Posts

Showing posts from October, 2016

MAGAZETI YA LEO TANZANIA OCTOBER 27

Image
TANZANIA

TAARIFA KUTOKA TCRA JUU YA SIM CARD

Image
 

UCHAGUZI WA RAIS CONGO WAAHIRISHWA HADI APRILI 2018

Image
Vyama vinavyounda muungano unaotawala Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo na vyama vyengine vidogo vimekubaliana kuchelewesha uchaguzi wa mwezi ujao hadi Aprili mwaka 2018 hatua itakayoyakasirisha makundi ya upinzani. Kundi kuu la upinzani nchini Congo halikuweza kupatikana mara moja kuzungumzia uamuzi huo lakini tayari limeitisha mgomo wa taifa hapo Jumatano kumshinikiza Rais Joseph Kabila kuachia madaraka mwishoni mwa muhula wake hapo mwezi wa Disemba. Kundi hilo kuu la upinzani linaloongozwa la Etiene Tshisekedi limesusia mazungumzo ya usluhishi wa kitaifa kwa hoja kwamba ni ni njama za Rais Kabila kuendelea kun'gan'gania madaraka. Mwezi uliopita madazeni ya watu waliuwawa wakati wa maandamano ya siku mbili mjini Kinshasa kupinga mipango ya kuchelewesha uchaguzi huo kwa kile serikali inachosema matatizo ya kifedha na vifaa katika kuwaandikisha mamilioni ya watu katika nchi kikubwa ya kimaskini. Muda zaidi kwa dafatri la wapiga kura Vyama hivyo vimekubaliana hapo

JESHI LA IRAQ LAANZA OPERESHENI KUIKOMBOA MOSUL

Image
Wanajeshi wa Iraq, wakijiandaa na mapambano Waziri Mkuu wa Iraq Haider Al Abadi amesema operesheni za kijeshi zimeanza kuurejesha mji wa Mosul, ambao ni wa pili kwa ukubwa. Mji huo kwa sasa unashikiliwa na wapiganaji wa Islamic State. Tangazo hilo limetolewa usiku wa manane kupitia Televisheni ya nchi hiyo. Mji wa Mosul ulishikiliwa na wapiganaji hao wa IS, wakati wa mapigano makali na kushuhudiwa eneo kubwa magharibi mwa Iraq, likichukuliwa na wapiganaji. Eneo kubwa la ardhi kwa sasa limerudishwa, na mji wa Mosul umebakia kuwa ngome ya mwisho ya wapiganaji hao. Ndege za Kivita za Marekani zimekuwa zikifanya mashambulizi katika mji huo, huku mjumbe maalumu wa Marekani katika Ushirika unaopambana na IS, brett McGurk akiandika katika mtandao wa Twitter kwamba Marekani inajivunia kuiunga mkono Iraq. Kwa miezi kadhaa Iraq imekuwa ikijiandaa kufanya mashambulizi makubwa. Huku Mashirika ya haki za Binadamu yakionya kuwa raia wengi watakumbwa na maafa.  BBC

WAZIRI MKUU AAGIZA MAPATO YA HOSPITALI YA NACHINGWEA YAKUSANYWE KWA NJIA YA KIELEKTRONIKI

Image
! WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ametoa mwezi mmoja kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Nachingwea, Bw. Bakari Mohammed kuhakikisha hospitali ya wilaya hiyo inakusanya mapato kwa kutumia mfumo wa kielektroniki. Ametoa agizo hilo leo (Jumapili, Oktoba 16, 2016) wakati alipotembelea hospitali ya wilaya ya Nachingwea akiwa kwenye ziara yake ya kikazi ya siku tatu mkoani Lindi. Waziri Mkuu amesema Serikali ilishaagiza taasisi zote za umma kutumia mfumo wa kielektroniki katika ukusanyaji wa mapato kwa lengo la kudhibiti mianya ya upotevu wa fedha za umma. Amesema taasisi ambazo tayari ziameanza kutumia mfuko huo katika ukusanyaji wa mapato zimeweza kuongeza kiwango cha makusanyo kutoka sh. 300,000 hadi milioni nne kwa siku. Pia aliwaagiza viongozi wa wilaya hiyo kuendelea kuwahamasisha wananchi kujiunga na Mfuko wa Afya ya Jamii (CHF) ambao utawawezesha kupata huduma ya matibabu bure katika kipindi cha mwaka mzima. Akizungumzia kuhusu matibabu kwa wazee, Wa

MAGAZETI YA LEO ALHAMIS ,OCTOBA 13

Image