MRADI WA KUKUZA TEKNOLOJIA KUPITIA WATOTO XPRIZE WAZINDULIWA DODOMA
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi, Profesa Simon Msanjila (kulia) akitoa hotuba ya ufunguzi wa mradi wa kukuza teknolojia kupitia watoto XPRIZE uliofanyika mjini Dodoma mwishoni mwa wiki. Kutoka kushoto ni Mkurugenzi Mwandamizi wa Uendeshaji kutoka Taasisi ya XPRIZE, Matt Keller, Kaimu Mkurugezi wa Elimu ya Msingi wa Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Kassim Kaoneka na Mkuu wa Ofisi na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) nchini, Bi. Zulmira Rodrigues. (Picha na Modewjiblog ) Kwa kutambua uwezo walionao watoto katika kubuni vitu mbalimbali, Taasisi ya XPRIZE iliyo na makazi yake nchini Marekani, imezindua mradi wa XPRIZE nchini ambao utahusisha watoto ambao hawapo shuleni ukiwa na malengo ya kukuza teknolojia ya dunia kwa kutumia uwezo walionao watoto wa miaka 5-12. Akielezea mradi huo, Mkurugenzi Mwandamizi wa Uendeshaji kutoka Taasisi ya XPRIZE, Matt Kelle