Posts

Showing posts from 2013

HII NDIO REPOTI ILIYOWAONDOA MADARAKANI MAWAZIRI WANNE

TAARIFA YA KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA ARDHI, MALIASILI NA MAZINGIRA KUHUSU TATHMINI YA MATATIZO YALIYOTOKANA NA OPARESHENI TOKOMEZA ; 1.0 UTANGULIZI Mheshimiwa Spika, wakati Bunge likijadili hoja ya kuahirisha shughuli za Bunge ili kujadili jambo muhimu la dharura kwa mujibu wa Kanuni ya 47 ya Kanuni za Kudumu za Bunge, Toleo la 2013, iliyowasilishwa na Mhe. Said Nkumba, Mbunge wa Sikonge kuhusu Mgogoro kati ya Wafugaji na Wakulima, Hifadhi na Uwekezaji, Mheshimiwa Spika alitoa Uamuzi ‘Speakers Ruling’ kuwa Kamati ya Ardhi, Maliasili na Mazingira ishughulikie kazi ya kutathmini na kuangalia jinsi Mpango wa Kupambana na Majangili ulivyopangwa na kutekelezwa na Serikali kupitia ‘Operesheni Tokomeza’. Kwa mujibu wa kumbukumbu za Taarifa Rasmi za Bunge za tarehe 1 Novemba 2013, wakati Bunge likihitimisha Hoja ya Kuairisha Shughuli za Bunge, Mhe. Spika alitoa uamuzi ufuatao:- …Kamati ile ya kawaida ya Maliasili itaendelea na kazi yake ya kufanya tathmini ya kuangalia jins...

JE USHAWAHI KUFIKIRIA JINSI YA KUPAMBANA NA VYETI FEKI, WILHELM ANA JIBU TUMPIGIE KURA

#‎ LETSVOTE‬ FOR OUR TANZANIAN TALENTED BROTHER IN ICT, Wilhelm Caspar Oddo AMBAYE ANASHIRIKI KATIKA SHINDANO LA KUTAFUTA APPLICATION BORA ZITAKAZO SAIDIA JAMII NA TAIFA KWA UJUMLA, APPLICATION HII "ACADEMIFY" NI MAHUSUSUSI KATIKA KUPAMBANA NA WANAOFORGE VYETI VYA ELIMU, KWA KUSHIRIKIANA NA NECTA,TCU KUPITIA APP HII HAINA HAJA YA MWAJIRI KUBEBA VYETI KUTOKA MIKOANI NA KWENDA NAVYO BARAZA KUVIHAKIKI!! KWA MAELEZO ZAID CLICK HIYO LINK CHINI NA ITAKUPA MAELEZO YA KUTOSHA JUU YA P ROJECT HII MAELEKEZO JINSI YA KUVOTE http://ideas.makingallvoicescount.org/a/dtd/Academify/12234-26650 ... bofya hapo halafu utaona project inaitwa Academify. Kunasehemu pameandikwa I Agree na ukibonyeza utaulizwa unataka ku log in kwa kutumia nini? Facebook, yahoo, twitter, gmail nakadharika. chagua moja na ingiza user name yako na password then bonyeza I Agree tena. Academify ideas.makingallvoicescount.org Academify ideas.makingallvoicescount.org

PICHA KALI 50 KUTOKA KATIKA MAHAFARI YA 15 YA CHUO CHA SAUT HIZI HAPA.

Image
Awali ya yote napenda kutoa shukrani zangu za dhati kwa Mwenyezi Mungu mwingi wa rehema kwa Baraka kwa kuweza kunisimamia katika safari yangu ya kimasomo iliyochukua miaka mitatu na kuhitimishwa hapo jana tarehe 30 November 2013 kwa kutunukiwa Shahada ya Mahusiano ya Umma na Masoko(Bachelor Degree in Public Relations and Marketing)kutoka katika chuo cha Mt. Agustino ( SAUT) na kuwa miongoni mwa wanafunzi 649 kutoka katika program hii tuliotunukiwa jana.  Shahada hii niliyotunukiwa nina ielekeza maalum kwa hayati Mama yangu, Godriver Poti ambaye ametangulia mbele ya haki miaka 4 iliyopita, kila mara alinihusia umuhimu wa elimu na alitamani kuniona mwanaye nafikia hatua hii niliyofikia leo lakini yote tunamuachia muumba mwenyewe kwani kila nafsi itaonja mauti basi nasi tupo safarini tuzidi kujiweka tayari na kufanya yale mazuri yanayompendeza muumba.  Kwenye kila safari hakukosi vikwazo mpaka nafikia hatua hii ya kutunukiwa shahada hii basi vikwanzo ni vingi nilivyovipitia...