PICHA KALI 50 KUTOKA KATIKA MAHAFARI YA 15 YA CHUO CHA SAUT HIZI HAPA.

Awali ya yote napenda kutoa shukrani zangu za dhati kwa Mwenyezi Mungu mwingi wa rehema kwa Baraka kwa kuweza kunisimamia katika safari yangu ya kimasomo iliyochukua miaka mitatu na kuhitimishwa hapo jana tarehe 30 November 2013 kwa kutunukiwa Shahada ya Mahusiano ya Umma na Masoko(Bachelor Degree in Public Relations and Marketing)kutoka katika chuo cha Mt. Agustino ( SAUT) na kuwa miongoni mwa wanafunzi 649 kutoka katika program hii tuliotunukiwa jana. 

Shahada hii niliyotunukiwa nina ielekeza maalum kwa hayati Mama yangu, Godriver Poti ambaye ametangulia mbele ya haki miaka 4 iliyopita, kila mara alinihusia umuhimu wa elimu na alitamani kuniona mwanaye nafikia hatua hii niliyofikia leo lakini yote tunamuachia muumba mwenyewe kwani kila nafsi itaonja mauti basi nasi tupo safarini tuzidi kujiweka tayari na kufanya yale mazuri yanayompendeza muumba.

 Kwenye kila safari hakukosi vikwazo mpaka nafikia hatua hii ya kutunukiwa shahada hii basi vikwanzo ni vingi nilivyovipitia siwezi kuvitaja vyote hapa lakini jambo la msingi ni kutokata tamaa kwa kile kitu unachokihitaji maishani kifanyike, hivyo work on it, usikate tamaa mapema, pambana mpaka hatua ya mwisho kuna wenzangu ambao wamekata tamaa ya kusoma lakini wana uwezo wa kufanya maajabu katika elimu mfano mzuri ni Ben carson mwandishi wa kitabu cha “Think Big” ambaye alikuwa ni mwanafunzi aliyekuwa akifanya vibaya sana darasani lakini mama yake aliweza kumbadilisha kisaikolojia na kuondokana na mawazo magando kwamba yeye si chochote mbele ya wenzake kwa kuwa na ufaulu mdogo sana na kutokuwa na confidence, lakini leo hii anaheshima kubwa sana duniani kwa kufanya maajabu ya kufanya operation mbalimbali za kuachanisha watu walioshikana tena sehemu hatarishi kama kichwani, haya ni baadhi ya maneno yake “Everyone in the world worth being nice to. Because God never creates inferior human beings, each person deserves respect and dignity” hivyo hakuna mtu ambaye hana uwezo wa kufanya jambo lolote lile na akafanikiwa. 

Napenda kutoa pongezi zangu za dhati kabisa kwa waadhili mbalimbali wa chuo kikuu cha Mt. Augustino kwa moyo wao wa kutufundisha bila kuchoka na kutupatia ushauri mbalimbali kila mara akiwemo Supervisor wangu wa Research. Prudence Rwehabura, H.O.D Cezalia Mwidima, Albert Tibaijuka,Denis Mpagaze, Mandu Lila, Mrisho,Madam Sakina na wengine wengi, lakini pia na wafanyakazi wote wa jumuia ya Mt. Augustino. 

 Pia napenda kuwashukuru sana Members wa group na 35 wa BAPRM kwa moyo wao wa kujituma katika kufanya kazi mbalimbali za shule lakini pia kwa upendo wao tuliishi kama wana familia,na wanafunzi wote wa BAPRM 2010- 2013 mmekuwa msaada mkubwa sana kwangu, pia familia yangu kwa kuonyesha ushirikiano wa kutosha katika wakati wote wa masomo yangu,haitakuwa vema kuwasahau wanachama wa SSPRA hawa nao napenda kuwashukuru sana na mwisho kabisa ni kwa members wote wa Gosheni Hostel mahali ambapo ubavu wangu ulikuwa ukipumzika katika kipindi cha miaka 3.

















































Comments

Popular posts from this blog

PATA UKWELI KUHUSU MWANAMALUNDI, MTU WA MAAJABU ALIYEWAHI KUTOKEA KATIKA HISTORIA YA KABILA LA KISUKUMA