfumo wa maji safi na maji taka. Kuliwa kwake ni Naibu Waziri wa Afya Dk Hamisi Kigwangalla wengine Kaimu Mkurugenzi wa hospitali hiyo ya Muhimbili, Prof. Laurance Masaru (kushoto) na Waziri wa Afya, Mh. Ummy Mwalimu (katikati). Mawaziri wa Serikali ya awamu ya tano chini ya Rais John Pombe Magufuli wameendelea kufanya kile ambacho wananchi wanataka ikiwemo suala la kutumikia wananchi ambapo mapema leo, Februari 17, Mawaziri wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mh. Ummy Mwalimu na Naibu wake, Dk. Hamisi Kigwangalla wameweza kutembelea Hospitali ya Taifa Muhimbili kwa lengo la kukagua majengo likiwemo lile aliloagiza Rais kuwa litumike kuwa wodi ya akina mama. Mawaziri hao wamefika Hospitali hiyo ya Taifa majira ya mchana na kisha kupokelewa na wenyeji wao akiwemo Kaimu