AY NA SEAN KINGSTON NDANI YA COLLABLE


Ambwene Yesaya (AY) kwa wakati huu yupo mjini Mombasa akisubiri kupiga Show katika maadhimisho ya Siku ya Mashujaa wa Nchini Kenya, lakini Ishu nayotaka kuzungumzia hapa ni kuhusiana na Collabo waliypanga Kupiga A.Y na Msanii wa Kimataifa Sean Kingston, Kama unakumbuka A.Y aliwahi kusema miezi ya Kumi au Kumi na moja atachomoka kuelekea Katika jiji la Miami nchini marekani, Kukutana na Sean Kingston, So Gwafara Gwafara ilimvutia wire, ili kujua Safari hiyo ipo ama ni Magumashi.


A.Y: Baada ya kutoka huku Mombasa Safari inayofuata ni ya kwenda Miami nchini Marekani, na tayari nimesha rekodi ngoma tatu, ambazo nitakwenda kumskilizisha Kingston so yeye atachagua ipi ambayo ipo mzuka kwake kutupia Vocal, lakini pia niko tayari kukaa nae chini kutunga Idea mpya ya wimbo kama hizi hazitomvutia.

255: Umesema umefanya Ngoma, Je Ngoma hizo umepigia Studio gani, na kuna msanii yeyote kutoka Bongo au Afrika Mashariki uliyemshirikisha kwenye Hizo ngoma?

A.Y: Ngoma hizo nimepiga chini ya Mtu mzima Producer Hermy B (B-Hits) na ndani yake sijamshirikisha msanii yeyote.

Comments

Popular posts from this blog

PATA UKWELI KUHUSU MWANAMALUNDI, MTU WA MAAJABU ALIYEWAHI KUTOKEA KATIKA HISTORIA YA KABILA LA KISUKUMA