JESHI LA IRAQ LAANZA OPERESHENI KUIKOMBOA MOSUL
Wanajeshi wa Iraq, wakijiandaa na mapambano
Waziri Mkuu wa Iraq Haider Al Abadi amesema operesheni za kijeshi zimeanza kuurejesha mji wa Mosul, ambao ni wa pili kwa ukubwa.
Mji huo kwa sasa unashikiliwa na wapiganaji wa Islamic State.
Tangazo hilo limetolewa usiku wa manane kupitia Televisheni ya nchi hiyo.
Mji wa Mosul ulishikiliwa na wapiganaji hao wa IS, wakati wa mapigano makali na kushuhudiwa eneo kubwa magharibi mwa Iraq, likichukuliwa na wapiganaji.
Eneo kubwa la ardhi kwa sasa limerudishwa, na mji wa Mosul umebakia kuwa ngome ya mwisho ya wapiganaji hao.
Ndege za Kivita za Marekani zimekuwa zikifanya mashambulizi katika mji huo, huku mjumbe maalumu wa Marekani katika Ushirika unaopambana na IS, brett McGurk akiandika katika mtandao wa Twitter kwamba Marekani inajivunia kuiunga mkono Iraq.
Kwa miezi kadhaa Iraq imekuwa ikijiandaa kufanya mashambulizi makubwa. Huku Mashirika ya haki za Binadamu yakionya kuwa raia wengi watakumbwa na maafa. BBC
Comments
Post a Comment