MAONYESHO YA NANE YA BIASHARA YA AFRIKA MASHARIKI KUANZA RASMI KESHO KATIKA VIWANJA VYA NYAMAGANA JIJINI MWANZA
Maonyesho ya NANE ya Biashara
kwa nchi za Afrika Mashariki (EastAfrica Tarade Fair) yanayoandaliwa na TCCIA mkoa
wa Mwanza yanataraji kuanza rasmi tarehe 30/08/2013 mpaka tarehe 8/09/2013
katika viwanja vya Nyamagana jijini Mwanza yakihusisha makampuni mbalimbali ya
bidhaa ndani na nje ya nchi.
Licha ya Maonyesho hayo kutumika
kama jukwaa kwa makampuni mbalimbali ya ndani
na nje kuonyesha shughuli na huduma wanazozitoa pia itakuwa ni fursa ya
yatatumika kama fursa ya kuanzisha mitandao katika dhana ya usambazaji wa bidhaa.
Mbali
na kushirikisha wadau wa biashara, viwanda na kilimo wa nchi za Afrika
Mashariki pia maonyesho hayo yatashirikisha makampuni ya wadau wa nchi
za Misri, Singapole na China.
Bidhaa na huduma
zisizoruhusiwa kwenye maonyesho hayo ni pamoja na Silaha za aina zote, Risasi,
Mizinga (Bidhaa za kivita), pamoja na huduma za masuala ya kisiasa na
kidini kwani ni Biashara na Uwekezaji tu ndiyo umezingatiwa na kamati ya
maandalizi
Maonyesho hayo yatazinduliwa nnamo tarehe 2 September 2013, ambapo mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Injinia Evarist Ndikilo.
Maonyesho hayo yatazinduliwa nnamo tarehe 2 September 2013, ambapo mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Injinia Evarist Ndikilo.
Comments
Post a Comment