TRENI YA KWENDA KIGOMA YAANZA

WAZIRI wa Uchukuzi, Omary Nundu amezindua safari ya treni ya pili inayosimamiwa na Kampuni ya Reli nchini (TRL) Kwenda Mkoa wa Kigoma kufuatia shida ya usafiri inayowakabili wakazi wa mkoa huo. Kuzinduliwa kwa treni hiyo kunatarajiwa kupunguza adha ya usafiri inayowakabili wakazi wa mkoa huo kwa kipindi kirefu sasa.
JE HUDUMA HII NI KWA SIKUKUU TU?
Akizungumza na baadhi ya abiria waliokuwa ndani ya treni hiyo jana,Waziri Nundu alisema kuzinduliwa kwa treni hiyo kutawasaidia wananchi kwenda kusheherekea sikukuu ya mwaka mpya ambapo Serikali imeamua kuruhusu treni hiyo ianze kazi ili kusafirisha abiria wanaopenda kwenda kula sikukuu ya mwaka mpya katika mikoa ambayo treni hiyo inapita.

STESHENI YA MWANZA, ZAIDI YA KUSAFIRISHA MIZIGO, KITUO HIKI HAKIJATOA HUDUMA YA USAFIRI KWA ABIRIA TANGU ZILIPOSITISHWA HUDUMA ZA TREN.
Hata hivyo wakati Nundu akizindua safari ya treni hiyo ilibainikia kwamba menejimenti ya Shirika la Reli nchini (TRL) inayongozwa na wawekezaji kutoka India hawakufurahishwa na hatua ya waziri huyo kuzindua safari hiyo. “Hii safari ni kiini macho kwa sababu wawekezaji hawaipendi na wameahidi kuisitisha baada ya sikukuu ya mwaka mpya” alisema mmoja wa wafanyakazi wa TRL huku akiomba jina lake lihifadhiwe.

Usafiri wa treni umezidi kudorora kila kukicha huku msongamano wa abiria ukizidi kuongezeka ndani ya treni kiasi cha kusababisha kero kwa abiria.

Comments

Popular posts from this blog

PATA UKWELI KUHUSU MWANAMALUNDI, MTU WA MAAJABU ALIYEWAHI KUTOKEA KATIKA HISTORIA YA KABILA LA KISUKUMA